Posts

Lowassa, Mbowe wamtembelea Kingunge Hospitali

Image
Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa kumjulia hali Mzee Kingunge Ngumbare Mwiru aliyelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili anapopatiwa matibabu. Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake . Hivi karibuni Rais John Magufuli alifika hospitalini hapo kumjulia hali Kingunge ambaye ni miongoni mwa wazee wakongwe kwenye siasa za Tanzania ambaye amewahi pia kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini tangu awamu ya kwanza hadi ya nne.

RAIS MAGUFULI AANIKA MADUDU ZAIDI WIZARA YA MADINI

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanika madudu mengine ya Wizara ya Madini akisema kuwa baadhi ya wateule wake katika wizara hiyo wamekuwa wazembe katika kutekeleza maagizo na kutimiza majukumu yao kama watendaji wa serikali. Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais ametolea mfano wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa bungeni mwezi Julai mwaka jana, ambapo amesema mpaka sasa wizara hiyo haijapitisha kanuni (regulations) ili sheria hiyo iweze kufanya kazi jambo ambalo amesema ni uzembe usiovumilika huku akimwagiza Waziri wa Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kukamilisha kanuni hizo na kuzisaini kufikia Ijumaa ya wiki hii. “Nakushukuru Mhe spika kwa kutoa ushauri kwa serikali na sisi tumekuwa tukiufuata sana. Wizara ya madini ina changamoto sana na hata sasa ina changamoto na haifanyi kazi vizuri. Spika utakumbuka mwezi wa saba mlifany

RAIS ABAINI MADUDU TENA BANDARINI, ATEUA KAMISHNA WA MADINI

Image
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kuwa Kamishna wa Madini. Rais ametangaza uteuzi huo leo Jumatatu Januari 8, 2018 alipokuwa akitoa hotuba fupi mara baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini. Nimesikia tatizo ni kamishna wa madini, sasa nimeamua kumteua kamishna mpya wa madini, jina lake linaanza na Prof. Shukrani Elisha, huyo atakuwa ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa madini. Mambo ya hovyo ni mengi mno, nilipotembelea bandarini niliunda katume kasirisiri hivi, kwa kulihusisha Jeshi la Wananchi, TISS na Polisi. Yanayogundulika huko ni ya ajabu, kuna hadi simenti za zamani sana, yapo makontena bandarini na pale Ubungo. Mimi sio mwanasiasa mzuri wa kubembelezabembeleza, nikitoka mimi mtapata wakubembeleza, ila mimi nataka kabla ya Ijumaa regulations (kanuni za sheria ya madini) ziwe zimesainiwa. Pro Kabudi nendeni mkazifanyie kazi, tafuta watu wa kukusaid

BREAKING NEWS: NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARALA LA NNE

Image
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifaulu vizuri katika mitihani hiyo. Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu, Januari 8, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo. Amesema wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha. Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu. Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwaweze

Pretty Kind afungiwa miezi sita kwakutoa Wimbo usio na maadili

Image
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amemfungia msanii Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind kujihusisha na sanaa kwa muda wa miezi sita. Akizungumza leo Jumapili Januari 7 jijini Dar es Salaam, Shonza amesema amechukua hatua hiyo kutokana na msanii huyo kutoa wimbo uitwao ‘viduduwasha’ usio na maadili. Msanii huyo pia amekutwa na kosa la kufanya  kazi ya sanaa bila kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuweka mtandaoni picha ya nusu utupu kinyume na maadili. ‘’Kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii kutoa nyimbo zenye maneno ya matusi na zisizo na maadili, pamoja wanawake kupiga picha wakiwa wamevaa nusu utupu na kuweka picha hizo katika mitandao,” amesema Shonza na kuongeza, “Nataka kuwapa angalizo wasanii wenye tabia hizi kuwa Serikali inawafuatilia kwa karibu na mwaka huu tumeanza na huyu na wengine wanafuata kama msanii Gift Stanford maarufu kama Gigy Money na  Jane Rimoy maarufu kama Sanchi.” Shonza amemtaka msanii

Madereva boda boda wenye hasira wateketeza Basi kwa moto

Image
Madereva wa Boda boda wenye hasira wameliteketeza Basi la abiria la Kampuni ya Simba  Coach lililokuwa linatokea jijini Nairobi kwenda Malindi nchini Kenya jana mchana. Basi hilo ambalo kabla ya tukio hilo mashuhuda wamesema kuwa lilimgonga muendesha bodaboda mmoja na kufa hapo hapo lakini halikusimama kitu ambacho kilipelekea waendesha boda boda kuanza kulikimbiza. Wakielezea tukio abiria wamesema dereva wa Basi alitaka ku-overtake gari ndogo katika eneo la Kijiwetanga na ndipo alipomgonga dereva huyo wa Boda boda. Abiria wamesema baada ya Basi hilo kusimamishwa na madereva boda boda waliamuriwa kutoka kwenye Basi hilo kabla ya kulichoma moto. Tayari Kamanda wa Polisi mjini Malindi,  Matawa Muchangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na dereva wa gari hilo bado anatafutwa huku Dereva wa boda boda aliyegongwa mwili wake umepelekwa katika Hospitali ya Malindi. Chanzo:The Star Kenya

Tundu Lissu Awasili Ubelgiji Kwa Ajili Ya Matibabu Ya Mazoezi Ya Viungo

Image
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu akiwa na madaktari baada ya kufika Ubelgiji. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amewasili katika uwanja wa ndege jijini Brussels, nchini Ubelgiji ambapo amepelekwa kwa ajili ya awamu ya tatu ya matibabu yake yatakayohusisha mazoezi ya viungo. Tundu Lissu amewasili jijini hapo akitokea katika Hospitali ya Nairobi, nchini Kenya alikokuwa anapatiwa matibabu kwa muda wa takribani miezi minne sasa kutokana na kushambuliwa kwa risasi mnamo septemba mwaka jana mkoani Dodoma Mbunge Tundu Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka Bungeni, majira ya saa 7 mchana, karibu na nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma. Kwa mujibu wa taarifa ya madaktari waliokuwa wanamtibu, walieleza kuwa jumla ya risasi 16 zilimpata Tundu Lissu mwilini mwake na wamefanikiwa kuzitoa 15, isipokuwa moja ambayo ipo nyuma ya uti wa mgongo. Tundu Li

MENEJA WA WAKALA WA MAJENGO (TBA) KIGOMA AKAMATWA

Image
  Jeshi la polisi linamshikilia Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Mgalla Mashaka kwa tuhuma za kushindwa kukarabati Shule ya Sekondari Kigoma. Meneja huyo alikamatwa akituhumiwa kushindwa kukarabati shule ya sekondari Kigoma kwa wakati licha ya kupewa zaidi ya shilingi milioni mia nne kati ya mia tisa tangu mwezi wa nane mwaka jana. Mhandisi Mgalla amekamatwa baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, kufanya ukaguzi katika shule hiyo ambayo imeanza kupokea takribani wanafunzi elfu moja huku katika miezi mitano ya ukarabati hadi sasa ukarabati wa vyoo, mabweni, maabara na vyumba vya madarasa haujakamilika Prof. Ndalichako amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBA kufika Kigoma kutatua tatizo hilo ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea. Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kujenga vyoo vya muda ili wanafunzi waweze kuanza masomo wiki ijayo. 

Breaking News: BOT yazifutia leseni Benki Tano

Image
 Benki Kuu ya Tanzania(BoT) imezifutia  leseni ya kufanya biashara benki tano na kuziweka chini ya ufilisi. Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na BoT imezitaja benki hizo kuwa ni Covenant Bank For Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited. BoT imeeleza kuwa imefanya hivyo kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 56(1)(g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2)(i), 11(3)(c) na (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuzifunga; kusitisha shughuli zake zote za kibenki; kufuta leseni zake za biashara ya kibenki; na kuziweka chini ya ufilisi. “Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu Na. 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006; Benki Kuu ya Tanzania imeiteua Bodi ya Bima ya Amana (The DEPOSIT INSURANCE BOARD) kuwa mfiiisi kuanzia tarehe 04 Januari 2018,” imeeleza taarifa hiyo.” “Ua

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA UGANDA YOWERI MUSEVENI, WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UGANDA SAM KUTESA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. < Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe maalum wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Ujumbe Maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiufungua na kuusoma Ujumbe huo maalum uliotoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni na kuwasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa

NUNUA JIKO TUKUPELKEE HADI KWAKO BUREEE (DAR) NA ZAWADI YA MAFUTA BUREEEE

Image
Kwa Mara nyingine tena Bngo Deco Electronics, tunakuletea majiko makubwa ya kupikia kwa bei poa kabisa. Majiko haya yanadumu sana na yanakuja na warranty  ya mwaka mmoja, likisumbua tu tutakurekebishia. Nakwa kuthamini mchanngo wa Muungwana Blog kila mteja atakatoka katika Muungwana atapew dumu la mafuta ya alizeti BUREE na kama yupo Dar tutampelekea BUREE hadi kwake.   Kwa wateja wa mkoani gharama za kutuma jiko kwenda mkoani ni jukumu la mteja mwenyewe ila kama ni kumpelekea kwenye basi au lori la kuja mkoani basi tutatoa usairi BUREE hadi sehemu ya kutumia. Tupo Magomeni Mapipa mtaa wa Idrissa karibu kabisa na Butiama Restaurant.

NANDY ACHARUKA BAADA YA TAARIFA KUSAMBAA KUWA ANATOKA NA RUGE MUTAHABA.

Image
January 3, 2018 kumekuwepo na post kwenye mitandao ya kijamii kuhusu msanii Nandy kudaiwa kutoka kimapenzi na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Nandy ameamua kuandika kwenye ukurasa wake wa Istagram kuhusu tuhuma hizo. Nandy Kupitia ukurasa wake wa Isntagram ameandika kuwa. “Mtu akifanya mziki wake kwa amani bila drama kuna watu wanakuwa hawatosheki kabisa. hivi mimi ni kichaa mpaka kujiachia kama uyo msambaza habari anavyo sambaza!” “Kwani suala la watu kusema na toka na boss wangu nalijua leo au nigeni kwangu sana mpaka nijiachie kwenda naye ma camp sijui ma club kama mnavosema???” – Nandy “Embu tuwe na utu please kwa hiyo me nimekuwa wakuja kiasi kwamba mshamba kiasi nikashindwa kujificha na mashungi juu basi kama ni hivyo  tumeshindwa kupishana kusafiri atangulie ndo nifuate,”– Nandy “Kwani sijui hata kama ingekuwa ni kwa nia nzuri  msingesema mnazani mambo ni marahisi kiasi hicho tupeane heshima kuna watu wengine hat

Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Aitwa Polisi

Image
MBUNGE wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ na mratibu wa chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameitwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo huku wakisema hawajui sababu ya wito huo. Wawili hao wamesema wanahisi wito huo unatokana na mkutano wa hadhara alioitisha mbunge huyo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Sugu amesema leo Jumanne kuwa, juzi jioni alipigiwa simu na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya (RCO) kwamba yeye na Masonga wafike jana ofisini kwa ajili ya mazungumzo lakini alimueleza kuwa itakuwa ni siku ya sikukuu hivyo itakuwa vigumu ngumu kwenda, hivyo walikubaliana wafike leo. “Polisi walinipigia simu juzi jioni wakinitaka mimi na Masonga twende Makao Makuu ya Polisi jana, nikawaambia itakuwa ni sikukuu hivyo tukakubaliana leo asubuhi. Sasa hivi tupo njiani tunaelekea huko kuitika wito. Sijajua sababu, lakini nadhani ni uchochezi,” amesema Sugu. Masonga amesema anaamini sa

Ikulu yatoa neno kuhusu kutokuapishwa kwa Dk. Slaa

Image
Balozi, Dk. Willibrod Slaa. WAKATI zikiwa zimetimia siku 40 baada ya kuteuliwa kuwa balozi, Dk. Willibrod Slaa (pichani), hajaapishwa na kuzua minong’ono hatimaye Ikulu imefunguka na kuweka kila kitu wazi. Itakumbukwa kuwa Rais Dk. John Magufuli alitangaza uteuzi wa Dk. Slaa kushika nafasi ya ubalozi Novemba 23, mwaka jana, lakini tangu wakati huo hajaapishwa. Rais Magufuli amekuwa na utamaduni wa kuteua viongozi na baada ya siku chache wanaapishwa, lakini kwa Dk. Slaa imechukua muda mrefu na kuibua sintofahamu. “Hili ni jambo ambalo siyo la kawaida, tumezoea mtu akiteuliwa kushika wadhifa fulani na rais baada ya siku chache, tunaona au kusikia kuwa ameapishwa, lakini kwa Dk Slaa ni zaidi ya mwezi sasa, kuna sababu zimetolewa? Tujulisheni,” ni moja kati ya simu nyingi za wasomaji wetu waliopiga chumba cha habari kutaka ufafanuzi. Kutokana na hali hiyo, Uwazi liliwasiliana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ili kujua kwa nini imechukua muda mrefu kumuapisha Dk

SIWEMA AFUNGUKIA KUMUONA MWANAYE KWA NAY

Image
Nay wa Mitego akiwa na watoto wake. MZAZI mweza wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Siwema Edson amefungukia ishu ya kumuona mwanaye, Cartes kuwa, si kweli kwamba hajawahi kumuona tangu aondoke kwa jamaa huyo. Siwema mwenye maskani yake jijini Mwanza aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, si kweli kwamba hajawahi kuomuona mtoto wake kwani mara nyingi anapokwenda kumuona kwa mama wa mwanamuziki huyo, Nay anakuwa hajui. “Naongea naye kila mara, nimeshakwenda kumuona zaidi ya mara tatu, sema tu baba yake hajui hivyo angekuwa anamuuliza mama yake angempa jibu,”   alisema Siwema.

Uchangudoa wa Zari Waibua Kimbembe!

Image
MAMBO ni moto! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kukiri kuwa yeye ni changudoa mzee, kauli yake imeibua kimbembe. KUPITIA SNAPCHAT Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Snapchat, mwishoni mwa wiki iliyopita, Zari alitupia ujumbe akionesha kuwa yeye ni changudoa mzee, lakini mwenye mafanikio akimjibu hasimu wake, mwanamitindo Hamisa Mobeto bila kumtaja. “Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+, mama uliyeachwa mara mbili na tuzo juu,” alisema Zari kupitia Snapchat. Kwa muda mrefu, Zari amekuwa kwenye tifu la aina yake baada ya Mobeto kuzaa na bwana wake, msanii wa Bongo Fleva miezi michache iliyopita. KIBEMBE KILIVYOIBUKA Kitendo cha Zari kutoa kauli hiyo, kimbembe kiliibuka mtandaoni mara baada ya ukurasa wa Instagram wa Global Publisher, kutupia habari hiyo ambapo wafausi wa mtandao huo walianza kurushiana maneno makali huku kila m