NI NINI MAANA YA MAPENZI

Katika kuongelea suala zima la mapenzi ni vigumu kujua maana halisi ya mapenzi kwa maana halisi ya mapenzi ni kutokana na mtu mwenyewe anavyoona.

Lakini kwa ujumla mapenzi ni ile hali ambayo watu wawili wanaingia katika mahusiano ambayo yanabeba mambo mengi iliwemo uvumilivu,kuchukuliana katika mambo yote yanayo husu maisha kwa ujumla.

MSINGI HASA WA MAPENZI 
  1. UVUMILIVU
  2. HEKIMA
  3. BUSARA
  4. UPENDO
  5. UWAZI
  6. HESHIMA

1-Uvumilivu katika mapenzi ni suala la msingi sana kwani kama nilivyotangulia kusema kuwa mapenzi ni kama safari ambayo ina mambo mengi ikiwemo mateso na mabadiko mbali mbali. kwa hiyo bila uvumilivu ni kazi bure.
2-Hekima ni hali ya kunyenyekea. ili mapenzi yaweze kuwa mapenzi lazima kuwe na unyenyekevu wa kutosha.
3 Busara ni hali ya kutengeneza uelewano na kuondoa tofauti eitha ya ki maneno au matendo.
4 Upendo ni hali ya kutengenza imani imara na sawia baina yenu wawili.
5 Uwazi ni hali ya kusomana na kufamiana ki myoyo kimwili na kifikra baina ya watu hawa wawili.
6 Heshima nayo pia ni njia kuu ya kuengeneza maelewano sawiya.

Comments

Popular posts from this blog