RIPOTI MPYA AFYA YA MZEE MAJUTO INDIA
Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ZIKIWA zimepita siku 19 tangu mkongwe wa vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ apelekwe nchini India kwa matibabu, ripoti mpya ya afya yake imetoka, Risasi Mchanganyiko linayo. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko , Ashraf ambaye alijitambulisha kuwa ni mtoto wa Mzee Majuto alieleza kwamba, kwa sasa afya ya Mzee Majuto inaendelea vizuri, tofauti na alivyokuwa hapa nchini licha ya kwamba bado anaendelea na matibabu. “Kwa sasa baba anaendelea vizuri kwa kweli, tumewasiliana na waliopo naye kule hospitalini India, wanasema hali yake imeanza kutengemaa tofauti na alivyokuwa hapa Bongo. Kwa sasa ni hayo tu, mengine familia itazungumza zaidi baadaye,” alisema Ashraf. MKE WA MAJUTO AFANYA SIRI Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na mke wa Mzee Majuto, Aisha Yusuf ambaye yupo hospitalini na mumewe huko India na kumuuliza kuhusu maendeleo ya mgonjwa ambapo mahojiano yalikuwa hivi; Risasi Mchanganyiko: Habari mama, vipi Mzee Majuto