Posts

‘Vita’ ya Alikiba na Samatta Imefika Pabaya

Image
NAHODHA wa Timu ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars na Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta ameingia kwenye vita ya ki-sport na msanii wa Bongo Fleva, Alikiba inayotarajiwa kufanyika Juni 9, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na miundombinu katika mashule. Samatta amesema mechi hiyo itakuwa itamuhusisha yeye na marafiki zake dhidi ya Alikiba na marafiki zake pia. “Itakuwa mechi ya hisani kama zilizo nyingine ambazo zimekuwa zikifanywa na wachezaji wakubwa, hii ni kati ya Samatta 11 na Alikiba 11, nitachagua marafiki zangu na Kiba atachagua marafiki zake. Nataka nifanye moja lakini itakuwa na radha tofauti, kwani timu pinzani itakuwa ya Alikiba. “Ok, nimepewa jukumu la kuandaa jeshi la maangamizi mchezaji gani ungependa kumuona siku iyo awe wa sasa au wa zamani?” amesema Samatta. Alikiba amesema amefurahi urafiki wake na Samatta kuzalisha kitu hicho kizuri huku akiwaomba wapenzi n

DKT ABBASI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO IMARISHENI USHIRIKIANO NA WATENDAJI WA KADA TOFAUTI KUTANGAZA MAFANIKIO YA SERIKALI

Image
MAAFISA Habari na Mawasiliano Serikalini  wametakiwa kujenga timu ya ushirikiano wa pamoja na Wataalamu wa kada mbalimbali waliopo katika maeneo yao ya kazi ili kutangaza vyema mafanikio ya miradi na program zilizotekelezwa na zinazotekelezwa na Serikali. Hayo yamesemwa jana Mkoani Arusha na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya siku tano ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali za Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. Dkt. Abbasi alisema malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa watendaji wote wa Serikali wanakuwa mstari wa mbele katika kuwaletea maendeleo ya haraka  wananchi wake kwani Serikali inajenga nyumba moja, hivyo ni wajibu wa watumishi wote kuungana pamoja katika kusukuma mbele gurudumu hilo hususani katika maeneo ya Mikoa na Halmashauri ambapo Serikali hupeleka kiasi kikubwa

MAGAZETI YA TANZANIA LEO ALHAMISI, MEI 24, 2018

Image
 

Tende, Maji Zinavyofaa Wakati wa Mfungo wa Ramadhani

Image
V YAKULA vinavyofaa kuliwa wakati huu wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vingi, leo tutaanza kuchambua kimoja baada ya kingine, Mbali na Waislamu, uchambuzi huu unawafaa pia wale ambao siyo Waislamu. Chakula kilichozoeleka zaidi kwa futari ni tende. Baada ya kushinda kutwa nzima na Swaumu, kiwango cha sukari ya mwili hupungua na hivyo, kuhitaji kujazilizwa tena. Aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini na hasahasa ubongoni ni glukosi. Mshuko wa sukari walioupata wale ambao hawakula au kunywa kwa kipindi kirefu, unaweza kusababisha ulegevu wa mwili. Pindi sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, viwango vya glukosi ya mwili hujisawazisha vyenyewe na kumfanya mtu aliyefunga asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho. Ingawaje tende, mara nyingi, si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta, na ni chanzo madhubuti cha sukari. Nusu ya sukari zitolewazo na tende ni kwa aj

Hamisa Mobetto afunguka kuhusu kupigwa na mama Diamond

Image
Mwanamitindo Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu taarifa zilizodai kuwa amepigwa na mama mzazi wa Diamond Platnumz, Sanura Kassim ‘Sandra’. Hapo jana katika uzinduzi wa kipindi cha Nyumba ya Imani cha Wasafi TV, Hamisa alipata time ya kuzungumza na waandishi wa habari na kusema jambo hilo ni binafsi zaidi ila kugombana kwa binadamu ni kitu cha kawaida. “Hilo siwezi kuliongelea, yeah!. is too person, is too private, is too family. Hata vikombe kwenye kabati vinagong’ana, so sisi binadamu vinaweza kutokea,” amesema. Alipoulizwa iwapo kwa sasa yeye na mama Diamond wana maelewano mazuri, alijibu; ‘Sina kinyongo na mtu, sina bifu na mtu, mimi am just fine, may be yeye mwenyewe sio upande wangu wa kuweza kuelezea,’. Taarifa za Hamisa kupigwa na mama Diamond zilianza kusambaa Jumatatu ya wiki iliyopita, May 14, 2018 ambapo usiku ya jana yake Hamisa na Diamond walihudhuria katika uzinduzi wa filamu ya Aunt Ezekiel ‘Mama’ na baada ya hapo anadaiwa waliongozana hadi Madale

HEKO RAIS JPM TUKO NYUMA YAKO

Image

Wanaowania Tuzo za Ligi Kuu Bara Msimu wa 2017/18 Yaanikwa

Image
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeanika majina ya wachezaji wanao wania tuzo za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) msimu wa mwaka 2017/18 ambazo zitatolewa Juni 23, 2018 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. TFF imesema kuwa mwaka huu wameongeza tuzo ya mwamuzi bora msaidizi ambayo haikuwepo hapo awali ikiwa na lengo la kuthamini nafasi na mchango wa waamuzi wasaidizi katika mchezo wa soka hapa nchini. Tuzo zitakazotolewa ni za Timu Bingwa, Mshindi wa Pili, Mshindi Tatu, Wanne, Mfungaji Bora, Timu yenye nidhamu, ‘ Under Twenty Player ’, mchezaji bora chipukizi, Mwamuzi bora msaidizi, Mwamuzi bora, Kipa bora na kocha bora, Goli Bora, ‘VPL Best Eleven’, Mchezaji wa heshima huku zawadi zikitarajiwa kutangazwa siku za huvi karibuni. Kamati ya tuzo ya TFF imekamilisha orodha ya wachezaji 30 watakao wania tuzo hizomsimu huu wa mwaka 2017/18. Kwenye majina ya wachezaji 30 waliyo orodheshwa kuwania tuzo hizo watachujwa mpaka kufikia 10 kisha watatu na kuta

Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kulawiti watoto watatu mtwara

Image
Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Mohamedi Kaisi Hamisi mwenye miaka 47 mkazi wa kijiji cha Kawawa mkoani Mtwara, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za ulawiti. Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba mwanaume huyo anatuhumiwa kulawiti watoto watatu wenye miaka 13, 14 na 15, wa shule ya msingi Kawawa, walipokuwa wanatafuta Nazi kwenye minazi iliyopo vichakani baada ya kutoka Kamanda Mkondya amesema kwamba baada ya kuwakuta watoto hao mtuhumiwa aliwatishia maisha kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama katika eneo la Nambonde. Hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwepo baada ya mtuhumiwa kukamatwa (Nassoro Abdala Nyoya, Sharifa Hassani na Julieta Athanas) kwa masikitiko makubwa wameiomba serikali ichukue hatua kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

BREAKING NEWS: KESI YA BABU TALE YAAHIRISHWA, ARUDISHWA MAHABUSU

Image
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, leo amefikishwa katika Mahakama Kuu jijini Dar ambako baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo kesi imeharishwa na Babu Tale atarudishwa mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam. Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi hicho baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

Mambo 8 Usiyoyajua Ndoa ya Kifalme ya Meghan na Prince Harry

Image
Prince Harry Akiwa na Mkewe Rachel Meghan Markle SI kipindi kirefu kimepita tangu watu wengi duniani wajiulize itakuwaje siku ya ndoa ya mwanadada ambaye ni muigizaji maarufu Marekani, Rachel Meghan Markle na mtoto wa Mfalme wa Wales, ambaye pia ni mjukuu wa Malkia Elizabeth II, aitwaye Prince Harry. Wengi walijiuliza ukubwa wa harusi hiyo, mastaa watakaohudhuria watakuwa wamevaa vipi, maharusi watakuwa kwenye muonekano upi, vituko gani vitatokea na mengine mengi! Lakini hayawihayawi hatimaye yamekuwa! Kila kitu kimejulikana baada ya Jumamosi iliyopita, watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kusimamisha shughuli zao kushuhudia tukio hilo la kihistoria, ambapo ndoa ilifungwa kwenye Kanisa la Kifalme la St. George la Anglican na kuhudhuriwa na watu wengi mashuhuri Kama yalivyokuwa mategemeo ya wengi, yapo mambo mengi yaliyojiri kwenye ndoa hiyo. Inawezekana umeyasikia tu lakini huyafahamu kiundani au hujayasikia kabisa. Basi usijali, Risasi Vibes inakumegea kwa

RIPOTI MPYA AFYA YA MZEE MAJUTO INDIA

Image
Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ZIKIWA zimepita siku 19 tangu mkongwe wa vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ apelekwe nchini India kwa matibabu, ripoti mpya ya afya yake imetoka, Risasi Mchanganyiko linayo. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko , Ashraf ambaye alijitambulisha kuwa ni mtoto wa Mzee Majuto alieleza kwamba, kwa sasa afya ya Mzee Majuto inaendelea vizuri, tofauti na alivyokuwa hapa nchini licha ya kwamba bado anaendelea na matibabu. “Kwa sasa baba anaendelea vizuri kwa kweli, tumewasiliana na waliopo naye kule hospitalini India, wanasema hali yake imeanza kutengemaa tofauti na alivyokuwa hapa Bongo. Kwa sasa ni hayo tu, mengine familia itazungumza zaidi baadaye,” alisema Ashraf. MKE WA MAJUTO AFANYA SIRI Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na mke wa Mzee Majuto, Aisha Yusuf ambaye yupo hospitalini na mumewe huko India na kumuuliza kuhusu maendeleo ya mgonjwa ambapo mahojiano yalikuwa hivi; Risasi Mchanganyiko: Habari mama, vipi Mzee Majuto

Mkuu wa Wilaya amwaga machozi kwa kipigo walichopata Wananchi wake

Image
Mkuu wa Wilaya ya Rombo Agnes Hokororo ametoa machozi baada ya kukuta wananchi wa eneo la Samanga katika eneo la Useri kulalamikia jeshi la polisi kushirikiana na majambazi katika kuwapiga pamoja na kuwadai rushwa ili waweze kuachiwa pale wanapokamatwa. DC Hokororo amelaani pia kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mikononi na kumuua jambazi anayetuhumiwa kuwaibia wananchi kijijini hapo.

BABU TALE ARUDISHWA MAHABUSU KISA MIL 250

Image
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale. Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’,  Hamis Taletale ‘Babu Tale’,  jana alikamatwa kwa amri ya mahakama na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo, alirudishwa mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam ili kufikishwa tena katika mahakama hiyo leo. Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi hicho baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi,  katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutu

DAWA ZAVUSHWA KUPITIA MTO WENYE MAMBA MKOANI RUVUMA

Image
  Wakazi wa vijiji vilivyopo kandokando ya mto Ruvuma wilayani Nyasa mkoani Ruvuma na wafanyakazi wa Bobari ya Dawa (MSD), wakisaidia kushusha maboksi yenye dawa na kuyaingiza kwenye mtumbwi baada ya kupelekewa na MSD Kanda ya Iringa leo na baadae kuyapeleka katika Zahanati ya Kijiji cha  Mitomoni .   Maboksi ya dawa yakiingizwa kwenye mtumbwi.   Wakazi wa Kijiji cha Mitomoni wakisubiri mtumbwi ili kuwavusha upande wa pili wa mto Ruvuma.   Dawa zikipelekwa Zahanati ya Mitomoni   Maboksi ya dawa kutoka MSD yakishushwa   Wananchi wakishusha maboksi hayo kutoka katika mtumbwi.   Mkazi wa Kijiji cha Mitomoni Khadija Salum, akizungumzia upatikanaji wa dawa kutoka MSD.   Mkazi wa kijiji hicho, Mbwana Koloma, akizungumzia changamoto ya miundombinu ya barabara na jinsi wanavyopokea dawa kutoka MSD.   Mwenyekiti wa kamati ya Afya wa Kijiji cha Mitomoni Omar Hassan akizungumza wakati wa kupokea dawa hizo. Mmoja wa viongozi wa Kiji