Miili ya Ndugu 13 Waliofariki kwa Ajali Uganda Ilivyoagwa Dar (Pichaz)
SIMANZI, vivlio na majozni imetawala wakati wa kuaga miili ya Watanzania 13 ambao ni ndugu wa familia moja waliofariki kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea nchini Uganda hivi karibuni.
Miili ya wanafamilia hao imeagwa leo Septemba 20, 2017 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kuelekea Arusha, Kilimanjaro na Mpwapwa kwa ajili ya mazishi.
Katika ibada hiyo ya kuwaaga marehemu, viongozi mbalimbali wa serikali walikuwepo wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala), Angela Kairuki, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijage, Waziri Maalum wa Kusimamia Jiji la Kampala, Betty Kamya kutoka Uganda aliyemwakilisha Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni kukabidhi miili ya marehemu kwa ndugu zao.
Aidha, Rais Museven ametuma salamu maalum za rambirambi ambazo zilisomwa na Betty kwa niaba yake na kupokelewa na Waziri Kairuki kwa niaba ya Rais Magufuli.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu, Septemba 18, 2017 katika eneo la biashara Lubanda takribani kilomita 80 kufika Kituo cha Polisi cha Fika Salama karibu na Mto Katonga Wilaya ya Mpigi, Kampala, Uganda.
Ajali hiyo mbaya ilihusisha gari aina
ya fuso yenye namba za usajili UAH 970P na coaster yenye namba T540 DLC
waliokuwa wakitumia Watanzania hao waliokuwa wakitoka kwenye harusi ya
binti wa Dkt. Annette Ibingira ambaye ni mke wa mhazini wa shule ya Wazazi ya Kampala nchini Uganda Dkt. Ibingira.
Aidha Majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Nkozi na Double Cure Clinic zilizopo nchini Uganda.
Tukio hilo lilimgusa pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyetumia salamu za rambirambi aliyewahi kuwa Naibu Waziri na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Gregory Teu kufuatia vifo vya watu hao ambao ni ndugu wa familia yake.
Comments
Post a Comment