Nyumba ya Professor Jay Yabomolewa, Afunguka Mazito
Kushoto ni muonekano wa nyumba ya Professor Jay baada ya kubomolewa. Mbunge wa Mikumi Mjini, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amekumbwa na zoezi la bomoa bomoa linaloendelea maeneo ya Kimara, jijini Dar es salaam kwa kuvunjiwa nyumba yake huku akieleza kuwa uvunjaji huo haukufuata sheria. Professor Jay akithibitisha taarifa hizo kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii amesema zoezi hilo limefanyika wakati yeye akiwa jimboni kwake na mbaya zaidi hakupewa taarifa na zoezi hilo limeendeshwa jioni ambapo sio muda wa kazi kiserikali. Mbunge wa Mikumi Mjini, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay. “Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu. Sijawahi kuumia kiasi hiki, nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyowe