Posts

Naibu Waziri Mavunde Kalazwa Morogoro

Image
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavundeakiwa kalala kitandani Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro akisumbuliwa na homa kali. Mavunde amesema alipelekwa hospitalini hapo usiku wa kuamkia Jumapili baada ya kujisikia vibaya na saivi anaendelea kupatiwa matibabu

MTOTO ALIYECHOMWA SINDANO KIMAKOSA NA MADAKTARI KICHWANI,CHAANZA KUOZA

Image
Leo stori ninayokusogezea ni kuhusu matukio ya kutokuwa makini katika idara ya afya hasa kwa madaktari yanazidi kuzua wasiwasi kwa wananchi nchini Kenya, tukio lililotokea siku za hivi karibuni ni la mtoto kuchomwa dawa isiyofaa na kumfanya aanze kuoza kichwa. Tukio hili limefanyika katika hospitali ya Malava General Hospital katika jimbo la Kakamega na linatokea huku kukiwa na kesi dhidi ya Madaktari wa hospital ya Kenyatta inaendelea baada ya Daktari kumfanyia upasuaji mgonjwa asiyestahili. Mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Clinton Luchivya alikuwa amepelekwa katika hospitali hiyo baada ya kuwa mgonjwa na madaktari kumchoma kichwani baada ya kukosa mshipa wa kumwekea dawa. Kulingana na mama wa mtoto huyo, mwanae alikuwa na ugonjwa wa Malaria kabla ya kupokea matibabu katika hospitali hiyo. Alisema kuwa mwanae alikuwa ameanza kubadilika badilika kabla ya kufahamu kuwa kichwa chake kinaoza.
Image
Huku Drama za Diamond na Wema Zikinoga, Kule Zari Bata Batani – Picha 7 WAKATI Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz akiendeleza drama ya mapenzi na aliyekuwa girl friend wake, Wema Sepetu kupitia mitandao ya kijamii, mzazi mwenzake na mwanamuziki huyo, Zari The Bosy Lady ameendelea kura raha katika Hoteli ya Sun City nchini Afrika Kusini anakoishi. Zari kupitia ukurasa wake wa Instagram ametupia picha saba akila bata katika hoteli hiyo kuonyesha kuwa haumizwi na kile anachokifanya x wake huyo mitandaoni kwa kujiweka karibu na Wema, kupost picha na maneno yanayoonyesha kuwa wamerudisha uhusiano wao. Zari baada ya kuweka picha hizo hakuandika maneno mengi bali ameweka caption hii;  Sun City typa weekend. Kuanzia jana Ijumaa kumekuwa na drama mitandaoni zikionyesha Wema na Diamond kama tayari wamesharudiana baada ya Wema kutupia picha na kipande cha video mpya ya Diamond, African Beauty na kumfagilia boy friend wake huyo wa kitambo. Wema aliandika  “I’m inlove

Mzee Mkapa Ataka Mjadala wa Kitaifa

Image
RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa amesema ipo haja ya kuitishwa mjadala wa kitaifa wa kujadili hali ya elimu nchini kufuatia shule za serikali kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa. Mkapa ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa tukio la kumuingiza kazini Makamu Mkuu mpya wa chuo kikuu hicho cha Dodoma Profesa Egid Mubofu na kumuaga Makamu Mkuu wa chuo hicho aliyemaliza muda wake Profesa Idrisa Kikula. Mzee Mkapa amesema mjadala huo unatakiwa kuhusisha makundi yote ya jamii bila kujali kama ni ya sekta binafsi ama ya umma sambamba na watu wa kawaida siyo wasomi pekee ambapo kupitia njia hiyo anaamini suluhu ya kudumu itapatikana. Hata hivyo, Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanya juhudi kubwa kuondoa ada kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne pamoja kuongeza madawati, nyumba za walimu, madarasa, vitabu, kulipa stahiki za walimu

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA ITAKAYOTUMIA UMEME SGR-KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA- DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali

Kauli ya Wakili wa viongozi mtandao wa wanafunzi

Image
Wakili wa viongozi wa  Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Reginald Martine amesema wateja wake wameitwa kuhojiwa na mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kutoa ushahidi wa tukio la ‘kutekwa’ kwa mwenyekiti wao, Abdul Nondo. Akizungumza na MCL Digital leo Machi 14, 2018, Martine amesema tayari viongozi wawili kati ya wanne wa mtandao huo wameshatoa ushahidi wao, kwamba hakuna vitisho vyovyote walivyopewa na polisi. Amesema kuwa polisi wamemhakikishia kuwa hawatawashikilia viongozi hao na mara watakapomaliza kutoa ushahidi wataruhusiwa kuondoka. “Utaratibu wa wakili mtu anapokuwa anatuhumiwa lazima uwe na mteja wako wakati anapohojiwa lakini kama mteja anatoa ushahidi wakili siyo lazima awepo hivyo wanaendelea kutoa ushahidi muda,” amesema. Amesema walishauriana na  mmoja wa makamishna kuwa yeye asiwepo na viongozi hao wakati wanatoa ushahidi wao. Waliofika kuhojiwa na  DCI ni mkaguzi wa haki za binadamu, Alphonce Lusako; katibu wa mtandao hu

Nyama kutoka Afrika Kusini yateketezwa na ZFDA

Image
Picha ya Mtandao Zanzibar. Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), imeteketeza  kilo 48 za nyama kutoka Afrika Kusini baada ya Serikali kusitisha uingizaji nyama kutoka nchini humo kutokana na mlipuko wa bakteria wa listeria. Ilibainika kuwa nyama hizo ziliingizwa nchini kinyume cha sheria, Nyama hizo ni mali ya kampuni ya Qamar ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, ilikamatwa Uwanja wa wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza leo Machi 14 wakati wa zoezi hilo, mkuu wa kitengo cha uchambuzi wa hatari zinazotokana na chakula wa ZFDA, Aisha Suleiman amesema kilichosababisha kuteketezwa kwa nyama hiyo ni katazo lililotolewa na ZFDA baada ya kutokea mlipuko wa ugonjwa wa listeriosis. Amesema ZFDA ndiyo yenye majukumu ya kuhakikisha wananchi wanapata chakula salama, Aisha amesema uamuzi ya katazo hilo umetokana na uwapo wa maradhi ya Listeriosis nchini Afrika Kusini, hivyo ofisi yao imepiga marufuku uingizwaji nyama, maziw

ANGALIA MAPOKEZI YA A BOY FROM TANDALE YA DIAMOND PLATINUMZ NCHINI KENYA

Image
Kwanza kabisa Diamond kafanya kitu kizuri kwa kuonesha ni kwa namana gani nchi hizi mbili zipo vizuri na kushirikiana vema si kama ambavyo watu wengine huleta ushirikiano wa maneno Sasa hivi Kenya na Tanzania wamekuwa ndugu kwa kuunganishwa na msanii wetu Diamond planumz. Kwa haraka haraka nimejaribu kupitia taarifa mbali mbali za kwenye media nikaona kenya wanampo support ya kutosha kijana wetu. Kwa pamoja tunapaswa kumsapot na kumpongeza kwa hatua hiyo na kwa ukalimu wa watu wa kenya wanao ufanya kwa ndugu yetu huyu.

Kesi ya Madawa: Shahidi Afunguka Alichokikuta Chumbani kwa Wema

Image
Msanii wa filamu, Wema Sepetu (katikati) akiwa na mama yake mzazi Miriam Sepetu (kulia)  wakitoka kusikiliza kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mama mzazi wa Wema Sepetu akishuka ngazi za mahakama baada ya kusikiliza kesi inayomkabili mwanaye. Wema Sepetu na mama yake, Miriam Sepetu  wakijadili jambo baada ya kusikiliza kesi nje ya mahakama. MJUMBE wa Shina Namba 39, nyumbani anakoishi msanii wa filamu, Wema Sepetu, Steven Alphonce ambaye ni shahidi katika kesi inayomkabili staa huyo, amedai wakati wa upekuzi walikuta kipande cha sigara wala si bangi. Alphonce amesema hayo leo Jumatatu, Machi 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wenzake wawili na kusema alishiriki katika upekuzi nyumbani kwa Wema na kukuta kipande hicho cha sigara jikoni na chumbani kwa

ASLAY HATIMAYE AANIKA UKWELI KUHUSU KUTOKA NA NANDY,AFICHUA YOTE

Image
Msanii wa muziki Bongo, Aslay amefunguka kuhusu ukaribu wake na Nandy kwa sasa. Muimbaji huyo wa ngoma ‘Natamba’ ameiambia FNL ya EATV kuwa kinachowaunganisha ni kazi tu hakuna mahusiano ya kimapenzi kama inavyokuwa ikiripotiwa. Nafikiri mashabiki zangu ambao wananifuatilia wanajua ni mtu ambaye nina mtoto, kuna mwanamke ambaye nimezaa naye. Nandy tupo kwenye kazi tu, tunafanya lakini hamna chochote kinachoendelea kati yangu na Nandy,” amesema. Aslay na Nandy kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma ‘Subalkheri’ ikiwa ni ngoma yao ya pili kutoa pamoja baada ya Mahabuba.

MAUWAJI YA KUTISHA TENA ,MTOTO ATEKWA NA KUUAWA KINYAMA

Image
MASKINI MTOTO HUYU! Atekwa na Kuuawa, Mama Mzazi Hoi! Maskini mtoto wa watu! Ndivyo walivyosikika mashuhuda wa tukio la mwanafunzi, Doricka Majeshi, anayesemekana kutekwa kisha kukutwa akiwa ameuawa na watu wasiojulikana ndani ya nyumba inayoendelewa kujengwa na kuibua simanzi nzito. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, mtoto Doricka mwenye umri wa miaka nane aliyekuwa anasoma darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Lukobe mjini hapo alidaiwa kukutwa na mkasa huo tangu Jumanne ya wiki iliyopita kisha kusakwa kwa siku tatu bila mafanikio, kabla ya mwili wake kukutwa ukiwa na majeraha Alhamisi iliyopita nyuma ya nyumba hiyo

Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA Ajiuzuru

Image
Naibu Katibu Mkuu Baraza la Vijana Chama cha Demokrasia na Maendeleo – Chadema (BAVICHA), Getrude Ndibalema amesema amejiuzuru nafasi hiyo na kubaki mwanachama wa kawaida ili kutimiza majukumu binafsi.

WAZIRI MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI

Image
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakati wa ufunguzi mkutano wa 14 wa kikao kazi cha Maafisa hao kilichoanza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi, 2018 Jijini Arusha. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi akizungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakati wa ufunguzi mkutano wa 14 wa kikao kazi cha Maafisa hao kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gabriel Daqqaro akuzungmza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakati wa ufunguzi mkutano wa 14 wa kikao kazi cha Maafisa hao kilich