Posts

Shule iliyotokea mlipuko wa bomu yafungwa

Image
Uongozi wa  Shule ya Msingi  Kihinga umaamua kuifunga kwa muda shule hiyo kwa lengo la kuwajenga kisaikolojia wanafunzi wake baada ya wenzao kupoteza maisha kutokana na mlipuko wa bomu. Akizungumza  Mwananchi leo Novemba 10 ,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aidan Makobero amesema   shule hiyo imefungwa kimasomo hadi Jumatatu ili wanafunzi waweze kupata malezi ya  kisaikolojia Aidha amesema kwa shule jirani  ya Nyarukubala iliyo karibu na mpakani na  Burundi mahudhurio yamepungua kutoka wanafunzi 700  na kufikia 100  leo  Novemba 10 “Hata shule nyingine ya Nyarulama nayo wanafunzi wake wamepungua  baada ya tukio la shuleni kwangu na kusalia majumbani wakiogopa kwenda shule wakidai nao wanaweza kukumbwa na tukio  kama la shule jirani’’ amesema  Makobero Pia majeruhi 33 kati ya 42 waliojeruhiwa kwa bomu wameruhusiwa na kurejea makwao baada ya afya zao kuimarika Mganga wa hospitali ya misheni ya Rulenge Dk Mariagoleth Frederick amesema majeruhi hao  ni wanafunzi w

Polisi wamnasa muuza risasi za kivita

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watu wawili kwa mahojiano baada ya kukamatwa na risasi za kivita ambazo wanazimiliki kinyume na sheria. Akitoa taarifa kwa Wanahabari Kamanda Mambosasa amesema kwamba Novemba 6 mwaka huu maeneo ya Serengeti Kigamboni lilipokea taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Willy Peter kuwa anafanya biashara ya kuuza risasi mtaani. Amesema kwamba baada ya kupata taarifa hizo Polisi walifanya ufuatiliaji na hatimaye kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na risasi 69 za kivita aina ya FN G3. Kamanda Mambosasa amefafanua kwamba baada ya  mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa risasi hizo alipewa na mtu aliyemtaja kwa jina la Matabu William kwaajili ya kwenda kuziuza na kwamba alimpatia risasi hizo huko nyumbani kwake Kiwalani jijini Dar es salaam. Hata hivyo polisi walifika nyumbani kwa Matabu William Matoke (52) kiwalani ambapo alikiri kufanya biashara hiyo ya risasi na alipopekuliwa katika nyumb

Saada Mkuya amshukia Waziri wa fedha

Image
Waziri wa Fedha wa utawala uliopita wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Saada Mkuya amemshukia Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango kwa kuandaa mpango wa taifa wa maendeleo pasina kuihusisha Zanzibar. Mkuya ambaye ni mbunge wa Welezo visiwani Zanzibar amesema Dk Mpango amekuwa na kawaida ya kutokujibu hoja ambazo zinatolewa na wabunge wa kutoka Zanzibar jambo ambalo limemsikitisha. Akichangia leo Novemba 10 bungeni mjini Dodoma Mpango wa Maendeleo ya Taifa, Mkuya ambaye katika mchango wake alisikitishwa na jinsi Waziri Mpango anavyoitenga Zanzibar licha ya kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Nadhani taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaundwa na pande mbili sasa Mheshimiwa Mwenyekiti  (Azzan  Zungu) cha kusikitisha na fedheha kabisa ni kuona hakuna hata eneo moja lililopangiwa mpango angalau tu likaelekezwa katika upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Mkuya “Hili niliseme wazi mheshimiwa mwenyekiti kupitia kwako

MSHTAKIWA SETHI AIOMBA MAHAKAMA IMRUHUSU KWENDA KUPATIWA MATIBABU YA PUTO LAKE NCHINI AFRIKA KUSINI

Image
Mshtakiwa Harbinder Singh Sethi,ameoimba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumruhusu kwenda kupatiwa matibabu ya puto lake lililoisha muda nchini Afrika Kusini kwa daktari wake maalumu kwa madai ya kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemueleza kuwa hawawezi kufanya upasuaji huo.Maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo na wakili wake, Joseph Sungwa leo Novemba 10/2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakati shauri hilo linalomkabili Sethi na James Rugemarila lilipopelekwa kwa kutajwa na Mawakili wa Serikali, Vitalis Peter na Leonard Swai kudai upelelezi haujakamilika. Ili mshtakiwa aweze kuja mahakamani kuudhuria kesi yake na hatimae kuweza kujitetea, tunaomba kama inawezekana aende kumuona daktari wake ambaye anaishi Afrika Kusini kwa matibabu”, alidai Sungwa.Ombi hilo lilipingwa vikali na wakili wa serikali,Swai akidai Muhimbili haijashindwa kumfanyia upasuaji wa puto mshitakiwa huyo, bali anajicheleweshwa mwenyewe kutokana na kutaka uwep

HAMISA MOBETTO AANGUKIA PUA KESI YAKE,MAHAKAMA YAAMUA HAYA LIVE

Image
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya Mwanamuzi Naseb Abdull ‘Diamond Platnum’ kuhusu matunzo ya mtoto.Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Hakimu, Devotha Kisoka baada ya kusikiliza hoja za pande mbili ukiwemo wa Diamond ambaye aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto. Katika uamuzi wake, Hakimu Kisoka alisema anakubaliana na hoja za upande wa mlalamikiwa kwamba kulikuwa na upungufu katika ufunguaji wa kesi hiyo.Kwa mujibu wa pingamizi lililowasilishwa na Diamond mahakama hapo, alidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa na Mobeto kupitia jopo la mawakili wake. Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine aliiomba mahakama imuamuru Diamond atoe matunzo ya mtoto waliozaa.Mobeto aliiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi ya Sh.mil 5 ambapo al

Kagasheki amvaa Kigwangalla

Image
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki amemvaa Waziri wa sasa wa sasa wa wizara hiyo Mh. Hamisi Kigwangalla kwa kumtaja kuwa ana mahusiano ya karibu na Mkurugenzi wa OBC ambaye ana kashfa kubwa ya rushwa. Kupitia mtandao wake wa Twitter Balozi Kagasheki alimtaka Mh. Kigwangalla amthibitishie kuhusu ukaribu wake na Mkurugenzi huyo na kuhusu rushwa aliyowahi kupokea ikiwa ni pamoja na kuuza vitalu. Balozi ameandika "Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla alinukuliwa kutaja "muwekezaji OBC" alivo na kashfa za Rushwa. Alinitaja mimi kuwa karibu na OBC. Napenda athibitishe ukaribu huo, vitalu nilivogawa nikiwa Waziri na rushwa niliyopokea," Balozi Kagasheki Hata hivyo baada ya ujumbe huo ambao ulienda moja kwa moja kwa Waziri Kigwangalla naye alijibu ujumbe huo ambao ulielekezwa kwake na kumuomba Mstaafu huyo wayazungumze nje ya mtandao "Mhe. Balozi Kagasheki , wewe ni kaka yangu na unajua nakuheshimu

Mchakato Katiba Mpya, Watolewa Majibu na Waziri Mkuu

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa Changamoto za jamii ni nyingi kuliko mahitaji ya Katiba hivyo suala la katiba sio kipaumbele cha serikali kwa sasa. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, ambapo alijibu swali la Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea lililohoji kuwa ‘Serikali ya awamu ya tano imetimiza miaka miwili lakini hakuna jitihada zozote zilizofanywa katika kuendeleza mchakato wa katiba ulioachwa na Serikali ya awamu ya nne. Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amefafanua, “Katiba mpya inahitaji gharama kubwa na sisi tumeanza na kutatua changamoto za jamii kwanza, ikiwemo mahitaji ya maji, changamoto za elimu, na sekta ya Afya”. Amesema Waziri Mkuu Waziri Majaliwa ameongeza kuwa Katiba ni muongozo tu na wakati ukifika serikali yake imemaliza changamoto basi wataanza mchakato huo. “Kila bajeti ina vipaumb

Breaking News: Rais Magufuli amtumbua Mkurugenzi mwingine Tunduru

Image
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 November 2017 ametengua uteuzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Bwa. Abdallah Hussein Mussa kwa kushindwa kumudu majukumu yake.

Rais Magufuli Anastahili Pongezi, Amefunua Blanketi Lililotufunika

Image
Rais Dk. John Pombe Magufuli. M UNGU ni mwema kwa sababu ametufikisha leo tukiwa wazima, hakika ahimidiwe daima. Leo nachukua nafasi hii kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa mafanikio aliyotuletea ndani ya miaka miwili ya utawala wake. Ninapofanya tathmini ya miaka miwili ya uongozi wa Rais Magufuli, ni kama narudia kwa sababu juzi na jana wengine wameandika au kusema kupitia vyombo vya habari. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 na Rais Magufuli kuibuka mshindi, alianza kuonesha kwa haraka kuwa yeye ni kiongozi asiyetaka mchezo kwenye kazi. Aliliambia taifa kuwa alipokea nchi ikiwa imejaa uozo kila idara na alitumia hoja hiyo kukataa hoja ya kupendekezwa kwa Katiba Mpya, iliyowahi kutolewa na baadhi ya watu wakati alipotimiza mwaka mmoja madarakani kwa kusema wazi, ‘niacheni niisafishe nchi kwanza.’ Mwaka wake wa kwanza alifanya mengi yaliyowafurahisha wananchi wengi, kama vile kufuta safari za nje kwa maofisa wa serikali labda kama ni za lazima s

Waziri Wa Tamisemi Atoa Maagizo 6 Kwa Wakuu Wa Mikoa

Image
Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo. Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, ametoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya darasa la saba. Waziri Jafo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo, ameeleza kwamba jumla ya watahiniwa 909,950 walifanya mtihani ambapo watahiniwa 662,035 wamefauli kwa daraja A – C ikiwa ni sawa na 72.76% ya watahiniwa wote. Kufuatia ufaulu mkubwa uliojitokeza ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikalli za Mitaa, imetoa maelekezo kwa mikoa yote ili waweze kuanza maandalizi mapema ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mapema mwakani kabla ya kukamilika kwa uchaguzi wa wanafunzi hao. Ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu mitihani wanapata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza Januari 2018, maelekezo yafuatayo yametolewa. 1. Wakuu wa Mikoa yote wametakiwa kuhakikisha kuwa miundo

BREAKING NEWS: Gavana afariki katika ajali, Kenya

Image
Gavana wa kaunti ya Nyeri nchini Kenya, Wahome Gakuru amefariki mapema siku ya Jumanne kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika eneo la Kabati katika barabara kuu ya Thika-Sagana katika kaunti ya Murang’a. Alikimbizwa katika Hospitali ya Thika Level 5 kwa matibabu ya dharura lakini akaaga dunia. Kaunti kamishna wa Murang’a John Elungata alithibitisha kifo hicho. Bwana Elungata alisema kuwa kabati ni eneo hatari na madereva hukosa mwelekeo kila kunaponyesha. Maafisa wa polisi wanasema kuwa gari la gavana huyo lilikuwa na abiria wanne wakati wa ajali hiyo ,akiwemo msaidizi wake wa kibinafsi, mlinzi wake na Dereva. Mkono na mguu wa msaidizi wake wa kibinafsi ilivunjika huku miguu ya mlinzi wake ikijeruhiwa vibaya huku Dereva akidaiwa kuwa katika hali nzuri. Polisi wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gurudumo moja la gari hilo kupasuka wakati mvua kali ilipokuwa ikinyesha. Mwili wa Gavana huyo umesafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Le

NDOA YA IRENE UWOYA NA DOGO JANJA NI BATILI,MASHEHE WAFUNGUKA HAYA LIVE

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na mwigizaji Irene Pancras Uwoya wakifanya yao baada ya kufunga ndoa.WAKATI sakata la ‘ndoa’ ya msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na mwigizaji Irene Pancras Uwoya likizidi kupamba moto, mashehe mbalimbali wameibuka na kutoa sababu zinazodhihirisha kuwa ndoa hiyo ni batili, Ijumaa Wikienda linakupakulia ubuyu wa motomoto. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Ijumaa Wikienda, mashehe watatu wa misikiti tofauti jijini Dar, walioomba hifadhi ya majina, walimkosoa Uwoya na Dogo Janja kwa kuonesha kwamba walichokifanya si sahihi. NI BATILI Mashehe hao walisema kuwa, ndoa hiyo ni batili kutokana na jinsi ilivyofungwa, lakini pia hata kama walikuwa wanafanya filamu, bado walikiuka taratibu za Dini ya Kiislam. Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmoja wa mashehe hao alianika sababu tano (5) zinazodhihirisha kwamba ndoa hiyo ni batili; SABABU YA KWANZA (MATITI NJE) Alisema kuwa, katika picha mbalimbali z

SERIKALI YASEMA HAIWEZI KUAJIRI VIJANA WOTE NCHINI

Image
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde. Serikali kupitia Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde amesema kuwa si kweli kwamba serikali inaweza kuwaajiri wote kwenye sekta ya umma ila inachokifanya ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo ufugaji na biashara.Mh. Mavunde ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Aida Joseph Kenani lililohoji, serikali ya awamu ya tano imepunguza wafanyakazi kwenye kada mbalimbali kwa kigezo cha kutokuwa na sifa. Je, ni lini sasa serikali itatoa ajira kwa kuwapa kipaumbele vijana wa nchi ambao kwa sasa ni wengi wamerundikana mtaani. “Katika azma ya kutengeneza nafasi nyingi za ajira hasa kwa kundi kubwa hilo la vijana serikali, imekuja na mipango mikakati mbalimbali, si kweli kwamba tunaweza tukawa tuna nafasi za kuwaajiri wote kwenye sekta ya

Vyakula Vinavyosaidia Kuondoa Maumivu Wakati Wa Hedhi

Image
WIKI iliyopita tuliona jinsi matunda yanavyosaidia kutibu maradhi mbalimbali mwilini, leo tutaangalia aina mbalimbali za matunda yanayoweza kutibu matatizo mbalimbali yanayowahusu wanawake wakati wa siku zao (menstruation period). Miongoni mwa matunda hayo ni papai bichi lakini lililokomaa ambalo lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya kipindi cha hedhi kutokuwa na maumivu. Katika suala hili, ili wanawake kujiepusha na kupatwa na matatizo ya maumivu, kutokwa damu kwa wingi kusiko kawaida, kuchelewa kuona siku zao, wanashauriwa kuzingatia suala la lishe. Wanapaswa kujua vyakula gani wale na vipi wasile ili kujiwekea kinga ya kudumu dhidi ya tatizo hili. LISHE YA KUDHIBITI MATATIZO YA HEDHI Matatizo mbalimbali yanayohusiana na hedhi, yanaweza kudhibitiwa na hatimaye kutokomezwa kabisa kwa kutibu mfumo mzima wa mwili, ili kuondoa sumu iliyojilimbikiza katika mwili wa mgonjwa kwa kipindi cha muda mrefu, sumu ambayo imegeuka na kuwa chanzo ch

Kunyonyana ulimi au kula mate Kunasababisha kuambukiza VVU?

Image
Swali:  Je kunyonyana ulimi au kula mate kunaweza kuambukiza VVU? Jibu: Njia ya mdomo inaweza kuchangia mtu kupata VVU kama mtu atakutana na mtu mwenye VVU mwenye vidonda au michubuko mdomoni nawe pia ukawa una michubuko au vidondamdomoni, ili kuweza kupata VVU kwa njia ya mate inabidi kulambamate lita 2 jambo ambalo ni gumu.

RAIS DKT. MAGUFULI AKIFUNGUA UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wa pili kutoka (kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuashiria ufunguzi rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi hao mara baada ya ufunguzi wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya ufunguzi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald kuashiri

Wakili Msomi Atinga Mahakamani Kudai Wanaume Wafutiwe Mahari

Image
Wakili msomi nchini Zimbabwe, Bi. Priccilar Vengesai ameanzisha kesi mahakamani ya kufutilia mbali mahari zinazotolewa na wanaume pale wanapooa akidai kuwa ni mila iliyopitwa na wakati. Tokeo la picha la pete ya ndoa Wakili huyo amewasilisha malalamishi yake katika mahakama juu nchini humo akitaka kusikilizwa kwa kesi yake huku akilalamika kuwa utamaduni huo unakiuka haki za kibinaadamu. Bi. Priccilar Vengesai anaamini kuwa endapo utamaduni huo utaendelea ,familia zote za mume na mke zinatakiwa kulipa mahari kwa maslahi ya usawa wa kijinsia. Akizungumza na gazeti la serikali nchini Zimbabwe la Herald, Wakili huyo amesema kuwa anataka kuolewa upya baada ya ndoa yake ya kwanza kuvunjika kwani hakuwa na sauti ya kuhoji kiasi cha mahari iliyotolewa na kujiona kama bidhaa. “Nataka kuolewa tena sitaki kupitia kama niliyopitia kwenye ndoa yangu kwani sikushiriki katika kuuliza gharama ya mahari. Sikupewa fursa ya kuuliza kwa nini mahari ilitolewa wa

RAIS MAGUFULI AAMURU WATATU KUCHUNGUZWA KWA KUTAKA KUIIBIA SERIKALI MABILIONI

Image
RAIS Dk. John Magufuli, ameamuru kukamatwa kwa watumishi watatu wa serikali, kwa tuhuma za kuandika madai yasiyo halali, kwa lengo la kuiibia serikali.Rais Magufuli ametoa amri hiyo wakati akizindua Uwanja wa Ndege wa Bukoba wenye urefu wa kilomita 1.5 ambapo amewataja watumishi hao kuwa ni Jackson Kaswahili Robert, Mwachano Msingwa na Gidioni Zakayo. Alifafanua kwamba, Jackson alijaza fomu zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.626 lakini madai hayo yalipochunguzwa, ilibainika kuwa hadai chochote.Akaongeza kwamba Mwachano yeye alijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.754 wakati ukweli ni kwamba anaidai shilingi milioni 2 tu huku Gidioni ZakayoAkijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi milioni 104 wakati si kweli.Hawa wote pamoja na maofisa wizarani walioidhinisha malipo haya, naagiza vyombo vya dola viwashughulikie. Tumekuwa na watu ambao hawana uchungu na wengine,” alisema Rais Magufuli.

Wanachama 12 wa Chadema Wafikishwa Makamani Arusha

Image
Wanachama 12 wa Chadema mkoani Arusha wanaotuhumiwa kumshambulia mgombea udiwani wa CCM katika Kata ya Muriet, Francis Mbise wamefikishwa Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso iliyopo jijini Arusha leo. Miongoni mwa washtakiwa hao ni Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Innocent Kisanyage na mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Mlimani, Yohana Gasper. Baada ya kufikishwa mahakamani wamepelekwa mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabili

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ulioanza leo tarehe 6 na unatarajiwa kumalizika tarehe 8 november, katika ukumbi wa APC Bunju, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)         Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna ya mashine ya kuchora kadi za mifumo ya umeme inavyofanya kazi na Mhandisi Vedastus Sichilima kutoka D.I.T (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​ Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, leo amefungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi. Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya APC Bunju wilayani Kinondoni, umeandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikianana Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ya nchini Finland. Akihutubia washiriki katika