Posts

Mkude Atajwa Namba Sita Bora 2017/18

Image
KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ametajwa kuwa ndiye kiungo bora mkabaji msimu huu kuliko wote. Hali hiyo inatokana na uwezo wake mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha uwanjani wakati akiitumikia timu yake hiyo katika Ligi Kuu Bara. Wakizungumza na Championi Ijumaa kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali za ligi kuu wamemtaja Mkude kuwa ndiye kiungo bora msimu huu. Beki wa kati wa Mwadui FC, Idd Mobby amesema Mkude ni bora zaidi kuliko msimu uliopita na amekuwa na msaada mkubwa kwa timu yake jambo ambalo linamfanya awe vizuri. Naye beki wa Prisons, Salum Kimenya, amesema: “Simba wanapaswa kujivunia mchezaji huyo, kawafanyia kazi kubwa, ukiangalia mechi nyingi ambazo hajacheza mabeki wao walipata shida sana tofauti na anapokuwepo uwanjani, binafsi naona anastahili kuwa namba sita bora msimu huu

MAGAZETI YA LEO 5/5/2018

Image

Jinsi ya kuepuka matatizo ya nguvu za kiume

Image
MATATIZO haya ya nguvu za kiume humuathiri mwanaume na mwanamke kwa ujumla.Tatizo hili hulalamikiwa aidha na mwanaume mwenyewe au mwanamke kwa kutofurahia tendo la ndoa, hasa kwa wale walio katika mahusiano. Zipo sababu nyingi kama tutakavyokuja kuona lakini matatizo haya humuathiri mtu zaidi kisaikolojia anapohisi anashindwa kutimiza wajibu wake au mwanamke kujihisi hapati haki yake ya kufurahia tendo. Mtu anaweza kuwa na tatizo dogo ambalo kama ni mshtuko na anapopata mshituko huo hujikuta tatizo linazidi hivyo kujikuta mgonjwa, yaani ana tatizo. Kwa hiyo ni vema unapotokewa na tatizo hili usikimbilie kutumia dawa hasa za asili na hata za madukani bali waone madaktari wakufanyie uchunguzi katika hospitali kubwa. AINA ZA MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME Tatizo la nguvu za kiume limegawanyika katika makundi mawili; Kwanza ni tatizo la kuzidi kwa nguvu za kiume. Watu wengi wamezoea ukisema tatizo la nguvu za kiume ni upungufu, lakini lipo hili la kuzidi isivyo kawaida na ku...

Huu ndiyo Ugonjwa Utokanao na Msongo wa Mawazo

Image
Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi. Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi. Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe  na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo. Ufuatayo ni ugonjwa unaosabishwa na msongo: Magonjwa ya moyo Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya...

TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA ZATIKISA JIJINI DAR

Image
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,(kulia) akizungumza jambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017. Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo. …Mwijage (katikati) akikabidhi tuzo kwa baadhi ya wamiliki wa viwanda . Mwijage (kushoto) akikabidhi tuzo kwa Zephania Shaidi kutoka Shirikisho la  Viwanda Tanzania (CTI) ambaye alipokea kwa niaba ya baadhi ya viwanda vilivyofanya vizuri ambavyo wawakilishi wake hawakuwepo. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mwijage (katikati). SHIRIKISHO  la Viwanda Tanzania (CTI) leo limetoa tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017 ambazo zimekabidhiwa na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage. Tuzo hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jam...

Rais Magufuli: Bora Kula Sumu Kuliko Fedha za Serikali

Image
Rais Magufuli leo Ijumaa ameweka jiwe la msingi la Barabara ya Kidatu – Ifakara. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Wabunge wote wa Chadema na CCM mkoani Morogoro. Moja ya kauli ambazo Rais amezungumza leo; “Kuna maeneo ambayo wakandarasi wamekula hela za miradi, wamekula sumu. Hela ya Serikali ya awamu ya tano hailiwi bora ule sumu kali. Waliokula fedha waanze kujiandaa, kurudisha fedha na kutekeleza miradi au kukumbana na sheria ya mwaka 97.” “Haiwezekani mimi nitafute hela halafu wewe uzile tu nikwambie umeula wa chuya. Kama makandarasi watakuwa wamekimbia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, polisi na Takukuru wawatafute popote. Watazitapika hizo fedha wanazozitafuna,” amesisitiza Rais. Amesema hatojali fisadi ametoka CCM, Chadema wala CUF au nje ya nchi, atawashughulikia. Mbunge wa Kilombero, Lijualikali(CHADEMA) “Ukiniambia leo uwape zawadi gani watu wa Morogoro maana kuna mengi lakini naomba watu wote ambao wamechukua ardhi yetu na hawaifanyii kazi basi naomb...

MAAMUZI YA JOHN HECHE BAADA YA MAZISHI YA MDOGO WAKE

Image
MBUNGE wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), John Heche amesema kutokana tukio la kuuawa kwa mdogo wake Suguta Chacha kwa kuchomwa kisu na askari polisi haturudi nyuma kupigania haki za watu ili haki na usawa kushamiri katika nchi. Heche amesema hayo leo Ijumaa, Mei 4, 2018 ikiwa ni siku moja baada ya mazishi mdogo wake huyo na kusema mdogo wake ameuawa kinyama, na kifo hicho kinazidi kumpa nguvu na sababu ya kupigania haki. “Nakuombea, upumzike kwa amani Suguta, kifo chako cha kinyama kinanipa sababu zaidi ya kuendelea kupigania. Utawala wa sheria haki na usawa katika taifa letu. Sitarudi nyuma nitapambana mstari wa mbele wakati wote kwa heshima yako na kwa heshima ya Watanzania wote wanaopenda kuona nchi yetu inaongozwa vizuri,” alisema Heche.  Aidha, Heche amewashukuru waombolezaji waliojitokeza kumzika mdogo wake huyo kwenye nyumba yake ya milele na kusema kuwa wamewapa faraja sana.  “Asanteni Watanzania wote na Wanatarime kwa...

Rais Magufuli ampigia simu Prof. Kitila mbele ya Wananchi

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempigia simu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kero ya maji katika eneo la Kidodi Morogoro. JPM amemtaka Prof. Kitila afike eneo hilo mara moja kushughulikia kero hiyo. Aidha, Rais Magufuli ameagiza Mkandarasi wa Maji Kata ya Kidodi, akamatwe mara moja kwa kushindwa kukamilisha mradi wa maji ndani ya wakati uliopo kwenye makubaliano ya utekelezaji wa mradi huo. “Ninafahamu kuna mradi wa maji wa Tsh. Milioni 800, mkandarasi alipewa lakini mpaka sasa maji hayajafika kwa wananchi, nilidhani mbunge wenu atauliza achukuliwe hatua gani lakini hajauliza, sasa mkandarasi kama alikula hela atazitapika, naomba mumfikishie huu ujumbe,” alisema Rais Magufuli.

Breaking News: Mahakama Kuu Yazuia Kanuni za Maudhui Mtandaoni

Image
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mtwara leo Ijumaa Mei 4, 2018 imetoa zuio la muda (Temporary Injuction) dhidi ya tangazo linalowataka wamiliki wa Blogs na Majukwaa ya Mitandaoni (Online Forums) kusajili huduma hizo kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutokana na matakwa ya kanuni mpya za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulations) ambazo matumizi yake yamekwishaanza na kesho Mei 5, 2018 ndiyo siku ya mwisho ya usajili huo. Maombi ya zuio hilo yaliyowalishwa mahakamani na waombaji sita wakiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Cente -LHRC), THRDC, MCT, TAMWA, Jamii Media na TEF ambapo katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo (Judicial review) washitakiwa ni Waziri wa Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communication Authority -TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Aidha, katika maombi ya msingi, waombaji wameiomba Mahakama kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa vigezo vifuatavyo; i) Waziri wa Habari amet...

John Stephen Akhwari Mwanariadha Shujaa Wa Tanzania

Image
John Stephen Akhwari akikimbia. M CHEZO wa ri­adha ni mchezo wa tatu unaopendwa zaidi na Watanza­nia, ukiondoa soka na ndondi bila shaka riadha ndiyo nam­ba tatu. Ukifungua ukurasa wa Google au YouTube kisha ukaandika John Stephen Akhwari hakika kile am­bacho utakiona kitakufanya utamani kutazama mpaka mwisho. Jina la mtu huyo litajitokeza mara nyingi kwenye kurasa hizo na k a m a u n ­amfa­hamu b a s i itaku­fanya utamani kumtazama na kuona historia yake kwa mara nyingine, kama ni mara yako ya kwanza bila shaka kuna kitu utajifunza hata kama siyo cha kimichezo basi kimaisha. Historia ya tukio lake lililotokea mwaka 1968 nchini Mexico bado ina­kumbukwa hadi leo, taswira ya kile wakati akikimbia kiliwa­fanya Wazungu wengi wakitambue kama ‘The Greatest Last- Place Fin­ish Ever in the Olympic games’. Maana isiyo ras­mi ya sen­tensi hiyo ni kuwa ni mtu wa mwisho bora ku­wahi kumaliza katika michezo ya Olimpiki, yaani alikuwa wa mwisho lakini ni bora kuwahi kut...

Simba Kufanya Mkutano wa Dharura Jumapili Mei 20

Image
Uongozi wa Klabu ya Simba unapenda kuwataarifu kwamba, kutakuwa na Mkutano wa Mabadiliko ya katiba utakaofanyika siku ya Jumapili ya tarehe 20/5/2018

Umaskini Utazidi Kukunyemelea Sana Kama Una Tabia Hizi Za Pesa

Image
Kushindwa katika maisha hakuji kwa bahati mbaya bali kuna kuja kutokana na tabia zetu ambazo tunazo kila siku kwenye maisha yetu. Tabia hizo kiuhalisia zinaturudisha nyuma sana kimafanikio kama tunazikumbatia. Kupitia makala haya ya leo nataka nikukumbushe baadhi ya tabia chache tu, na kama tabia hizo utazikumbatia uwe na uhakika unazidi kuukaribisha umaskini ukunyemelee kwenye maisha yako na kukupoteza kabisa. Inatakiwa kuwa makini sana na tabia hizi ambazo zinaweza zikaingilia uhuru wako wa kifedha na kuweza pengine kukuharibia karibu kila kitu kwenye maisha na kukuacha ukiwa mtupu hauna kitu. Tabia hizi ni zipi, twende pamoja tuweze kujifunza;- Tabia 1: Matumizi yako ni makubwa sana. Kama una matumizi makubwa kwa namna yoyote ile huwezi kukwepa kuishiwa. Inatakiwa matumizi yako uweze kuyabana kiasi cha kwamba yapate nafasi ya kukupa pesa ya ziada. Ni vizuri kuwa na daftari la kumbukumbu litakalokusaidia kutunza kumbukumbu zako za matumizi ili kimatumizi u...

MAAMUZI YA RAIS KUUPANDISHA HADHI MJI WA DODOMA KUWA JIJI NI SAHIHI-MAJALIWA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma Mei 3, 2018. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema maamuzi ya  Rais Dkt John Magufuli ya kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji ni sahihi na ameyafanya kwa wakati muafaka na hakuna sheria iliyokiukwa. Aprili 26, 2018 Rais Dkt Magufuli aliupandisha hadhi mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 3, 2018) wakati akijibu swali la Bibi Felista Bura (Viti Maalumu) katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma. Bibi Felista alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya baadhi ya watu wanaobeza maamuzi ya Rais Dkt. Magufuli ya kuupandisha hadhi mji wa Dodoma. Amesema kuwa Rais Dkt Magufuli hakukiuka sheria kwa sababu a...

BREAKING NEWS: YONDANI ASIMAMISHWA KUITUMIKIA YANGA

Image
Beki wa Yanga, Kelvin Yondani (kushoto). Bodi ya Ligi Tanzania, imetangaza kumsimamisha beki wa Yanga, Kelvin Yondani kutokana na kuonekana katika video akimtemea mate beki, Asante Kwasi. Mtendani wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amezungumza hivi punde na kusema suala lake limepelekwa Kamati ya nidhamu baada ya kuonekana haliwezi kusikilizwa na Kamati ya Saa 72 iliyokaa. “Kwa hiyo sasa tunamsimamisha hadi hapo kamati itakapokaa na kuamua kuhusiana na suala lake,” alisema Wambura. Katika picha ya video ilimuonyesha Yondani akimtemea Kwasi raia wa Ghana katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba ambao walishinda kwa bao 1-0. Suala hilo lilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau, wakiwemo waliomtetea Yondani na walioona haikuwa sahihi.

MLINGA ‘KUMCHOMA’ MWANAFUNZI SINDANO, WAZIRI UMMY: SI SAHIHI

Image
KUFUATIA picha zilizosambaa mitandaoni zikimuonyesha Mbunge wa Ulanga, Morogoro (CCM), Goodluck Mlinga, kuonekana ameshika sindano kama anamchoma mwanafunzi chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi, jambo hilo limeibua hisia tofauti miongoni mwa wadau huku wakihoji kuhusu mtu asiye na taaluma ya afya anapata wapi mamlaka ya kutoa chanjo hiyo. “Siasa imeingia sehemu mbaya sana, tiba si eneo la mzaha kiasi hiki, hili ni eneo hatari, na mchezo huu kwa afya za watu unaweza kusababisha maumivu hata ulemavu, si kila mtu anaweza kutoa chanjo,” alitoa maoni mmoja wa wadau kupitia mtanda wa Twitter. Akijibu hoja hiyo kupitia akaunti ya Twitter, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema jambo hilo si sahihi kwani wanaotakiwa kutoa huduma za afya ni watu wataalamu wa tiba na si mtu mwingine huku akimuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kutoa maelekezo kwa waganga.

AJISALIMISHA POLISI BAADA YA MAHINDI ALIYOIBA KUNASA MABEGANI

Image
KIJANA Frank Japhet (23), mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, amelazimika kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 20, anaodaiwa kuuiba kung’ang’ania mabegani. Wakati akihojiwa kituoni hapo, mtuhumuwa huyo amesema mzigo huo, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la Mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, mkoani Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Mei 3, 2018, akaongeza kwamba aliondoka na mzigo huo hadi eneo la Stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, ambapo mzigo huo uling’ang’ania kichwani. Ameendelea kusema kwamba alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka hivyo akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini...

Vijana wa CCM wanatamani sana nionyeshe naiunga mkono serikali ya awamu ya tano!

Image
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatamani sana yeye aonekane anaiunga mkono serikali ya awamu ya tano na kusema kuwa watasubiri sana kwa jambo hilo. Msigwa amesema hayo leo Mei 3, 2018 baada ya moja ya video yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuoonyesha akimsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa katika kipindi chake amekuwa hajali vyama kwani hata wao watu wa CHADEMA wamekuwa wakipokea fedha ambazo zimewawezeshja kujenga barabara kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa wilaya ambayo imegharimu zaidi ya bilioni tatu, wana stendi ya Ipogolo ambayo nayo imegharimu zaidi ya bilioni tatu na kudai kuwa Rais hapendelei. Baada ya video hiyo kusambazwa sana Mchungaji Msigwa amesema kuwa "Vijana wa CCM wanatamani sana nionyeshe naiunga mkono serikali ya awamu ya tano! (Dying for my endorsement ) Mtasubiri sana"`

KANISA LAPIGA MARUFUKU SHELA KWA WAJAWAZITO WAKATI WA NDOA

Image
KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limewapiga marufuku wanawake wajawazito kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa kwa madai vazi hilo ni alama ya ubikira kwa mwanamke na sio vinginevyo.   Hayo yamesemwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padre Festus Mangwangi  wakati akiweka mkazo juu ya tamko lililotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Isaack Amani , wakati akiadhimisha misa ya shukrani iliyofanyika Jumapili iliyopita, baada ya kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Francis kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo. Kabla ya uteuzi huo uliotangazwa Desemba 27 mwaka 2017 , Askofu Mkuu Amani alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi na kusema haitakiwi kwa mwanamke yeyote ambaye anajijua ni mjamzito kuvaa shela kipindi anafunga ndoa kwa kuwa vazi hilo linavaliwa na mwanamke asiyemjua mwanaume ( bikra ).   Aidha, Padre Festus Mangwangi amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao wa kike kutunza miili yao na kuishi maisha ya kimaadili hadi watakapopata w...