SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAFUTA GHAFI TOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI TANGA KUFANYIKA AGOSTI 5, 2017
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani anawaalika wananchi
katika halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta
ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania. Uzinduzi huo
unatarajiwa kufanyika Agosti 5, 2017 eneo la Chongoleani jijini Tanga
ambapo utahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri
Museveni. UDUGU WETU, FAHARI YETU - BOMBA LETU KWA MAENDELEO YA WATU
WETU
Comments
Post a Comment