KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI,SANAA UTAMADUNI NA MICHEZOAMTEMBELEA MWANARIADHA ANAYEHESHIMIKA DUNIANI MZEE JOHN STEVEN AKHWARI NYUMBANI KWAKE MBULU MKOANI MANYARA
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akisalimiana na Mzee John
Steven Akhwari Mwanariadha anayeheshimika Duniani mara baada kwasili
alipomtembelea nyumbani kwake Eneo la Sani mjini Mbulu mkoani Manyara
jana, John Steven Akhwari aliiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki
iliyofanyika Mexco City mwaka 1968
John Steven Akwari aliyekuwa wa
mwisho kumaliza mashindano ya marathon mwaka 1968 Mexico City katika
mioyo ya mamilioni ya watu anakumbukwa kama shujaa ambapo mwaka 2008
katika mashindano ya Olimpiki ya Beijing nchini China miaka 40 baadaye,
Akhwari aliteuliwa kuwa balozi wa heshima wa Olimpiki. Katika mashindano
hayo ya mwaka 1968, Akwari akiwa na umri wa miaka 30 akiiwakilisha
Tanzania alikuwa mwanariadha wa mwisho (57) kumaliza mashindano kati ya
75 walioanza.
Mshindi wa mashindano hayo Mamo
Wolde wa Ethiopia alitumia saa 2:20:26 huku Akhwari akimaliza zaidi ya
saa moja baadaye yaani alitumia saa 3:25:27 kukiwa na watazamaji
wachache uwanjani na jua lilikwisha kuzama. Awali wakati anaanza mbio
hizo, Akwari alianguka na kupata majeraha kwenye goti ikichangiwa kwa
kiasi kikubwa na hali ya hewa ya Amerika ya kati kuwa tofauti na
nyumbani. Wanariadha wenzake walimpita moja baada ya mwingine na hivyo
kukatiza ndoto yake ya kuiletea Tanzania medali ya kwanza kabisa ya
Olimpiki, lakini hakukata tamaa bali alinuia kumaliza hayo mashindano.
Akiwa amefungwa bandeji mguuni
huku akitokwa na damu, Akhwari alitokeza uwanjani saa moja baada ya
mshindi kutangazwa, na kukiwa na watazamaji wachache na waandishi wa
habari na giza likianza kuingia, uwanja ulizizima kuona Akhwari
anachechemea akiwa na maumivu kuelekea mstari wa kumaliza mbio, wengi
waliguswa baada ya kushuhudia tukio hilo. Alipoulizwa na waandishi kwa
nini aliendelea na mashindano baada ya kuumia, aliwajibu kwa utulivu
jibu rahisi “Nchi yangu haikunituma maili zaidi ya 5000 kuanza mbio,
bali kuzimaliza“
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Mbulu Bw. Hudson Kamoga akisalimiana na MZee John Steven Akhwari wakati
alipoongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo aliyemtembelea mzee huyo nyumbani kwake eneo la Sani mjini
Mbulu.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza jambo na Mzee John Steven Akhwari.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Mee John Steven
Akhwari alipokuwa aktoa maelezo kwake kuhusu mbambo mbalimbali
aliyowahi kuyafanya katika masuala ya mchezo wa Riadha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mbulu wakiangalia tuzo mbalimbali ambazo Mzee John Steven
Akhwari kulia aliwahi kutumikiwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mbulu wakionyeshwa mwenge wa Olimpiki ambao Mzee John
Steven Akhwari kulia kutumikiwa jijini Beijing China baada ya
kuukimbiza akiwa Balozi wa Mashindano hayo mwaka 2008.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyeshwa moja ya tuzo
ambayo Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa nchini Uswisi .
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akionyesswa Nisahani ambayo
Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili
Mzee Ali Hassan Mwinyi
Hapa wakionyeshwa vyeti
mbalimbali ambavyo Mzee John Steven Akhwari aliwahi kutunikiwa kutambua
mchango wake katika mchezo wa Riadha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri
ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga wakiwa katika picha ya pamoja na
Mzee John Steven Akhwari mara baada ya mazungumza yao.
Comments
Post a Comment