PICHA MATUKIO YANAYOJIRI TAMASHA LA SIMBA Y UWANJA WA TAIFA
Mashabiki wa Simba waliojitokeza kwenye Tamasha la Simba Day linalofanyika Kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salam .. Klabu ya Simba yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam ina utaratibu wake wa kuenzi vitu vyake vya klabu kwa kuanzisha siku maalumu ambayo wanasimba wote hukusanyika pamoja kujadiliana mambo mbalimbali.Agosti 8 ya kila mwaka huwa ndiyo siku hiyo iliyopewa jina la āSimba Dayā, wameichagua wao Wanasimba kama sehemu ya kumbukumbu ambapo huchagizwa na mambo mengi ikiwemo kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka, kubadilishana mawazo, na mwisho huchezwa mechi ambayo ndiyo huitimisha kila kitu.