Posts

WEMA: NISIPOPATA MTOTO NAFUNGA KIZAZI

Image
Wema Abraham Isac Sepetu. Exclusive! Hapo nyuma kumepita matukio mengi yaliyomhusu staa mwenye jina lake kwenye tasnia ya sinema za Kibongo, Wema Abraham Isac Sepetu , lakini mwenyewe hakuwa tayari kufungua kinywa kutoa ufafanuzi na hisia zake. Ni kupitia Ijumaa Wikienda ambalo limethubutu kufanya naye mahojiano maalum ambayo ndani yake alifunguka mambo mazito kuhusu maisha yake ya sasa na kuelezea dhamira yake ya kutaka kufunga kizazi endapo safari hii hatajaliwa kupata mtoto baada ya kupata mpenzi mpya. NYUMBANI UNUNIO Katika mahojiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Wema, Ununio jijini Dar, staa huyo ambaye ni Miss Tanzania 2006/07, aliweka wazi mambo ambayo watu wamekuwa wakiyasema bila mpangilio wala kusikia kauli yake. UNGANA NA WEMA Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Wema? Ni muda mrefu sana mashabiki wako hawajakusikia. Je, ni kwa nini umeamua kuwa kimya kiasi hicho? Wema: Sasa hivi nimebadilisha ratiba nzima ya maisha yangu. Kuna vitu ambavyo

Mwana FA: Kuoa mapema kuna faida kubwa

Image
Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hip, Mwana FA amedai amegundua kuoa mapema kuna faida nyingi ambapo amedai humfanya mtu atulie na kuanza kufocus katika maisha mapema. Rapa huyo ambaye aliingia kwenye maisha ya ndoa mwaka mmoja uliopita, amesema ni kweli msanii akioa anatakiwa kubadiika kutoka katika mfumo wa maisha yake ya kawaida ili kuendana na mfumo mpya wa maisha ndani ya ndoa.

Mbunge Aliyeondolewa CUF Azuiwa Kuingia Kwenye Kikao cha Madiwani

Image
Salma Mwasa . Mbunge wa Viti Maalumu ( CUF ) aliyevuliwa ubunge hivi karibuni Salma Mwasa amesikitishwa na kitendo cha askari wa Manispaa ya Ubungo cha kutaka kumzuia asikanyage kwenye halmashauri hiyo. Mwasa ni miongoni mwa wabunge kumi waliovuliwa uanachama sanjari na madiwani wawili wa CUF kwa madai ya kukihujumu chama hicho, hali iliyosababisha kukosa fursa za kuwa wabunge. Akisimulia tukio hilo lililotokea leo Jumatatu, Julai 31, Mwasa amesema aliitwa na askari hao na kuambiwa hatakiwi kuonekana katika eneo hilo la manispaa na kwamba, hiyo ni amri kutoka juu kwa wakubwa. “Mimi ninachojua amri zipo kumi tu, sasa hiyo 11 inatoka wapi? Lakini niliwaeleza kwamba mimi ni mkazi wa Ubungo sasa mnaponizuia nisije hapa hamnitendei haki kwa sababu nakuja kufanya mahitaji mbalimbali,” amesema.   “Mimi nimekuja kama mwananchi wa kawaida. Naomba umma utambue mimi bado ni mbunge hapa nilipo nina barua ya uteuzi na sina barua ya utenguzi,” anasema Mwasa. Hata hiv

MAJADILIANO SERIKALI NA BARRICK GOLD YAANZA RASMI

Image
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi (wa pili kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa na Rais. John  Magufuli kujadiliana na uongozi wa Barrick Gold Corporation akiwa na ujumbe wa kampuni hiyo kabla ya kuanza  mazungumzo hayo leo  jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU Majadiliano kati ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli na wawakilishi kutoka kampuni ya Barrick Gold Corporation kuhusu madini yanayochimbwa  na kampuni hiyo nchini yameanza leo, Julai 31 jijini Dar es Salaam. Prof. Kabudi akiwaelekeza jambo. Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa,  imesema kamati ya Tanzania inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na kamati kutoka Barrick inaongozwa na Ofisa Mwendeshaji Mkuu, Richard Williams. Prof. Kabudi akiwa na wageni hao. Profesa Kabudi amekaririwa katika taarifa hiyo akisema wamejipanga vizuri kujadiliana na Barrick juu ya

CHADEMA Yalia na Ugumu wa Maisha kwa Wananchi

Image
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Serikali imeshindwa kusimamia mfumuko wa bei ya chakula nchini kwa sababu haitambui umuhimu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA). Mbowe amesema mwakà 2015, NFRA ilihifadhi tani 446,000 za chakula lakini kufikia mwaka huu wakala huyo amehifadhi tani 74,826 za chakula. Mbowe amesema chakula kinapanda bei kwa sababu hakuna mkakati wowote wa Serikali kuwainua wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo. "Usalama wa taifa ni usalama wa chakula, kama hakuna usalama wa chakula hakuna usalama wa Taifa. "Mtakubaliana na mimi kuwa kwa miaka hii miwili vitu vimepanda bei lakini kipato cha wananchi hakijaongezeka "Bei ya mahindi kwa mwakà 2015 ilikuwa ndogo lakini mwaka huu imefika zaidi ya 90,000. Wananchi wanapata shida kwa sababu Serikali yao imewatupa wakulima." Amesema Mbowe

Safari ya Kichuya yanukia

Image
Siku chache baada ya kiungo wa Simba, Said Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio katika Klabu ya AFC, mshambuliaji wa timu hiyo, Shiza Kichuya anaweza akapata shavu la kucheza soka nchini Misri. Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema klabu moja ya Misri inamtaka Kichuya ili imsajili kwa ajili ya kuichezea timu yao na sasa wapo katika mazungumzo. Bado mazungumzo ya Simba na klabu hiyo yanaendelea na wakifikia muafaka muda wowote Kichuya ataondoka kwenda nchini humo. “Kuna timu ya Misri kupitia wakala aliyemuona Kichuya kwenye ligi na kufanya mawasiliano na sisi na tayari kuna barua wameleta wakimtaka Kichuya. “Kuna dau ambalo wamelipendekeza ili waweze kumsajili Kichuya lakini sisi hatujakubaliana nalo, hivyo tupo katika mazungumzo ya kuweza kufikia makubaliano lakini tunataka waongeze dau. “Hata hivyo, itabidi tumuachie Kichuya akacheze soka la kulipwa kwani kumzuia mchezaji kwa sasa ni sawa na bure, kwani amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na hatut

IGP SIRRO ALIPONGEZA JESHI LA POLISI MKOA WA SINGIDA

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipiga saluti wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua mapema leo kwenye viwanja vya kambi ya FFU mjini hapa. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua baadhi ya askari wa jeshi la polisi mjini Singida leo piga saluti wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada kukagua askari polisi waliokuwa kwenye paredi kwenye viwanja vya kambi ya FFU mjini hapa. …………………………. Picha/Habari na Gasper Andrew. Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amelipongeza jeshi la polisi Mkoani Singida kwa juhudi zake za kupunguza matukio ya uhalifu yakiwemo ya utekeji wa magari kwa kiwango kikumbwa.IGP Siro ametoa pongezi hizo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kweye viwanja vya kambi ya kikosi c

MAGAZETI YA LEO JULY 29,2017

Image

SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAFUTA GHAFI TOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI TANGA KUFANYIKA AGOSTI 5, 2017

Image
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani anawaalika wananchi katika halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 5, 2017 eneo la Chongoleani jijini Tanga ambapo utahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni. UDUGU WETU, FAHARI YETU - BOMBA LETU KWA MAENDELEO YA WATU WETU

Maazimio ya Baraza Kuu la CUF Lililokutana Leo Zanzibar

Image
Baraza kuu la Uongozi la Taifa la CUF ijumaa ya Julai, 28 limekutana kujadili mambo mbalimbali ambayo yanahusu chama hicho ikiwa ni pamoja na kujadili uamuzi wa CUF ya upande wa Prof. Lipumba kuwavua uanachama wabunge nane jambo lililofanya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwavua auanachama. UTANGULIZI: Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) leo hii Ijumaa, tarehe 28 Julai, 2017 limefanya kikao cha dharura kilichoitishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama ya mwaka 1992 (Toleo la 2014), kifungu cha 80 (1). Wajumbe 45 kati ya wajumbe 52 halali wa Baraza Kuu wamehudhuria ambao ni sawa na asilimia 86 ya wajumbe wote. Katika kikao hiki, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lilipokea, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu ajenda moja tu iliyowasilishwa kwake na Kamati ya Utendaji ya Taifa ambayo ilikuwa ni: • Taarifa kuhusu kile kinachoitwa kuwavua uanachama Wabunge wanane (8) na Madiwani wawili (2)