Posts

Kikosi cha Simba dhidi ya Waarabu Leo

Image
KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, tayari ameshakipanga kikosi chake ambacho kitaanza leo Jumatano kwenye mchezo wao dhidi ya Al Masry ya Misri, huku akiwapa jukumu zito la kufunga mabao washambuliaji wake, Emmanuel Okwi na John Bocco. Mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa ni wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika na utaanza majira ya saa 12 jioni, ingawa Lechantre hakufura­hishwa na muda huo uliopangwa na viongozi. Katika mazoezi ya juzi Jumatatu yaliyoanza majira ya saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Boko uliopo jijini Dar, Championi lilimshuhudia Lechantre akipanga kikosi chake kilichoonekana ndicho cha maan­gamizi ambacho kitatumika kum­maliza Mwarabu leo. Katika kikosi hicho ambacho golini yupo Aishi Manula, walinzi wake ni Shomary Kapombe, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Yusuf Mlipili na James Kotei. Kwenye kiungo wapo; Jonas Mkude, Nicholaus Gyan, Shiza Kichuya, Bocco na Okwi. Katika ma­zoezi hayo yaliyomalizika saa 1:30 usiku, kocha huyo

Mwenyekiti Mtandao wa Wanafunzi Hajulikani Alipo

Image
TAARIFA zilizoenea mchana huu zinadai kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hajulikani alipo tangu jana saa sita usiku. Marafiki za Nondo wamedai alituma ujumbe kwa viongozi wenzake wa TSNP kuwa yuko katika hatari na baada ya kutuma ujumbe huo simu yake ilikuwa ikipokelewa lakini hakuwa akiongea chochote, na baada ya muda alianza kujiondoa kwenye magroup ya WhatsApp. Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa TSNP kuhusu Nondo inasema hajulikani alipo wakiwemo wazazi wake.   Viongozi wa TSNP wamefika Kituo cha Polisi kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na  kutoa taarifa za kupotea kwake. Feb 18, 2018, Nondo alijitokeza na kuikosoa mienendo ya Jeshi la Polisi na Waziri wa Mambo ya Ndani, na mara ya mwisho kuongea na wanahabari, alishinikiza Waziri  Mwigulu Nchemba ajiuzulu. Hivi karibuni pia akizungumza na

TFDA kuzuia soseji kutoka Afrika Kusini zenye bakteria

Image
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema itazuia uingizaji wa soseji kutoka Afrika Kusini zilizobainika kuwa na bakteria aina ya listeria. Uamuzi wa TFDA unatokana na soseji hizo aina ya Polony kubainika kuwa na aina hiyo ya bakteria wanaosababisha ugonjwa wa listeriosis uliosababisha vifo vya watu 180 nchini Afrika Kusini. Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza akizungumza na Mwananchi jana alisema mamlaka hiyo inalifanyia kazi suala hilo ikiwa ni pamoja na kuzuia uingizwaji wa soseji hizo nchini, “Tunalifanyia kazi kwa kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama soseji husika zipo katika soko,” alisema. Soseji hizo kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na vyombo kadhaa vya kimataifa zinatengenezwa na kiwanda cha tiger brands unit enterprises na cha RCL foods vyote vya Afrika Kusini. Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi alikaririwa na mitandao ya kijamii akisema ameagiza kuondolewa sokoni soseji hizo, huku akiwashauri wananchi kuacha kula. Mot

Tanzia:Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma mjini afariki dunia Muhimbili

Image
ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Dkt. Kabourou ambaye alizaliwa Mei 23, 1949, amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CHADEMA) kabla ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma. Aidha, Dkt. Kabourou amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki akiiwakilisha Tanzania kuanzia Juni 05, 2007 hadi Juni 04, 2012. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa sasa wa Kigoma Mjini amesema kwao huo ni msiba mkubwa, na umewaacha na majonzi tele. “Tumeamka asubuhi na habari za kusikitisha kuwa Dkt. Amani Walid Kabourou, Mbunge Mstaafu wa Kigoma Mjini ametangulia mbele ya haki. Hakika ni msiba mkubwa kwetu. Mola ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,” ameandika Zitto.

MAGAZETI YA LEO 5/3/2018

Image

Fahamu Madhara Ya Usukaji Wa Nywele Bandia Na Uvaaji Wa Mawigi

Image
Katika karne ya sasa , uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususan na wanawake. Ingawa uvaaji wa wigi huwafanya wanawake hao kuonekana ni walimbwende zaidi. Wigi huvaliwa zaidi na kinamama wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa asili ya Afrika. Lakini tukiangalia moja ya chimbuko hasa la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe  na nywele zisizo shombeshombe walifanyishwa kazi ngumu za mashambani. Watumwa waliopelekwa barani Amerika hawakuweza kuzihudumia nywele zao kutokana na hali ngumu, na mabwenyenye waliwashusha hadhi na kuwavunja moyo kwa kuwaambia hawakuwa na nywele bali ni "manyoya". Lakini sababu nyingine inayodhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya Afrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu pengine hadi mgongoni ni mrembo zaidi. Pia siku hizi warembo na wanaoshiriki katika mashindano ya urem

Ikulu Yakanusha Taarifa Dhidi Ya Waziri Hamis Kigwangala

Image
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amekanusha kuwa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala kwa mujibu wa barua inayosambaa kwenye mitandao kuwa ni uzushi na imetengenezwa na wahalifu.        Alichokisema Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa. Barua inayosambaa kwenye mitandao ambayo imetengenezwa na wahalifu.

DIAMOND KULAMBA SHAVU KOMBE LA DUNIA SIRI YAFICHUKA!

Image
DAR ES SALAAM: Nyuma ya tukio la Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kulamba shavu la kuimba wimbo wa uzinduzi wa Michuano ya Kombe la Dunia 2018, Ijumaa Wikienda limebaini siri iliyochangia uteuzi wake huo. Katika uchunguzi mdogo uliofanywa na gazeti hili, mambo matatu makubwa ambayo ndiyo sababu kubwa iliyowafanya waandaaji wampe kipaumbele rais huyo wa Wasafi Classic Baby (WCB). Ijumaa Wikienda lilibaini kuwa, jambo la kwanza lililochangia Diamond ateuliwe ni bidii ya uongozi wake chini ya Sallam SK. Sallam ametajwa kuwa miongoni mwa mameneja ambao wana ‘connection’ nyingi za vituo vikubwa vya redio na televisheni ambavyo hucheza nyimbo za Diamond duniani. Ilielezwa kuwa, connection hizo ndizo zilizochangia kuwashawishi waandaaji wa michuano hiyo wakati walipokuwa wanaangalia ni wasanii gani wa Afrika ambao wana uwezo na ushawishi mkubwa, wakampendekeza Diamond. Mbali na hilo, jambo lingine lililochangia Diamond ateuliwe na kushiriki katika uzinduzi wa mashindano

BREAKING NEWS : AJALIMBAYA DALADALA YAGONGANA NA GARI LA TAKA,LASABABISHA VIFO NA MAJERUHI DODOMA

Image
Watu sita wamefariki dunia papo hapo huku wengine sita kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mkoani Dodoma. Eneo la ajali ambapo watu sita wamefariki baada Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gillece Muroto amesema ajali hiyo imetokea leo Jumapili Machi 4, 2018 majira ya mchana ambapo daladala aina ya Toyota Hiace iliyokuwa na abiria kugongana na lori la kubebea taka. Taarifa zaidi nitazitoa baada ya kufuatilia lakini kwa ufupi ajali hiyo ipo na watu sita wamekufa na wengine sita wapo katika hospitali ya rufaa ya mkoa na hali zao sio nzuri,” amesema Muroto kwenye mahohjiano na Gazeti la Mwananchi.

Kilimo Bora Cha Viazi Vitamu

Image
Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Zao la viaViazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro,Kagera,Arusha na Ruvuma. Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha mboji. Aina za viazi vitamu Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista. Faida: vina wanga, vitamin, kambalishe, madini ya kalisiuamu, potasiamu, chu

Breaking News: Moto Waunguza Shule ya Wasichana Korogwe

Image
Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe  iliyoko wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, inaungua moto usiku huu, huku chanzo cha ajali ya moto huo kikiwa hakijajulikana. Inadaiwa watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na moto huo. Hakuna vifo vilivyoripotiwa ama kuthibitishwa hadi sasa. Tunaendelea kufuatilia kwa kina, taarifa zaidi tutakuletea baadaye.

Breaking News: Watano Wafariki Basi la New Force Kugongana na Hiace

Image
WATU watano wamefariki dunia leo asubuhi baada ya basi la New Force lilikokuwa linatokea Msamvu kwenda Mikese kugongana na gari dogo la abiria (Hiace) lililokuwa linatokea Msamvu, mkoani Mogororo. Pia watu kadhaa ambao idadi yao bado haijajulikana, wamejeruhiwa. Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema chanzo ni dereva wa gari hilo la Hiace kutaka kulipita gari la mchanga lililokuwa mbele ambapo lilijikuta likigongana uso kwa uso na basi hilo.