Jinsi ya kuepuka matatizo ya nguvu za kiume
MATATIZO haya ya nguvu za kiume humuathiri mwanaume na mwanamke kwa ujumla.Tatizo hili hulalamikiwa aidha na mwanaume mwenyewe au mwanamke kwa kutofurahia tendo la ndoa, hasa kwa wale walio katika mahusiano. Zipo sababu nyingi kama tutakavyokuja kuona lakini matatizo haya humuathiri mtu zaidi kisaikolojia anapohisi anashindwa kutimiza wajibu wake au mwanamke kujihisi hapati haki yake ya kufurahia tendo. Mtu anaweza kuwa na tatizo dogo ambalo kama ni mshtuko na anapopata mshituko huo hujikuta tatizo linazidi hivyo kujikuta mgonjwa, yaani ana tatizo. Kwa hiyo ni vema unapotokewa na tatizo hili usikimbilie kutumia dawa hasa za asili na hata za madukani bali waone madaktari wakufanyie uchunguzi katika hospitali kubwa. AINA ZA MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME Tatizo la nguvu za kiume limegawanyika katika makundi mawili; Kwanza ni tatizo la kuzidi kwa nguvu za kiume. Watu wengi wamezoea ukisema tatizo la nguvu za kiume ni upungufu, lakini lipo hili la kuzidi isivyo kawaida na ku