Posts

Waziri Mkuu Akagua Shamba La JKT

Image
Waziri Kassim Majaliwa amekagua shamba la uzalishaji wa mbegu bora za mihogo aina ya mkombozi linalomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Rwamkoma wilayani Butiama. Amekagua shamba hilo linalomilikiwa na Kikosi cha JKT Rwamkoma leo (Jumamosi, Januari 20, 2018) alipowasili wilayani Butiama akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara. Kikosi hicho kimewezeshwa na Halmashauri ya Butihama. Waziri Mkuu amewakipongeza kikosi cha JKT Rwamkoma kwa uamuzi huo wa kuzalisha mbegu bora za mihogo ambazo baadae zitasambazwa kwa wakulima wa zao hilo wilayani hapa.Pia amewataka wakazi wanaoishi karibu na shamba la kikosi hicho hilo kulitumia kama shamba darasa kwa ajili ya kujifunza namna bora ya kulima zao hilo. Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali David Msakulo alisema shamba hilo linaukubwa wa ekari 60, na mbegu zitakazozalishwa zitatosha kupanda ekari 900.Mkuu huyo wa kikosi hicho aliongeza kuwa mbegu hizo zinazozalishwa katika shamba hilo zi

Tahadhari Kuhusu Homa ya Chikungunya, Hakuna Tiba Mahusi Wala Kinga

Image
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeutahadharisha umma kuhusu ugonjwa wa Homa ya Chikungunya ambao huambukizwa na mbu aina ya aedes na hauna tiba mahsusi wala kinga. Isome taarifa hii kuelewa zaidi kuhusu ugonjwa huo.    

Waziri Aagiza Kaimu Mkurugenzi Wa Maji Kusimamishwa Kazi

Image
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Maji Mijini, Clement Kivegalo. Pia, Kamwelwe amemwagiza mkurugenzi wa utawala wa wizara hiyo, Barnabas Ndunguru  kuwahamishia Dodoma watumishi 178 wa wizara ifikapo Januari 30, 2018 la sivyo atamchukulia hatua. Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20, 2018 jijini Dar es Salaam, Waziri Kamwelwe amesema jana Januari 19, alizivunja bodi  za maji safi za Mkoa wa Arusha na Musoma baada ya kujiridhisha kuwa utendaji wao si mzuri. “Juzi tu niliuondoa utendaji wa Lindi, kuna tatizo la utendaji wa wakandarasi hapa Dar es Salaam, Chalinze na tuna tatizo Kigoma, mamlaka za maji za miji ya mikoa  zinasimamiwa na mkurugenzi wa maji mijini, hapa tuna idara kama tatu au nne zinasimamia utekelezaji wa miradi hiyo,” amesema Mhandisi Kamwelwe na kuongeza, “Idara ya maji mijini inaongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mhandis

Nicole Aingilia Ishu Ya Wastara Kuchangiwa Pesa

Image
Msanii wa filamu Bongo, Nicole Francklyn. MSANII wa filamu Bongo, Nicole Francklyn amewataka wasanii wenzake kuungana na kuendesha kampeni ya kumchangia msanii mwenzao, Wastara Juma kutokana na maradhi ya mguu yanayomsibu, kwa kuwa hakuna aijuaye kesho. Wastara Juma Akizungumza na Star Mix , Nicole alisema, kama wasanii wangekuwa na umoja na kuungana katika hilo, kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakijionyesha kumwaga pesa kwenye mambo ya starehe, endapo wangejitoa kwa moyo mmoja kwenye suala hilo, basi kivyovyote vile michango ingekuwa imetimia. “Niwasihi wasanii wenzangu tuungane kumchangia Wastara michango iweze kutimia akamilishe matibabu yake, naamini sapoti ya wasanii iliyopo bado haitoshi waongeze nguvu kwenye hili, hata kama mtu ana visasi naye aweke kando kwa sasa, kwa sababu matatizo yanaweza kumfika yeyote yule,” alisema

Agizo la Waziri Mwigulu kwa Polisi kuhusu kukamata wazururaji

Image
January 20, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutafuta namna ya kupunguza wahalifu wanaokamatwa kwa makosa kama uzururaji ili kupunguza mrundikano kwenye mahabusu. Ameeleza kuwa suala hili pia litaepusha watuhumiwa wanaopelekwa mahabusu kwa makosa ya uzururaji kupata nafasi ya kuzungumzia masuala ya uhalifu na watuhumiwa waliozoea. Kwa upande mwingine Dr. Mwigulu ameagiza wananchi kushirikiana na serikali katika ujenzi wa vituo vya polisi kwa kuwa suala la ulinzi ni ajenda ya kila Mtanzania na linapaswa kupewa kipaumbele. Akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Dr. Mwigulu amesema kuwa mkakati wa Halmashauri hiyo kujenga kituo cha kisasa cha polisi ni kitendo cha kupongezwa kwani wanalenga kukomesha uhalifu wa aina zote.

NI NINI MAANA YA MAPENZI

Image
Katika kuongelea suala zima la mapenzi ni vigumu kujua maana halisi ya mapenzi kwa maana halisi ya mapenzi ni kutokana na mtu mwenyewe anavyoona. Lakini kwa ujumla mapenzi ni ile hali ambayo watu wawili wanaingia katika mahusiano ambayo yanabeba mambo mengi iliwemo uvumilivu,kuchukuliana katika mambo yote yanayo husu maisha kwa ujumla. MSINGI HASA WA MAPENZI  UVUMILIVU HEKIMA BUSARA UPENDO UWAZI HESHIMA 1-Uvumilivu katika mapenzi ni suala la msingi sana kwani kama nilivyotangulia kusema kuwa mapenzi ni kama safari ambayo ina mambo mengi ikiwemo mateso na mabadiko mbali mbali. kwa hiyo bila uvumilivu ni kazi bure. 2-Hekima ni hali ya kunyenyekea. ili mapenzi yaweze kuwa mapenzi lazima kuwe na unyenyekevu wa kutosha. 3 Busara ni hali ya kutengeneza uelewano na kuondoa tofauti eitha ya ki maneno au matendo. 4 Upendo ni hali ya kutengenza imani imara na sawia baina yenu wawili. 5 Uwazi ni hali ya kusomana na kufamiana ki myoyo kimwili na kifikra bain

MAGAZETI YA LEO 18/1/2018

Image

BREAKING NEWS: POLISI DAR YAKAMATA SILAHA NZITO

Image
JESHI la Polisi kanda Maalumya Dar es Salaam limekamata silaha mbalimbali zikiwemo bunduki, bastola na vifaa vingine vya kufanyia matukio ya uhalifu pamoja na watuhumiwa mbalimbali wa makosa ya uhalifu ambao walikuwa wakijiandaa kutekeleleza matukio hayo. Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasaamesema jeshi hilo limekamata silaha aina ya AK 47 na watuhumiwa wawili nyumbani kwa mzee Said Omary (62) baada ya kupata taarifa kuwa kuna wahalifu wanataka kufanya tukio la wizi wa kutumia silaha. Aidha Polisi imewakamata watuhumiwa 2 wa wizi wa magari ambao baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na radio call, kadi 10 za benki mbalimbali, leseni za udereva, master keys 15 ambapo baada ya kuhojiwa walikiri kutekeleza matukio mbalimbali ua uhalifu huku wakionesha magari mawili na pikipiki moja vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi.

Zitto kabwe azuiwa kufanya mkutano wa hadhara

Image
Jeshi la Polisi Kigoma limemzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kufanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Uwanja wa Mwanga Community Center, mkoani Kigoma ambao ulipaswa kufanyika leo Januari 16, 2018. Taarifa iliyotolewa na OCD inasema kuwa kiongozi huyo hakufuata utaratibu wa kutoa taarifa ndani ya masaa 48 kabla ya kufanyika kwa mkutano huo jambo ambalo Mbunge Zitto Kabwe amelilamikia na kusema kuwa amezuiwa kufanya Mkutano kinyume na sheria ya Bunge ya mwaka 1988. "Mimi sitaki kuwapa polisi sifa ya kupambana nasi. Tumeahirisha mkutano mpaka siku ya jumamosi Lakini tumewaandikia barua rasmi kuwa sheria waliyonukuu sio sheria halali na haihusiani na mikutano ya Mbunge kwenye jimbo lake la Uchaguzi. Sheria wanayopaswa kunukuu ni sheria namba 3 ya mwaka 1988 kifungu cha 4(1)". Alisema Zitto Kabwe Kufuatia jambo hilo Zitto Kabwe amedai kuwa atamwandikia barua rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuhusu suala hil

Breaking: Mbunge Sugu Anyimwa Dhamana, Apelekwa Mahabusu Gerezani

Image
Mbunge Joseph Mbilinyi “Sugu”. MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepelekwa mahabusu katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya baada ya kukosa dhamana katika kesi ya uchochezi inayomkabili. Sugu na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Januari 16 na kupelekwa mahabusu leo Jumanne Januari 16, baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa washtakiwa kutokana na kosa walililotenda. Sugu naMasonga wakipelekwa mahabusu. “Kosa walilolitenda washtakiwa ni kutoa maneno ya fedheha yanayomtaja rais kuwa muuaji hivyo wakiwa nje wanaweza kupata matatizo kwa wananchi ambao hawajapendezwa na maneno hayo,” alidai Wakili Pande. Masonga akihutubia. Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alikubaliana na ombi hilo ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa dhamana. Washtakiwa hao wanadaiwa k

KUFURU! Vee Money na Jux Wamwaga Minoti Harusi ya Shilole

Image
Uchebe na Shilole waati wa harusi yao usiku wa kuamkia leo. COUPLE ya wakali wa Bongo Fleva, Juma Jux na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ usiku wa kuamkia leo wamefanya kufuru baada ya kugawa minoti kwenye harusi, Shilole na Uchebe iliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam. Katika harusi hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao wakiwemo wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Couple ya Jux na Vanessa walipata fursa ya kutoa nasaha na kumpongeza Shilole kwa kufunga ndoa pia wakimpongeza Uchebe kwa kumpata mke aliye bora. Jux na Vanessa. Kwa upande wa Jux alisema zawadi kubwa anayoitoa kwa Shilole ni kumsomesha mtoto wake mmoja kwa mwaka mmoja huku Vee Money akisema atamlipia muimbaji huyo kulala katika Hotel ya Nyota Tano ya Kilimanjaro. Baada ya hapo, Jux alichana pochi na kumkabidhi Vanessa mkwanja ambapo aliwavagaa maharusi na kuanza kuwarushia pesa hizo kama zawadi.

Nufaika Na Kilimo Bora Cha Matango

Image
Habari rafiki na karibu sana katika safu hii ya makala za kilimo. Katika somo liliopita tuliangalia juu ya umuhimu wa kutumia mbegu bora na faida zake. Sasa leo tutaangalia kilimo cha matango kwa kutumia mbegu bora inayoitwa Hybrid Cucumber YETU F1 ambayo utaanza kuvuna baada ya siku 45-50 kutoka kupandwa kwake. YETU F1 ni mbegu chotara ambayo ina umbo zuri na hupendwa sana na walaji. Kiasi cha mbegu 300g(Gramu 300) huweza kutosha ekari moja ambayo utainununua kwa shilingi laki tatu(300,000/=) za kitanzania.  UANDAAJI WA SHAMBA. Chagua sehemu iliyo nzuri,na ukipata sehumu ya tifutifu iliyo changanyikana na mchanga itakuwa vizuri zaidi. Pia ukipata sehemu yenye udongo mzito lakini usiwe una tuamisha maji. Lima shamba na hakikisha umelisawazisha vizuri(yaani hallowing),baada yapo panga matuta yako. KIASI CHA MBEGU . Gramu 300 zenye kiasi ya YETU F1 kinatosha kupanda eneo la ekari moja(100m×40m). Na hii aina ya mbegu 1g ina mbegu 30-40. Kabla ya kupanda hakikish

Majaliwa amuagiza CAG kuchunguza mfuko wa CDTF

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameuvunja Mfuko wa Wakfu wa kuendeleza zao la Kahawa (CDTF) na amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza mwenendo wa mfuko huo tangu ulipoanzishwa. Majaliwa agizo hilo leo wakati akizungumza na wadau wa zao hilo kwenye kikao cha kujadili maendeleo ya zao la kahawa alichokiitisha, mjini Dodoma. Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kwamba uundwaji wa mfuko huo si wa kisheria bali ni wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB). Pia aliagiza kufungwa kwa ofisi za CDTF ili kupisha uchunguzi na baada ya CAG kukamilisha uchunguzi na kukabidhi ripoti, kazi zote zilizokuwa zinafanywa na mfuko huo zitafanywa na Bodi ya Kahawa. Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku wanunuzi wa kahawa kwenda kununua kwa wanavijiji na badala yake kahawa yote itauzwa kwa njia ya minada.

Mbunge Haonga afichua kuwa wabunge wanajiuza

Image
Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe kwa tiketi ya (CHADEMA), Pascal Haonga amefunguka na kusema kuwa baadhi ya wabunge wamekuwa wakijiuza na kununuliwa kwa bei ndogo na kudai yeye hawezi kuwa sehemu ya watu hao ambao wananunuliwa. Haonga amesema hayo alipokuwa akifanya mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo lake la Mbozi na kusema wabunge na wanasiasa ambao wana hama vyama kwa kununuliwa na kujidai wanaunga mkono utendaji wa Rais wana upungufu wa akili. "Mimi siwezi kufanya kama wabunge wengine huko ambao wamekua wakijiuza kwa bei ndogo, mmesikia madiwani wananunuliwa, wabunge wananunuliwa. Hivi inangia akilini kweli wananchi walikuchagua na wengine walichoma nyumba za wengine, wengine waliamua kuchoma na magari, wengine waliamua kuchoma na mahakama, baiskeli na Pikipiki halafu unakuja kusema eti namuunga mtukufu kwa jitihada na kazi anazofanya. Hivi wewe Mbunge utakuwa na akili au matope" alihoji Haonga Mbali na hilo Mbunge huyo amewaeleza wananch

Maneno ya Uhuru Kenyatta na Odinga baada ya Olunga kuwa Mkenya wa kwanza kufunga Hat-trick

Image
Michael Olunga amekuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi kuu ya Uhispania ~La Liga. Olunga amefunga magoli matatu (Hat-trick) dhidi ya Las Palmas na kuweka rekodi ya kuwa Mkenya wa Kwanza kufunga hat-trick kwenye Laliga. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kuona taarifa hiyo hakukaa kimya kupitkia ukurasa wake wa Facebook akampongeza Michael Olunga kwa kusema “Ongera Michael Olunga kwa kuweka historia kuwa Mkenya wa kwanza kufunga goli katika ligi ya Hispania La Liga na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwa klabu ya Girona katika ligi ya Spain” Nae kiongozi wa Muungano wa Upinzania nchini Kenya Raila Odinga amepost katika ukurasa wake wa Twitter kumpongeza Olunga.  

Kumbe bila kuitwa na Waziri tusingejua Gigy ana mimba

Image
Msanii Gigy Money ambaye hivi karibuni ameonekana akiwa mjamzito na kuwashangaza wengi, amesema hakukusudia kuwajulisha watu bali ilikuwa kwa bahati mbaya wamejua Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv pia Gigy Money amewataka watu kumshukuru Naibu Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na Michezo Juliana Shonza kwa kumuita, kwani bila wito huo watu wasingemuona mtaani na kumuona akiwa na ujauzito wake. “Kwanza Mumshukuru yule waziri la sivyo msingeuona, huwa sipendi kabisa kuongelea masuala ya ujauzito wangu ila siku ile ilitokea bahati mbaya watu wakauona, alafu hao wanaosema nimeweka mimba feki ili serikali inionee huruma mi nina undugu na serikali? Kama mtoto anaokotwa basi subirini nami wangu nitamuokota”, amesema gigy Money. Kauli hiyo ya Gigy Money imekuja siku chache baada ya watu kumuona na ujauzito, huku wengine wakidai ameweka mimba feki ili serikali imuonee huruma.

Rais Magufuli ammwagia sifa Kagame

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame atalisaidia bara la Afrika kusonga mbele kimaendeleo kwa kuwa kiongozi huyo anajua matatizo na shida za nchi nyingi za Afrika. Magufuli amesema hayo leo Januari 14, 2018 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mazungumzo yake na Rais Kagame ambayo yamefanyika leo Ikulu na kusema kuwa Kagame ni mwanamapinduzi wa kweli wa Afrika hivyo atakavyokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika atalisaidia bara hilo kusonga mbele zaidi. "Kagame atakapokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) sisi Tanzania tumeipokea hii kwa raha sana kwa sababu tunamfahamu Rais Kagame lakini pia ni jirani yetu mwema sasa Mwenyekiti atakuwa anatoka ndani ya East Africa Community, nimemuakikishia kuwa sisi Tanzania tutampa ushirikiano wa hali ya juu sana katika nafasi hii atakayokwenda kuichukua na nimemthibitishia kutokana na ushawishi wake Afrik

Pombe Za Johari Ilikuwa Stresi

Image
J OHARI amefunguka kuwa pombe alizokuwa akinywa zilikuwa zikichangiwa na msongo wa mawazo. Johari ameliambia Spoti Xtra kuwa kutokana na ugumu wa kazi za filamu kwa hivi sasa lazima mtu uchanganyikiwe nini kifanyike ili filamu zisife. “Wakati mwingine nilikuwa nakunywa pombe sana kwa ajili ya msongo wa mawazo lakini niliona sio suluhisho kunywa pombe,” alisema Johari.

BAADA YA UBINGWA WA MAPINDUZI CUP, AZAM FC IMECHUKUA MAAMUZI HAYA KUHUSU SURE BOY…

Image
Salum Abubakar ‘Sure Boy’. Azam Fc imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, hiyo ni baada ya kuifunga URA ya Uganda kwa penati 4-3. Awali katika dakika 90 za mchezo huo, timu hizozilitoka suluhu ya 0-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, jana usiku kisiwani Unguja. Baada ya kukabidhiwa ubingwa huo, taarifa kutoka Azam FC zinaeleza kuwa ubingwa huo wameutoa zawadi kwa kiungo wa timu hiyo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, na hii ni baada ya kufiwa na Mama yake mzazi wiki iliyopita wakati akiwa na timu hiyo kwenye harakati za kuwania taji hilo. Hadi Azam FC inatwaa ubingwa, imeweza kucheza jumla ya mechi sita, ikishinda mara tano na kupoteza mmoja huku ikiruhusu nyavu zake kuguswa mara moja tu, na hii ni walipofungwa bao 1-0 dhidi ya URA kabla ya kulipa kisasi kwenye mchezo huo wa fainali. Kikosi hicho kilitarajiwa kuondoka visiwani Zanzibar, asubuhi ya leo Jumapili kurejea jijini Dar es Salaam tayari kabisa kuanza maandalizi ya kuwakabili Majimaji

KAULI YA ALBERTO MSANDO KUHUSU SAKATA LA LEMUTUZ LILILOTIKISA MTANDAONI

Image
From @albertomsando -Kaka na rafiki yangu @lemutuz_superbrandtz; Nimetamani sana nikae kimya upambane na ‘msala’ wako mwenyewe. Lakini nimeshindwa. Nimeshindwa kwa sababu naelewa na najua inavyokuwa pale unapopitia unachopitia. I have been there. Niseme kwamba kwa comments zote unaweza sasa kuelewa kiasi cha chuki dhidi yako. Kiasi cha furaha kwa maadui zako. Lakini ndani yake usiache kuona kiasi kidogo cha upendo na huzuni kutoka kwa marafiki zako. Kosa lako ni kuruhusu kile ambacho wengi wanafanya kufika hadharani kwa kuwa karibu na kumpa nafasi aliyefikisha. Hilo ndio kosa lako la kwanza. “Kosa” la pili ni unavyoishi. Umeamua kuishi maisha yako vile ambavyo wewe mwenyewe umechagua. Kuna wengi wanakereka bila hata sababu. Ni maisha yako! Kosa sio ‘kibamia’ au kujifuta ulipotoka kuoga. Wengi sana wana ‘vibamia’ na wanaoga na kujifuta. Wengi wamekutana navyo na wanaishi navyo. Wala hakuna kosa kuwa na kibamia. Utu na heshima yako ni zaidi ya kila kitu. Ni huzuni