Posts

Hali Ilivyo Jijini Nairobi… Raila Odinga Vs Jeshi la Polisi

Image
POLISI Kikosi cha Kuzuia Ghasia wamefunga eneo lote la viwanja vya Uhuru Park jijini kabla ya mkutano ulioandaliwa na muungano wa National Super Alliance (NASA) kwa ajili ya kiongozi wake mkuu Raila Odinga kutoa tamko zito kuhusu mchaguzi wa marudio kesho. Maofisa wa polisi wakiwa katika sare zao wamesambazwa muda mfupi baada ya uongozi wa Kaunti ya Jiji la Nairobi kumwandikia kamanda wa Japhet Koome akipinga uwanja huo kutumiwa na Nasa. Gavana wa Nairobi Mike Sonko amemtaka kamanda Koome kuhakikisha eneo hilo linakuwa na usalama akihofia unaweza kutumika kwa “mkutano ambao haujaruhusiwa”. “Nimefahamishwa kwamba viongozi wa National Super Alliance (Nasa) wanapanga kutumia viwanja vya Uhuru Park kwa mkutano wa kisiasa leo. Hata hivyo, rekodi za uongozi wa jiji zinaonyesha hawajafuata utaratibu wa kupata kibali kwa ajili ya mkutano huo,” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Kamanda Koome. Sonko amesema hakuna mkutano utakaoruhusiwa kwenye viwanja hivyo bila ya ri

Zitto Kabwe: Nipo Tayari Kuwajibika Rais Akitekeleza Ombi Hili

Image
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa atakuwa tayari kuwajibika endapo Rais Dkt John Magufuli ataruhusu uchunguzi huru wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na mapato ya serikali yatakutwa hayajashuka kama ambavyo amekuwa akisema. Zitto ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu Rais Magufuli alipokanusha madai yake akivitaka vyombo vya dola kuwafikisha mahakamani  watu wanaobadilisha takwimu za serikali wakiwamo wanaosema kuwa mapato ya serikali yameshuka wakati sio kweli ili wakathibitishe kauli yao. “Kama Rais anaamini kuwa Mapato hayajaporomoka, aruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye Mapato ya July na Agosti 2017 na ukaguzi huo uwekwe wazi Kwa umma. Rais akifanya hivyo NITAWAJIBIKA.” Katika taarifa yake, Zitto amezidi kusimamia msimamo wake akidai kuwa taarifa za mapato za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni za uongo, na kwamba,  taarifa ya kupikwa kwa takwimu za Pato la

Mbunge ashtakiwa kwa kukojoa hadharani Uganda

Image
Mahakama moja nchini Uganda imempiga faini ya Shilingi 40,000 za Uganda mbunge mmoja nchini humo kwa makosa ya kukojoa hadharani. kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya Mbunge Ibrahim Abiriga wa manispaa ya Arua siku ya Jumanne aliwasili mbele ya mahakama ya mji wa Kampala na kushtakiwa kwa kukojoa katika ukuta wa jumba la wizara ya fedha. Alikiri kufanya makosa hayo na akaachiliwa baada ya kulipa faini. Kwa mujibu wa gazeti hilo Kiongozi wa mashtaka aliambia mahakama kwamba mbunge huyo alifanya makosa hayo mwezi Septemba 25 mwaka huu katika barabara ya Kyaggwe mjini Kampala. Upande wa mashtaka ulisema kuwa vitendo vya mbunge huyo vilikuwa kinyume na sheria za baraza la manispaa ya Kampala za 2016. Kukiri kwake kunajiri baada picha kadhaa za yeye akikojoakando kando ya barabara kusambaa katika mitandao ya kijam

Zijue sababu zinazopelekea wapenzi wengi kuchokana mapema

Image
Hivi uliwahi kujiuliza hivi ni kwanini baadhi ya mahusiano ya kimapenzi hufa mapema, kama si kufa basi kushuka kwa mahusiano hayo? Moja kati ya sababu ambayo husababaisha kufa kwa mahusiano ni ile tabia ya kuchokana mapema katika mahusiano na moja kati ya sababu kubwa ambayo hupelekea kuchokana mapema ni: 1. Mazungumzo Mazungumzo ni njia muhimu ya kujenga ndoa na kuiimarisha , aidha ni njia ya mkato ya kuchokana na kuchukiana. Mwanamke ambaye hajui wakati gani aseme nini na wakati gani asiseme, hujikuta katika wakati mgumu ndani ya ndoa yake. Kwa mfano: Mwanamke ambaye kila anapoongea na mume wake huanza mazungumzo yake na matatizo na lawama humfanya mumewe awe na woga kila anaposikia sauti yake, na kuiona nyumba chungu, kwa sababu hakuna binadamu anayependa kusikia matatizo tu wakati wote Mwanamke wa aina hii huwa anamsubiri mumewe kwa hamu kubwa, na anapofika tu na kabla hata ya kupata rizki, anaanza kumsomea orodha ya matatizo; watoto wamerudishwa shule, karo h

Prof. Luoga Afunguka Baada ya Kuteuliwa Kuwa Gavana Benki Kuu

Image
Profesa Florens Luoga. Gavana mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amesema amepokea kwa heshima kubwa dhamana aliyopewa na Rais John Magufuli na anatambua changamoto za nafasi hiyo. Profesa Luoga ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) – Taaluma, amesema leo Jumatatu Oktoba 23,2017 kuwa atatumia wataalamu wa BoT kufanya kazi. Amesema anahitaji ushirikiano wa kila mtu katika kufanikisha kazi aliyopewa. “Nimepokea kwa heshima dhamana niliyopewa nikitambua kwamba zipo changamoto. Nitakwenda kujifunza zaidi kwa sababu sijawahi kuwa Gavana, nitatumia wataalamu waliopo katika kutekeleza majukumu yangu,” amesema Profesa Luoga. Rais Magufuli Julai 11,2017 alimteua Profesa Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akichukua nafasi ya Bernard Mchomvu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Novemba mwaka jana na bodi hiyo kuvunjwa. Profesa Luoga ni mtaalamu katika masuala ya sheria za kodi na amefundish

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 24.10.2017

Image
                                                  Post Views: 77

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image
   

MAGAZETI YA UDAKU LEO

Image
    Post Views: 32

MHASIBU UBALOZI WA TANZANIA MSUMBIJI APANDISHWA KORTINI KISUTU

Image
Mhasibu Joyce Moshi akishuka ngazi za mahakama baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili. MHASIBU wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Joyce Moshi (56) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka tisa ikiwemo ya utakatishaji fedha wa dola za Marekani 150,000. Moshi ambaye ni Mkazi wa Temeke alifikishwa mahakamani hapo leo na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Wakili wa Serikali, Saimon Wankyo alidai kuwa Oktoba 25, 2016 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Maputo nchini Msumbiji, alighushi barua ikionesha kwamba Ubalozi wa Tanzania Nchini Msumbiji Umeielekeza Benki ya MIllenium kupeleka Dola za kimarekani elfu kumi  katika akaunti inayomilikiwa na Joyce Moshi akijua yakuwa siyo kweli. Inadaiwa barua hiyo ilionyesha kuwa ubalozi umeelekeza Benki ya ya Millennium BIM ya Maputo, kuhamisha dola za Marekani 10,000 kutoka akaunti namba 79667362 kwenda akaunti namba 182283177 inayomilikiwa na

ZARI THE BOSS LADY , BWANA’AKE WAWAFUNGA MIDOMO WABONGO!

Image
              Mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ambaye pia ni mzazi mwenza wa Mbongo Fleva, ambao hivi karibuni ilisemekana wamemwagana kutokana na mgogoro mzito uliosababishwa na Mbongo Fleva huyo kuchepuka na kuzaa na mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto, hatimaye leo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wamewaziba watu midomo, baada ya kutupia video wakiwa pamoja kisiwani Zanzibar. Video hiyo iliwapa joto mashabiki na wakajikuta wamepigwa na butwaa, kwani stori zilishaenea kuwa wawili hao wameshapigana kibuti na imebaki stori, lakini baada ya wawili hao kutupia video hiyo ikajibu maswali yote kuwa wapo pamoja tena kwenye dimbwi zito la mahaba. N

Dida: Sijawahi Kuhongwa Chochote Na Mwanaume

Image
Khadija Shaibu ‘Dida’. MTANGAZAJI wa redio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefunguka kuwa katika maisha yake hajawahi kuhongwa chochote na mwanaume, mafanikio yake utafutaji kwa sababu hapendi kupewa wala kujibweteka anapambana na ataendelea kupambana kwani anaamini mwanaume hawezi kumfanya awe na maendeleo. na kujikuta hawana thamani tena, jamani pambaneni mbona inawezekana wanawake kufanikiwa bila kuwatumia wanaume na miili yetu!” alisema Dida.

Nape Apigilia Msumari Kauli ya Msekwa Kuhusu Ukomo wa Madaraka kwa Rais

Image
Nape Nnauye. MBUNGE wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amepigilia msumari kauli iliyotolewa na Spika wa zamani wa Bunge, Pius Msekwa kuhusu miaka ya uongozi na kusema misimamo hiyo ndiyo misimamo ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwalimu Julius Nyerere. Nape Nnauye ameweka video ya Pius Msekwa akielezea juu ya ukomo wa kiongozi madarakani na kusema chama hicho kilishafikiria miaka ya nyuma kuongeza miaka kutoka 10 na kuendelea lakini waliona miaka kumi inatosha kwa mtu kuongoza na kusisitiza ikiwa miaka 15 ikatokea mkapata kiongozi mbaya miaka hiyo itakuwa ni mingi sana. “Miaka 15 mkipata kiongozi mbaya ni mingi sana, nashauri ibaki miaka 10 kama kiongozi ni mbaya angalau tumvumilie kwa miaka 10 tu halafu basi ndivyo hoja ya miaka 10 ilivyopita si kama hiyo mingine hatukufikiri ilifikiriwa ndiyo maana naposikia kuna Mbunge mmoja anataka kupendekeza twende kwenye miaka saba kwa vipindi viwili ninataka kumjulisha kwamba hili si wazo jipya tulishafikiri na lilik

Miili ya Wanajeshi wa JWTZ Waliouawa DRC Yaagwa

Image
Miili ya askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imeagwa tayari kwa kurejeshwa nchini. Askari hao walikuwa kwenye operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa (UN). Habari zilizopatikana zilisema miili ya askari hao iliagwa jana. JWTZ katika taarifa kwa umma juzi iliwataja askari hao kuwa ni Koplo Maselino Paschal Fubusi na Praiveti Venance Moses Chimboni. Taarifa ilisema askari wengine 12 walijeruhiwa katika shambulio lililofanywa na kundi la wapiganaji la ADF. Taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya JWTZ ilisema askari hao walishambuliwa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi Oktoba 9, wakiwa umbali wa kilomita 24 mashariki mwa mji wa Beni. JWTZ ilisema UN inaandaa utaratibu wa kuirejesha miili ya askari hao na utakapokamilisha wataujulisha umma mapokezi, kuaga na mazishi yatakavyokuwa. Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amelaani mauaji hayo ya

Hatari ya kuvalia viatu bila soksi

Image
               Ukivalia viatu vyako bila soksi unajiweka katika hatari ya makubwa zaidi kuliko kunuka kwa miguu pekee.Chuo cha tiba ya miguu nchini Uingereza kinasema karibuni kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya maradhi yanayosababishwa na kuvu kutokana na kuvuma kwa mtindo wa kuvalia viatu bila soksi, hasa miongoni mwa vijana.Mtaalamu Emma Stephenson anasema amekuwa akipokea wanaume wa kati ya miaka 18-25 walio na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovalia soksi au kuvalia viatu visivyowatosha vyema.Kutovalia soksi siku hivi kumekuwa mtindo maarufu wa mavazi, na mwanamuziki Sam Smith ni miongoni mwa watu wanaojitokeza hadharani wakiwa na viatu bila soksi.                   Wanaume wengi katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila soksi.Mwanamuziki Tinie Tempah amejishindia tuzo nyingi kwa sababu ya mitindo na mara nyingi katika maonesho ya mitindo ya Londo huketi viti vya mbele.Yeye pia huwa mara nyingi hav