MAUWAJI YA KUTISHA TENA ,MTOTO ATEKWA NA KUUAWA KINYAMA

MASKINI MTOTO HUYU! Atekwa na Kuuawa, Mama Mzazi Hoi! Maskini mtoto wa watu! Ndivyo walivyosikika mashuhuda wa tukio la mwanafunzi, Doricka Majeshi, anayesemekana kutekwa kisha kukutwa akiwa ameuawa na watu wasiojulikana ndani ya nyumba inayoendelewa kujengwa na kuibua simanzi nzito.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, mtoto Doricka mwenye umri wa miaka nane aliyekuwa anasoma darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Lukobe mjini hapo alidaiwa kukutwa na mkasa huo tangu Jumanne ya wiki iliyopita kisha kusakwa kwa siku tatu bila mafanikio, kabla ya mwili wake kukutwa ukiwa na majeraha Alhamisi iliyopita nyuma ya nyumba hiyo

Comments

Popular posts from this blog