HAMISA MOBETTO AANGUKIA PUA KESI YAKE,MAHAKAMA YAAMUA HAYA LIVE

 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya Mwanamuzi Naseb Abdull ‘Diamond Platnum’ kuhusu matunzo ya mtoto.Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Hakimu, Devotha Kisoka baada ya kusikiliza hoja za pande mbili ukiwemo wa Diamond ambaye aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto.

Katika uamuzi wake, Hakimu Kisoka alisema anakubaliana na hoja za upande wa mlalamikiwa kwamba kulikuwa na upungufu katika ufunguaji wa kesi hiyo.Kwa mujibu wa pingamizi lililowasilishwa na Diamond mahakama hapo, alidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi.
Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa na Mobeto kupitia jopo la mawakili wake.


Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine aliiomba mahakama imuamuru Diamond atoe matunzo ya mtoto waliozaa.Mobeto aliiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi ya Sh.mil 5 ambapo alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.

Pia kupitia hati ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.Katika kesi hiyo, Diamond kupitia mawakili wake aliwasilisha hati ya majibu kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh.mil 5 kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

Comments

Popular posts from this blog