Mawaziri na Manaibu Waziri wakiapa, Ikulu Dar. MAWAZIRI na manaibu walioapishwa na Rais John Magufuli, wametoa ahadi ya jinsi watakavyotekeleza majukumu yao. Mawaziri na manaibu walioapishwa leo Jumatatu wametoa ahadi muda mfupi baada ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. Waziri Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika amesema atahakikisha watumishi wanakuwepo ofisini kuwahudumia wananchi. Amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenda kunywa chai, hivyo atahakikisha wanabaki ofisini kutoa huduma. Kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, Mkuchika amesema, “Nitatoa elimu na nitatumia muda wangu mwingi na ndugu zangu wa Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa). Nitaongea na Waziri wa Elimu somo la rushwa lifundishwe kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.” “Ni wizara yenye changamoto nyingi, ng’ombe wanapigwa mnada, hawana maeneo ya malisho, viwanda vya mifugo na mchango wa maziwa ni tatizo, niko katika tafakari, nin