Posts

DONGOBESH FC YAICHAPA STAND FC YA HAYDOM GOLI 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KURUGENZI CUP 2018

Image
 Mchezaji wa timu ya Dongobesh FC Antipas Vicent akiwa amebebwa juu juu na mchezaji mwenzake mara baada ya kumalizika kwa mchezo katika yake na timu ya Stand FC ya Mjini Haydom ambapo mchezaji huyo ndiye aliyeifungia timu yake goli 1-0 na timu ya Dongobeshi kufanikiwa kuingia nusu fainali katika michuano ya Kurugenzi Cup 2018 linaloandaliwa na Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom.ikidhaminiwa na Kiwanda cha maziwa cha ASAS cha Iringa, na benki za NMB na CRDB.  Wachezaji wa timu ya Dongobash FC wakisikiliza maelezo ya Mmoja wa Waratibu wa michuano hiyo Bw. Phars Nyanda wakati akiwapa utaratibu mara baada ya mchezo huo kumalizika.  Benchi la Ufundi la Timu ya Dongobesh FC likinyanyuka juu na kushangilia mara baada ya kuifunga timu ya Stand FC ya mjini Haydom katika mchezo uliofanyika leo jioni kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Haydom.  Golikipa wa timu ya Stand FC ya mjini Haydo

Ukiwa na sifa hizi, kila mwanaume atatamani kukuoa!

Image
KUOLEWA ni heshima kwa mwanamke. Heshima hiyo inaenda mbali zaidi hadi kuwagusa wazazi wa binti ambaye ataolewa. Wazazi wanatembea kifua mbele pindi binti yao anapoolewa, tena wanafurahia zaidi binti huyo anapoolewa akiwa angali bado hajazaa. Wanamshukuru Mungu kwa binti yao kujitunza. Wanamshukuru binti kwa kuwapa heshima katika familia yao na ndiyo maana siku ya sherehe ya kuagwa (send off) wazazi wanafurahi sana kuagana na binti yao kwa heshima. Hali hiyo huwa inaleta shauku kubwa kwa warembo wengi kutamani kuingia kwenye ndoa. Wengi wanaguswa na rekodi za wanawake wenzao ambao wamejitunza na hatimaye kuwaletea heshima wazazi wao. Kinyume chake, wengi wamejikuta wakijilaumu kwa kushindwa kuleta heshima katika familia zao. Binti umri unaenda, anatamani kuingia kwenye ndoa lakini hapati wa kumuoa. Au mwingine inatokea, anatamani kuolewa lakini anaishia kupigwa mimba na kuachwa. Badala ya kuleta heshima, analeta aibu katika familia yake kutokana na mila na destu

VIDEO QUEEN MBARONI KWA WIZI

Image
M UUZA sura kwenye video za Kibongo ‘Video Queen’ aliyejipatia umaarufu kwa kutupia picha za utupu mitandaoni, Agness Mmasi, yamemkuta mazito, baada ya kuswekwa rumande kwa tuhuma za utapeli Ijumaa linakumegea ishu kamili. Akipiga stori na Ijumaa, chanzo wa kuaminika kilieleza kwamba muuza sura huyo, mpaka juzi (Jumatano), alikuwa bado akisota rumande katika Kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa takribani siku nne. “Mnahabari kamba Agness amedakwa kisa kutapeli nguo maeneo ya Kijitonyama? Kama hamjazidaka ni kamba alichukua kwa mkopo, baadaye akawa anamzungusha mwenye mzigo, mara amtukane hapo ndipo alipodakwa na mpaka sasa anasota nyuma ya nondo,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta anayedaiwa kuwa ndiye mwenye mzigo huo wa nguo ambazo Agness alichikichia nazo, aliyefahamika kwa jina moja la Nyange na alipopatikana alikiri kutapeliwa na mwanadada huyo. “Ni kweli alichukua mzigo wa ngu

Rais Magufuli aibua mapya bandarini

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia Dkt. John Pombe Magufuli, leo amefanya ziara ya kushtukiza bandarini jijini Dar es salaam kukagua matanki ya mafuta ya kula, ambayo yameadimika hapa nchini. Baada ya ziara hiyo na kufanya ukaguzi, Rais Magufuli amebaini kuwa kuna mafuta ambayo yameingizwa nchini huku kukiwa na taarifa za udanganyifu ili kukwepa kodi, yakiwemo mafuta ambayo yameshakamilika (refined oil) na kusema kuwa ni mafuta gahfi (crude oil). Baada ya kugundua hilo Rais Magufuli amewataka wamiliki wa mafuta hayo kulipa ushuru wake unaostahili, pamoja na fine kutokana na udanganyifu walioufanya. "Kwenye bidhaa walizosema ni crude kumbe ni refined oil walipe 25% pamoja na fine, hatuwezi tukawa tunaibiwa kila siku tunahitaji kujenga viwanda vetu, haiwezekani crude oil ukachaji sawa na semi refined, na hii sheria yetu inawezekana kulifanyika mchezo, wabunge walipitisha kitu kingine, kinachojadiliwa kingine, kilicholetwa huku ni kingine, kinachokuja kupi

Magufuli ampandisha cheo baada ya kushtukiza bandarini

Image
Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kumpandisha cheo Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA bandari ya Dar es Salaam Ben Usaje na kuwa Kamishna kamili bandarini hapo ndani ya wiki hii. Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo wakati alipokuwa anazungumza viongozi mbalimbali kwenye bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza kwenye bandari na kusema amefanya hivyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya Ben Usaje katika kusimamia maslahi ya nchi vizuri. "Nawapongeza watu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kazi nzuri mnayoifanya,  Waziri wa Fedha kampeni tu huyu ukamishna kamili kwa sababu amesimamia haki halisi kwaajili ya maslahi mapana ya nchi yetu, najua wanamchukia sana wengine wafanyabiashara lakini waache wakuchukie Mungu anakupenda na watanzania tutaendelea kukupenda kwa hiyo mka-confirm. Katibu Mkuu mkazungum

TAARIFA RASMI YA MAGEREZA KUHUSU KUACHIWA KWA LULU

Image
Taarifa rasmi ya Jeshi la Magereza kuhusu kuachiwa kwa Muigizaji wa Filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye sasa atatumikia kifungo cha nje kumalizia miaka yake miwili aliyohukumiwa kwa kosa la kumuua Steven Kanumba bila kukusudia.

Shamsa Kamjibu Harmonize, Mumewe Kutembea na Wolper

Image
MSANII wa Filamu nchini, Shamsa Ford, amefunguka kuhusu mumewe, Chidi Mapenzi kutajwa na Harmonize kutajwa na Harmonize kwenye orodha ya wanaume waliowahi kutoka kimpenzi na muigizaji mwenzake, Jacqueline Wolper.

BREAKING NEWS: LULU ATOKA GEREZANI .

Image
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imembadilishia adhabu ya kifungo, Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, ambaye kuanzia sasa atatumikia kifungo cha nje. Lulu  Novemba 13 mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake ambaye alikuwa pia mpenzi wake, Steven Charles Kanumba, tukio lililotokea April 7, 2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje, amesema Lulu amebadilishiwa adhabu hiyo kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ambapo atatumikia kifungo cha nje. Amesema pia kwamba, msanii huyo aliachiwa tangu juzi Jumamosi Mei 12, huku akisisitiza kuwa si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, ambayo kisheria inaitwa ‘community service.

Shamsa akiri kuumizwa na Harmonize

Image
Muigizaji wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amekiri kuumizwa na kitendo cha Harmonize kumuhusisha mume wake katika ugomvi wake na ex-girl friend wake, Wolper. Utakumbuka wiki iliyopitia katika kurushiana maneno kati ya Harmonize na Wolper, mume wa Shamsa Ford, Chid Mapenzi alitajwa na Harmonize katika orodha ya wanaume 12 aliodai wametoka kimapenzi na Wolper. Sasa Shamsa amesema si kwa mume wake pekee bali hata mtu wake wa karibu anapozungumzwa kwa ubaya huwa anaumia. “Lazima uumie ukiwa kama binadamu hasa kwa mtu ambaye unampenda sio lazima kwa mume kwa mtu yeyote ambaye unampenda, yupo katika sehemu ya maisha yako lazima ujisikie vibaya,” amesema Shamsa.

Tambua Madhara ya Ulaji wa Chipsi

Image
Chips ni aina ya chakula ambacho hupendwa na watu wengi na pia ni miongoni mwa vyakula vyenye mafuta mengi. chips pia inasemekana ni miongoini mwa vyakula ambavyo hupikwa katika joto la juu zaidi ya 300 degree. Chips ni chakula chenye mafuta mengi na mafuta yanapoingia mwilini huenda kuzunguka sehemu ya mwili wa mwanadamu. kama ni mtu ambaye mazoezi pia hufanyi madhara yake ni kupata magonjwa ya moyo. hivi sasa idadi kubwa ya vijana wanaugua magonjwa mengi yanayo sababishwa na mkusanyiko wa mafuta katika miili yao amabayo huchangiwa na kuto kufanya mazoezi madhara yake mafuta kuziba mirija Mafuta yakiliwa sana husababisha kuzidi mwilini. Pia inasadikika mafuta yaliyopo katika chipsi katika sahani moja ya chisi ya moto endapo utaamua kuchuja kuna uwezekano wa kupata nusu glasi ya mafuta ya kupikia. Kwa hali hii ujue ni hatari. Na mwili huwa hatupi kinachofaa, na badala yake kama hakitumiki wakati huo basi huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Ndio maana tunapokula vy

Mkude Atajwa Namba Sita Bora 2017/18

Image
KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ametajwa kuwa ndiye kiungo bora mkabaji msimu huu kuliko wote. Hali hiyo inatokana na uwezo wake mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha uwanjani wakati akiitumikia timu yake hiyo katika Ligi Kuu Bara. Wakizungumza na Championi Ijumaa kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali za ligi kuu wamemtaja Mkude kuwa ndiye kiungo bora msimu huu. Beki wa kati wa Mwadui FC, Idd Mobby amesema Mkude ni bora zaidi kuliko msimu uliopita na amekuwa na msaada mkubwa kwa timu yake jambo ambalo linamfanya awe vizuri. Naye beki wa Prisons, Salum Kimenya, amesema: “Simba wanapaswa kujivunia mchezaji huyo, kawafanyia kazi kubwa, ukiangalia mechi nyingi ambazo hajacheza mabeki wao walipata shida sana tofauti na anapokuwepo uwanjani, binafsi naona anastahili kuwa namba sita bora msimu huu

MAGAZETI YA LEO 5/5/2018

Image

Jinsi ya kuepuka matatizo ya nguvu za kiume

Image
MATATIZO haya ya nguvu za kiume humuathiri mwanaume na mwanamke kwa ujumla.Tatizo hili hulalamikiwa aidha na mwanaume mwenyewe au mwanamke kwa kutofurahia tendo la ndoa, hasa kwa wale walio katika mahusiano. Zipo sababu nyingi kama tutakavyokuja kuona lakini matatizo haya humuathiri mtu zaidi kisaikolojia anapohisi anashindwa kutimiza wajibu wake au mwanamke kujihisi hapati haki yake ya kufurahia tendo. Mtu anaweza kuwa na tatizo dogo ambalo kama ni mshtuko na anapopata mshituko huo hujikuta tatizo linazidi hivyo kujikuta mgonjwa, yaani ana tatizo. Kwa hiyo ni vema unapotokewa na tatizo hili usikimbilie kutumia dawa hasa za asili na hata za madukani bali waone madaktari wakufanyie uchunguzi katika hospitali kubwa. AINA ZA MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME Tatizo la nguvu za kiume limegawanyika katika makundi mawili; Kwanza ni tatizo la kuzidi kwa nguvu za kiume. Watu wengi wamezoea ukisema tatizo la nguvu za kiume ni upungufu, lakini lipo hili la kuzidi isivyo kawaida na ku

Huu ndiyo Ugonjwa Utokanao na Msongo wa Mawazo

Image
Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi. Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi. Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe  na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo. Ufuatayo ni ugonjwa unaosabishwa na msongo: Magonjwa ya moyo Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moy

TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA ZATIKISA JIJINI DAR

Image
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,(kulia) akizungumza jambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017. Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo. …Mwijage (katikati) akikabidhi tuzo kwa baadhi ya wamiliki wa viwanda . Mwijage (kushoto) akikabidhi tuzo kwa Zephania Shaidi kutoka Shirikisho la  Viwanda Tanzania (CTI) ambaye alipokea kwa niaba ya baadhi ya viwanda vilivyofanya vizuri ambavyo wawakilishi wake hawakuwepo. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mwijage (katikati). SHIRIKISHO  la Viwanda Tanzania (CTI) leo limetoa tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017 ambazo zimekabidhiwa na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage. Tuzo hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanz

Rais Magufuli: Bora Kula Sumu Kuliko Fedha za Serikali

Image
Rais Magufuli leo Ijumaa ameweka jiwe la msingi la Barabara ya Kidatu – Ifakara. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Wabunge wote wa Chadema na CCM mkoani Morogoro. Moja ya kauli ambazo Rais amezungumza leo; “Kuna maeneo ambayo wakandarasi wamekula hela za miradi, wamekula sumu. Hela ya Serikali ya awamu ya tano hailiwi bora ule sumu kali. Waliokula fedha waanze kujiandaa, kurudisha fedha na kutekeleza miradi au kukumbana na sheria ya mwaka 97.” “Haiwezekani mimi nitafute hela halafu wewe uzile tu nikwambie umeula wa chuya. Kama makandarasi watakuwa wamekimbia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, polisi na Takukuru wawatafute popote. Watazitapika hizo fedha wanazozitafuna,” amesisitiza Rais. Amesema hatojali fisadi ametoka CCM, Chadema wala CUF au nje ya nchi, atawashughulikia. Mbunge wa Kilombero, Lijualikali(CHADEMA) “Ukiniambia leo uwape zawadi gani watu wa Morogoro maana kuna mengi lakini naomba watu wote ambao wamechukua ardhi yetu na hawaifanyii kazi basi naomb

MAAMUZI YA JOHN HECHE BAADA YA MAZISHI YA MDOGO WAKE

Image
MBUNGE wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), John Heche amesema kutokana tukio la kuuawa kwa mdogo wake Suguta Chacha kwa kuchomwa kisu na askari polisi haturudi nyuma kupigania haki za watu ili haki na usawa kushamiri katika nchi. Heche amesema hayo leo Ijumaa, Mei 4, 2018 ikiwa ni siku moja baada ya mazishi mdogo wake huyo na kusema mdogo wake ameuawa kinyama, na kifo hicho kinazidi kumpa nguvu na sababu ya kupigania haki. “Nakuombea, upumzike kwa amani Suguta, kifo chako cha kinyama kinanipa sababu zaidi ya kuendelea kupigania. Utawala wa sheria haki na usawa katika taifa letu. Sitarudi nyuma nitapambana mstari wa mbele wakati wote kwa heshima yako na kwa heshima ya Watanzania wote wanaopenda kuona nchi yetu inaongozwa vizuri,” alisema Heche.  Aidha, Heche amewashukuru waombolezaji waliojitokeza kumzika mdogo wake huyo kwenye nyumba yake ya milele na kusema kuwa wamewapa faraja sana.  “Asanteni Watanzania wote na Wanatarime kwa jinsi ambavyo