Posts

BREAKING: Polisi watoa taarifa Kuhusu tukio la mlipuko ofisi za mawakili

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 28/08/2017                TUKIO LA MLIPUKO KWENYE OFISI ZA MAWAKILI WA IMMA Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 26/8/2017 lilitoa taarifa ya awali ya tukio la mlipuko uliotokea katika ofisi za mawakili wa IMMA zilizopo katika eneo la Upanga jijini Dar Es Salaam. Hivyo Jeshi la Polisi linapenda kuufahamisha umma kuwa  uchunguzi wa awali uliofanyika umebaini kwamba usiku wa kuamkia tarehe 26/8/2017 majira kati ya saa 7:00-8:00 watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi kamili, walifika katika ofisi za mawakili wa kampuni ya IMMA (IMMA ADVOCATES) wakiwa na magari mawili wakijifanya ni askari na kuwarubuni kisha kuwachukua walinzi wa jengo hilo na kuondoka nao kwenye moja ya gari walilokwenda nalo,ambapo baadaye walinzi hao walikutwa maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui. Aidha, kundi lililobaki liliingia ndani ya Ofisi hizo na kuweka milipuko iliyotengenezwa kienyeji ambayo baada ya watu hao kuondoka ililipuka na kusaba

RAS-Dodoma- Wakumbukeni Idara za Elimu katika PlanRep Mpya.

Image
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dododma  Rehema Madenge akifungua mafunzo ya siku nane kwa wataalamu wa Afya, Mipango na Fedha kutoka Mikoa Mitano chini ya ufadhili wa mradi wa Uimarishaji Mifumo (PS3) Serikali mkoani hapa imesema ili mpango wa PlanRep uweze kufanikiwa kwa ufasaha hakuna budi kuzijumuisha idara za Elimu katika mafunzo yanayoendelea mkoani Dodoma yanayo wajumuisha wataalam wa mipango pamoja na afya kutoka mikoa mitano ya Tanga, Tabora, Manyara, Singida na wenyeji Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya bajeti kwakutumia mfumo mpya wa PlanRep na FFARS. Akifungua mafunzo ya siku nane mkoani hapa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge, amesema moja ya vitu vilivyokuwa vikikwamisha masuala ya bajeti ni pamoja na kutokuwa na takwimu sahihi huku akinyooshea kidole takwimu za idara za elimu. “Ninatamani sana takwimu za elimu ziwe sahihi hasa katika uwasilishaji wa taarifa za mitihani ili ziweze kuendana na idadi ya wanafunzi na fedha zinazo o

JAJI MKUU, POLISI WATOA ONYO MGOMO WA MAWAIKILI NCHI NZIMA

Image
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma. Kaimu  Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini, wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi, vinavyochunguza tukio la mlipuko, uliotokea kwenye ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam. Profesa Juma jana  alisema TLS hawana haki ya kutoa agizo kwa mawakili, kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza mengine, kwa kuwa kila wakili ana mkataba binafsi na mteja wake. Profesa Juma alisema uhuru wa mahakama ni pamoja na kuheshimu mamlaka nyingine za nchi zinapokuwa zinafanya kazi zake.  Alisema kwa kuwa tukio la kulipuliwa kwa ofisi za Mawakili wa Immma ni tukio la kihalifu, hivyo wanasheria waiache Polisi na vyombo vingine vya upelelezi kufanya kazi yao. “Kama kutatokea wateja watakaolalamika kuwa mawakili wao hawakufika mahakamani siku ya Jumanne na Jumatano, hatua

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA TAKUKURU

Image
Rais Maguduli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola (Picha na Maktaba). Ulinzi umeimarishwa katika ofisi za makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) zilizoko Upanga, jijini Dar es Salaam huku ikielezwa kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatembelea ofisi hiyo. Saa 3:17  asubuhi yaleo  Agosti 28 , msafara wenye magari yapatayo 10 uliingia katika ofisi hiyo. Katika kuimarisha ulinzi, barabara zinazoingia kwenye ofisi hiyo nazo zimefungwa. Taarifa zaidi kuhusu alichokizungumza Rais alipotembelea TAKUKURU tutakujuza baadaye. Endelea kufuatilia habari zetu.

CHRISTINA SHUSHO AANDIKA UJUMBEE HUU KUHUSU WIMBO WA ALIKIBA SEDUCE ME

Image
Ni siku mbili sasa zimepita tangu mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ ambao umekuwa ukizungumziwa na watu mbalimbali wasanii na wasiokuwa wasanii na wanasiasa pia. Mmoja wa wasanii waliouzungumzia wimbo huo ni pamoja na Mwimbaji wa nyimbo za Injili Christina Shusho ambaye anafahamika zaidi kutokana na nyimbo zake za kumsifu Mungu lakini kupitia Instagram yake aliandika huu ujumbe kwa Alikiba. ”Leo unaeza kuta mtu kaitwa kanisani aongoze wimbo wa sifa halafu akalianzisha seduce me….eeh jamani Kiba we noma. – Wimbo ni mzuri sana Professionally in boss ruge ‘s voice. – Hauna picha za aibu , naeza watch na familia, though sijui maana ya SEDUCE ME. #team Kigoma #wamanyema oyeeeee LAST @OFFICIALALIKIBA BASI SIKU NYINGINE TUTEMBELEE KANISANI. UKIWA MFALME HUCHAGUI DINI WOTE WAKO.”

RC Makonda aamua kufunguka kuhusu Diamond na Alikiba

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Dar ss Salaam Paul Makonda ameamua kuandika maoni yake kutokana na kile anachokiona kuhusu wasanii wa Bongofleva wanaoshindanishwa kimuziki ambao ni Alikiba na Diamond. RC Makonda ameaandika maneno 17 kwenye Instagram ambayo yanawahusu mastaa hao wanaotajwa kuwa wana ushindindani kimuziki akionesha kufuraishwa na kazi za mastaa hao lakini akiwaonya tofauti zao kutovuka mipaka na kuvunja sheria au tamaduni za kitanzania. “Tofauti zenu mimi nazipenda, kwani zinaleta ushindani mzuri kwenye mziki. Ila naomba mzingatie sheria na Utamaduni wetu..” – RC Makonda

Kocha Mayanga atangaza kikosi cha Taifa Stars

Image
 Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Botswana utakao pigwa Septemba 2 mwaka huu. Wachezaji hao wa Taifa Stars wanatarajia kuingia kambini Agosti 27 siku ya Jumapili saa mbili usiku nakuanza mazoezi tarehe 28 ya mwezi huu tayari kwa maandalizi ya mchezo. Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga amesema “Tunategemea kuanza kambi siku ya keshotarehe 27 saa mbili usiku hapa hapa Dar es salaam na tunategemea kuwa na vijana 21 kambini ambao watafanya mazoezi sikua ya Jumatatu jioni na kumaliza mazoezi tarehe 1 na siku inayofuata ndiyo mchezo wetu na Botswana katika uwanja wa Uhuru”, amesema Mayanga. Kwa upande wake Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Alfred Lucas amesema “Kutakuwa na mabadiliko ya ratiba ya ligi  kwa sababu tulitarajia zaidi kwamba tarehe za FIFA zisianze tarehe 28 tulitegemea zingeanza baadaye lak

JOYCE KIRIA AWAPA SOMO WAKAA UCHI MITANDAONI

Image
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria . KUTOKANA na matukio ya baadhi ya wanawake kujianika uchi mitandaoni kushika kasi, Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live,  Joyce Kiria  ameibuka na kuwapa somo kwamba, waachane na kujiuza, kisa njaa na kama wanapenda umodo, basi wafuate kanuni na taratibu za kimaadili na si kutumia njia hiyo. Staa wa Bongo, Gigy Money. Akizungumza na  Risasi Jumamosi , Joyce alisema kuwa, anashangazwa na wanawake wanaojianika uchi mitandaoni hivyo kuwataka waache kwani baadaye watajutia baada ya kupata madhara makubwa.           Amber Lulu “Mimi mwenyewe maisha ya kutegemea wanaume kwa kutafuta fedha nimeyaishi na yalinitesa sana maana unajikuta unajichosha na kujiingiza kwenye mambo ya hatari,” alisema Joyce. Joyce alimalizia kwa kusema kuwa, mwisho aliamua kutumia akili na hadi sasa ni mjasiriamali na fedha anayoipata anaifurahia kwani anaamini ni jasho lake.

WEMA ZARI, WAUNGANA KUMBUTUA MOBETO

Image
Mwanamitindo wa kitaifa na kimataifa, Hamisa Hassan Mobeto. MAMBO yanazidi kuwa mambo! Lile saga la mwanamitindo wa kitaifa na kimataifa, Hamisa Hassan Mobeto,kudaiwa kuzaa na msanii wa bongo Fleva linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha, nyumayake kukiwa na sarakasi nyingi ambazo siyo za nchi hii. Ubuyu mpya mjini unadai kwamba, staa mwenye jina kubwa Bongo, Wema Isaac Sepetu amejitosa kwenye sakata hilo akidaiwa kuungana na mpenzi wa sasa wa Wema, Zari… msanii huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa ajili ya kumbutua Hamisa kwa kuwa jamaa huyo pia aliwahi kuwa mpenzi wa Wema (x boyfriend wake). Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Wema, baada ya Hamisa kutikisa kwa ishu hiyo na kuungwa mkono na Wabongo wengi huku Zari akibaki peke yake, Wema na timu yake (Team Wema), wanadaiwa kuungana na Zari kwa ajili ya kumsaidia kujibu mashambulizi mitandaoni. “Yaani kila kukicha mambo yanazidi kupamba moto kwenye mitan

BOB JUNIOR NAYE AJITOSA SAKATA LA DIAMOND NA KIBA,ASEMA SIMBA KAONA HAKUNA NYAMA MBUGANI

Image
Mwimbaji wa kitambo ambaye pia ni producer wa Sharobaro Records aliyehusika katika kutengeneza nyimbo kadhaa za Bongofleva Bob Junior amefunguka kupitia Instagram yake na kuweka ujumbe ambao anadai kupotezewa na Diamond Platnumz. Kupitia Instagram yake Bob Junior kaandika SIMBA NILIE MZOEA SIKU ZOTE NI SIMBA RAFIKI NI SIMBA NDUGU NI SIMBA KIPENZI LEO KAONA HAKUNA NYAMA MBUGANI KAAMUA KUNILA HADI MIE KWELI SIMBA HANA URAFIKI NA WAANADAMU MYAMA ATABAKI KUWA MYAMA NA BINAADAMU MYONGE ATABAKI KUWA MYONGE ACHA NIWE MYONGE ILA MUNGU NDIO MFALME NA YEYE NDIO ANAE TETEA WALE WANYONGE KAMA MIMI BABA MUNGU ULIE JUU HUKUMU UTAITOA WEWE.” – Bob Junior

Zitto Kabwe afunguka tena

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, ameweka wazi kuwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi hususan chakula yanazidi kushuka tofauti na tunavyonunua katika kipindi hiki ambacho nchi inapambana kuingia kwenye uchumi wa viwanda. Kwenye ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe ameandika tathmini ya hali ya uchumi kwenye mauzo, na kusema kuwa anguko kubwa la mauzo tofauti na tunavyonunua, linatufanya kuzidi kuwa tegemezi. “Uagizaji wa bidhaa za chakula kutoka nje umeongezeka kwa 14% ndani ya mwaka mmoja wa Mei 2016 mpaka Mei 2017, ambapo Tanzania ilitumia dola 480 milioni kuagiza vyakula kama sukari, nafaka na mafuta ya mawese. Tumekuwa tegemezi zaidi, tunauza bidhaa kidogo zaidi nje ya nchi, na tunanunua bidhaa zaidi kutoka nje", aliandika Zitto Kabwe. Mbunge Zitto Kabwe aliendelea kuandika kuwa pesa ambayo serikali inapoteza kwa anguko la mauzo ya bidhaa ndani ya miaka miwili ni nyingi, ambayo ingeweza hata kununua ndege 23 za aina ya bomberd

Floyd Maywether amtwanga McGregor kwa TKO

Image
 Baada ya tambo za bondia Conor McGregor kuelekea pambano dhidi ya Floyd Maywether ambaye hajawahi kupoteza pambano, asubuhi ya August 27 katika ukumbi wa  T-Mobile Arena mjini Nevada, USA majibu yalipatikana. Mayweather alikuwa anaingia kucheza pambano lake la 50 dhidi ya McGregor ambaye yeye lilikuwa ni pambano lake la 25 akiwa ndio kapoteza kwa mara ya pili na kashinda mara ya 23, ushindi wa leo wa Mayweather unakuja baada ya kumpiga bondi wa Philipino Manny Pacquiao May 3 2015 kwa point mjini Las Vegas. Bondia Floyd Mayweather leo ameshinda pambano lake la 50 akiwa kacheza mapambano 50 bila kupoteza, amefanikiwa kuendelea kutetea rekodi yake kwa kumpiga Conor McGregor kwa Technical Knock Out (TKO) katika round ya 10 pambano la round 12.

DADA YAKE DIAMOND PLATINUMS AFUNGUKA HALI ALIYOKUWA NAYO MAMA YAKE DIAMOND BAADA YA PICHA YA OOY DIMPOZ

Image
Instagram ilichafuka juzi kati baada ya Mwimbaji Ommy Dimpoz kupost picha akiwa na Mama mzazi wa Diamond Platnumz ikiwa ni moja ya njia alizotumia kujibu mashambulizi ya diss ya wimbo wa Diamond Platnumz.Kwenye hii video kuna mahojiano na Dada wa Diamond Platnumz Esma Platnumz na Mume wake Petitman ambapo moja ya maswali aliyoulizwa Esma ni kuhusu hali ya Mama Diamond baada ya Dimpoz kupost ile picha. Esma alicomment kwenye hiyo picha ya Ommy Dimpoz na kumtaka mwimbaji huyo kutomuhusisha mama yake na ‘maugomvi yao’ ambapo baada ya kuhojiwa leo na AyoTV, Esma amesema Mama yake alikua kimya tu na hakuongea chochote kuhusu ile picha… unaweza kutazama kwenye hii video hapa chini

Waziri Lukuvi: "Bomoabomoa hainihusu"

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefunguka na kusema zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Kimara na Kibamba yeye halimuhusu hivyo awataka watu wamuulize Waziri wa ujenzi, uchukuzi Waziri Lukuvi alisema zoezi linaloendelea Kimara na Kibamba ni sheria ya barabara ndiyo inayofanya ile kazi na siyo yeye na kuwataka watu wamtafute Waziri husika ili aweze kuwapa maelezo juu ya jambo hilo. "Hapana siwezi kuzungumzia hilo nenda kamuone Waziri wa Ujenzi kwani Sheria ya barabara ndiyo inayofanya ile kazi siyo mimi hivyo siwezi kuzungumza lolote kwenye hilo jambo kwani mimi bomoabomoa hiyo hainihusu, kwani kila mtu anaapa kwa kipande chake na mimi siyo Waziri wa jumla, Waziri wa jumla ni Waziri Mkuu" alisema Lukuvi  Aidha Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani vikali zoezi la bomoabomoa linaloendelea katika maene

Taarifa muhimu kwa wote walioomba na watakaoomba kazi Serikalini

Image
Mtakumbuka Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika 2016/2017 iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya 52,000 kwa Watanzania, ambapo katika siku za hivi karibuni Serikali imekuwa ikitoa vibali vya kuajiriwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo Waalimu wa Sayansi, Kada za Afya na maeneo mengine kulingana na mahitaji. Kama mnavyofahamu mojawapo ya jukumu la msingi la kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni pamoja na kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi wanaofaulu usaili, ambapo tangu Serikali ilipoanza kutoa vibali baada ya kusitishwa tumeshapokea jumla ya vibali kwa ajili ya mamlaka za Ajira 239, kati ya hivyo vipo ambavyo vimeshafanyiwa kazi na vingine mchakato wake unaendelea katika hatua mbalimbali. Aidha, baadhi ya vibali ambavyo mchakato wake umeshakamilika ni pamoja na  kibali cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo tulipokea jumla ya  maombi ya kazi 6,8

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 25.08.2017

Image