Posts

Alichokisema John Mnyika baada ya Spika kubariki kufutwa uanachama Wabunge 8 wa CUF

Image
Mbunge wa Kibamba John Mnyika leo July 28, 2017 ameielezea hatua ya Spika Ndugai kubariki kufutiwa uanachama Wabunge wa Viti Maalumu wa CUF akisema ni makosa kwa kuwa kuna kesi Mahakamani kuhusu utata wa uongozi wa Chama hicho. Aidha, Mnyika amemuomba Spika kutangaza wateule ambao wametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi July 27, 2017 kuwa hawataapishwa mpaka mashauri yao yaliyopo Mahakamani yamalizike. Hatua ya John Mnyika imekuja siku chache baada ya Spika kuridhia kufutiwa uanachama Wabunge wanane wa CUF baada ya kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wake Prof. Lipumba kisha kutangaza nafasi zao kuwa wazi na kumuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya taratibu zilizostahili ambapo alitangaza majina ya Wabunge wengine wanane kuziba nafasi zao.

NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA UBUNGO

Image
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakisoma muongozo. Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo anapenda kuwatangazia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa Kama ifuatavyo:- Msaidizi wa Hesabu Daraja la II X 3 SIFA: Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambulikajja Serikali au Cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na hizo zinazotambulika na NBAA. KAZI NAMAJUKUMU: i)Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu. ii) Kutunza kurnbukurnbu zahesabu. iii) Kupeleka barua/nyaraka za Uhasibu benki. iv) Kufanya Kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu NGAZI YA MSHAHARA – TGS.B -Shilingi 390,000/- MASHARTI YA JUMLA: • Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania, • Awe amehitimu na Kupata Cheti cha Taaluma cha kidato cha Nne (IV) NB. Results Slip hazikubaliki • A

Shaffih Dauda ajitoa kugombea TFF

Image
Shaffih Dauda. Mtangazaji wa Clouds Media Group, Shaffih Dauda ametangaza kujitoa rasmi katika kinyang’anyiro cha kuwania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatia tuhuma za rushwa zinazomkabili. Shaffih ambaye ni mmoja wa wachambuzi maarufu wa soka nchini ametangaza uamuzi huo mapema leo asubuhi Julai 28 wakati akizungumza kupitia kipind cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds Tv. Akieleza sababu za uamuzi huo, Shaffih amesema kuwa imekuwa ni kazi ngumu ya miaka mingi kuweza kulijenga jina lake hadi kufikia hapo alipo leo, hivyo hawezi kuacha tuhuma hizo za rushwa zinazomkabili sababu ya uchaguzi wa TFF ziendelee kumchafua. “Nimetumia muda mrefu kujenga brand yangu hakuna haja kuendelea kung’ang’ania. Suala la Rushwa ni kunichafua na mimi sitaki,” alisema Shaffih. Uamuzi huu umekuja ikiwa ni siku chache tu tangu alipokamatwa na kuhojiwa na TAKUKURU yeye na wenzake kwa tuhuma za kupanga kufanya vitendo vya rushwa jambo amb

Breaking News: Mfanyakazi wa Acacia Akamatwa Airport Dar Akiondoka Nchini

Image
Kampuni ya Acacia imesema kuwa mmoja wa wafanyakazi wake wa kimataifa anayefanya kazi na Pangea Minerals Limited amezuiwa kuondoka Tanzania leo Julai 28 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya asubuhi. Acacia wameeleza kuwa, mfanyakazi huyo ambaye hawakumtaja jina alikamatwa na hati yake ya kusafiria ilichukuliwa huku na yeye akishikiliwa kwa muda. Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya kampuni hiyo, Acacia wamedai kuwa baada ya kuingilia sakata hilo kisheria, mfanyakazi huyo aliachiwa na hati yake ya kusafiria ikarejeshwa. Aidha, wamesema tukio hilo limetokea kipindi ambacho kwa takribani siku mbili sasa wafanyakazi wake wamekuwa wakisumbuliwa na maafisa mbalimbali wa serikali. Kuhusu tuhuma hizo, serikali kupitia kuwa Msemaji Mkuu, Hassab Abas imesema kuwa inafuatilia tuhuma hizo na baada ya muda mfupi watatoa taarifa kamili. “Tunafuatilia ukweli wa madai ya Acacia kuwa mmoja wa maafisa wake amezuiwa kuondoka Tanza

Mke wa Mugabe amtaka mumewe kumtangaza mrithi

Image
Rais Mugabe na mkewe bi Grace Mugabe Rais wa Zimabwe ametakiwa na mkewe kumtaja ''mrithi'' wake ili kupunguza migawanyiko kuhusu mtu atakayemrithi. ''Rais hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno alke litakuwa la mwisho'',alisema bi Grace Mugabe. Bwana Mugabe ndio kiongozi mzee zaidi na chama chake cha ZANU PF kimemchagua kuwania urais kwa mara nyengine mwaka ujao. Lakini makundi pinzani yamekuwa yakiwania urais ili kuimarisha uwezo wao huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.

KESI YA AKINA RUGEMALIRA NA SINGASINGA YAAHIRISHWA

Image
James Rugemalira (mwenye mvi) na mwenzake  Harbinder  Singh Sethi wakifikishwa mahakani. MAHAKAMA  ya  Hakimu Mkazi Kisutu  leo imeahirisha kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya  IPTL, Harbinder  Singh Sethi  maarufu kama  ‘Singasinga’   na  mfanyabiashara  James Rugemalira wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara. Rugemalira na Harbinder Singh Sethi baada ya kutoka kortini. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 3 mwaka huu, mbele ya  Hakimu Mkazi Mkuu ,  Huruma Shaidi  baada ya wakili wa serikali, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Ester Bulaya Ambwaga Tena Wasira Kortini

Image
Ester Bulaya. Mahakama ya Rufani imetupilia mbali rufaa dhidi ya Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) . Hukumu ya rufaa hiyo imesomwa leo Julai 28 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Elizabeth Mkwizu. Wapiga kura hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walikata rufaa mahakamani hapo wakipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, iliyompa ushindi Bulaya katika kesi ya uchaguzi waliyoifungua wakipinga matokeo yaliyompa ushindi Bulaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 dhidi ya Steven Wasira (CCM) .   Wasira . Rufaa hiyo ilisikilizwa Mei 11 mwaka huu na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani. Akisoma hukumu hiyo Naibu Msajili Mkwizu amesema kuwa hoja za warufani hao hazina msingi kwani kasoro walizokuwa wakizilalamikia hazikuwa na athari katika matokeo ya uchaguzi huo.

Ruby Amuanika Baba Kijacho Wake

Image
BAADA ya kufanya vizuri na baadhi ya ngoma zake kama Na Yule , Sijutii, na nyingine nyingi, staa wa Bongo Fleva , Ruby , amemuanika baba kijacho wake kwenye ukurasa wake wa Instagram. . Huyu ndiye Jamali mpenzi wa Ruby Ruby ambaye ‘amejaza na akajazwa’ na sasa ni mama kijacho amemtundika ‘ handsome boy ’ wake huyo anayeitwa Jamal na kumuandikia ujumbe ufuatao. “ My prince charm, my smile maker, Baba princess Ruby ” NA ISRI MOHAMED/GPL

MANCHESTER UNITED WATANDIKWA NA FC BARCELONA,NEYMAR ATUPIA

Image
Neymar celebrates after his first-half goal gave Barcelona the lead against Manchester United at the FedExField Neymar capitalises on a poor first touch Antonio Valencia to bare down on the Manchester United goal United's Ecuadorian right back looks on despairingly as Neymar takes the ball away from him to score the opener Neymar passes the ball home into the United net after getting it out of his feet with Messi watching on  Manchester United's players look dejected in the background as Brazilian superstar Neymar wheels away to celebrate Barcelona starting XI (4-3-3): Cillessen; Semedo, Umtiti, Mascherano, Alba; Busquets, Rakitic, Alena; Messi, Suarez, Neymar. Goal: Neymar 32. Man United (4-2-3-1): De Gea (Romero 46); Valencia (Tuanzebe 88), Lindelof (Jones 46), Smalling (Bailly 46), Blind (Darmian 46); Carrick (Fellaini 46), Pogba; Rashford, Mkhitaryan (Pereira 62), Lingard (Martial 62); Lukaku Booked: Fellaini. Att: 80,162. Lindelof

Wanawake Watano Wauawa kwa Kuchomwa Moto

Image
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. WANAWAKE watano wameuawa kwa kuchomwa moto Kijiji cha Undomo, Uchama, Nzega mkoani Tabora kwa tuhuma za kuhusika na imani za kishirikina. Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ameziagiza kamati za ulinzi za mkoa na wilaya kusitisha mara moja kazi zote za sungusungu kwa madai kwamba sungusungu hao wanahusika na mauaji hayo na kuvitaka vyombo vya usalama kuhakikisha vinawakamata na kuwafikisha mbele ya sheria watu wote wanaohusika. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwataja waliouawa kuwa ni Ester Kaswahili, Njungu Maswari, Christina Said, Kabula Kagito. Kamanda Mutafungwa ameeleza kwamba wamewakamata viongozi wa eneo tukio hilo lilipotokea, akiwemo diwani, Ofisa mtendaji wa kata na Ofisa mtendaji wa kijiji kwa madai kwamba walikuwa wakifahamu kinachoendelea kwenye eneo lao lakini kwa makusudi, waliamua kutotoa taarifa kwa jeshi la polisi, j

BREAKING NEWS: Tundu Lissu Aachiwa kwa Dhamana

Image
  Tundu Lissu akiwasalimia wananchi waliofika mahakamani hapo. MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria nchini, Tundu Lissu mapema leo asubuhi. Lissu ametakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja ataweka bondi ya dhamana ya shilingi milioni 10 huku akiwekewa zuio la kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali maalum cha mahakama. Aidha kesi yake imepangwa kusikilizwa Agosti 24 mwaka huu baada ya wadhamini wake kukamilisha taratibu zote za kumdhamini. Tundu  Lissu ambaye alikamatwa Alhamisi, Julai 20 mwaka huu, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akijiandaa kuelekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki (EALS), alifikishwa Mahakamani hapo Jumatatu Julai 24 na kusomewa mashtaka  ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, kosa ambalo anadaiwa kulitenda Julai 17. Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa n

Serikali Yatoa Onyo kwa Wanaotumia Vibaya Mitandao ya Kijamii

Image
Serikali imesema inajipanga kukabiliana na matumizi mabaya ya mtandao ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wanaotumia vibaya. Akizungumza katika majadiliano ya usalama wa mitandao ya kijamii kati ya Tanzania na China, Naibu Waziri wa Wizara wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Edwin Ngonyani amesema serikali itawachukulia hatua kali wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii wakiwamo wanaotuma ujumbe wenye dhamira ya kuwachafua wengine. Kwani Tanzania bado inakabiliwa na changamoto ya udhibiti wa usalama wa matumizi ya mitandao ya kijamii. “Tanzania bado iko nyuma katika masuala ya kudhibiti usalama wa matumizi ya mitandao kama vile Twitter, Facebook, Instagram na YouTube, wenzetu China wamefanikiwa kudhibiti suala hilo,” amesema Injinia Ngonyani. Naibu Waziri wa Udhibiti wa mtandao wa China, Ren Xianliang alisema nchi yao imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kudhibiti matumizi ya usalama wa mtandao kwa kuwa walianz

BREAKING NEWS:MAKONTENA 10 YA KEMIKALI BASHIRIFU YAKAMATWA BANDARINI

Image
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imekamata makontena 10 yenye lita 200,000 za kemikali bashrifu katika Bandari ya Dar es Salaam yenye ambayo yameingizwa kutoka nchini Swaziland kinyume cha sheria.

Madiwani 3 wa CHADEMA Wajiuzulu LEO na Kujiunga CCM

Image
Wakati Wimbi la Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kujiunga na Chama cha Mpinduzi (CCM) likiwa limepamba moto mkoani Arusha, majirani zao wa Kilimanjaro nao wameanza kutimka kwa kile wanachodai kuwa ni kuweza kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli. Mapema leo mchana Julai 26, 2017, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewapokea madiwani watatu kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambao wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga CCM. Madiwani waliojiuzulu ni, Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Goodluck Kimaro, Diwani wa Kata ya Weruweru, na  Diwani wa Kata ya Mnadani, Everist Peter Kimati. Akizungumza wakati wa kutangaza azma hiyo, Goodluck Kimaro alisema kwamba CHADEMA hakuna demokrasia kama ambavyo chama hicho kimekuwa kikijinasibu.  Akitolea mfano Halimashauri ya Wilaya ya Hai ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ni Mbunge wa jimbo hilo, alisema chama hakina uwezo wa

VILIO, SIMANZI VYATAWALA KUAGWA KWA MTOTO NORAH

Image
Jeneza lenye mwili wa marehemu. NI huzuni na simanzi kubwa kwa ndugu jamaa na marafiki iliyoambatana na vilio wakati wa shughuli yaa kuaga mwili wa mtoto Norah Jimmy (11) aliyefariki dunia juzi kwa kile kinachodaiwa kuwa alibakwa kisha kunyongwa. Wanafunzi wenzake wakiwa katika majonzi. Wanafunzi waliokuwa wakisoma na Norah wameingiwa na simanzi kubwa na kushindwa kujizuia na kuangua vilio baada ya kuona jeneza lenye mwili wa mwenzao alitetangulia mbele za haki. …Wakiangua vilio. Norah aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Atlas iliyopo Sinza, ameagwa leo nyumbani kwao maeneo ya Sinza Mori jijini Dar na anatarajiwa kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni. Gari lenye mwili wa marehemu likiwasili nyumbani kwao. Inadaiwa mtoto huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili cha kubakwa kisha kunyongwa mpaka kufa na mjomba wake aitwaye John Msigala. Mwili wa marehemu ukipelekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa. Mpaka sasa bado

UJIO MPYA WA MPOTO NA CASSIM MGANGA HAUTAMUACHA MTU SALAMA!

Image
Mrisho Mpoto ‘Mjomba. Baada ya kufanya vizuri na kibao chake cha Sizonje, mwanamuziki wa miondoko ya Asili, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ ambaye aliamua kufuata nyayo za kobe na kukaa kimya kwa muda, hatimaye anatarajia kuibuka na wimbo wake mpya unaoitwa Kitendawili. Wimbo huo aliomshirikisha msanii wa Bongo Fleva, Cassim Mganga, utaachiwa rasmi Agosti 1, mwaka huu ambapo staili ya kuimba ya Mpoto iliyozoeleka imebadilika kabisa, ni moja kati ya nyimbo ambazo zitaacha historia kwenye muziki wake. Cassim Mganga “Kitendawili ni wimbo ambao ni kitendawili kama jina lake, audio nitaiachia Agosti 1, mwaka huu, kiukweli sijawahi kuhisi kama ninaweza kufanya muziki wa tofauti na ukawa na ladha kama huu, mashabiki wangu mkae mkao wa kula msubiri kukitegua kitendawili siku hiyo,” amesema Mpoto na kuongeza: “Yawezekana ukanisikia kwenye singeli au ninachana au hata Taarab, ni staili gani nimekuja nayo hicho ndicho kitendawili chenyewe.” Na Isri Mohamed/GPL

Wizara ya Afya Yatangaza Nafasi 3,152 za Kazi

Image
Tangazo la nafasi za kazi 3,152 kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Linah Ajifungua Mtoto wa Kike

Image
Linah . Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kama Linah amejifungua mtoto wa kike salama katika hospitali ya Marie Stopes, Mwenge jijini Dar es Salaam. Linah amejifungua leo, Jumanne, Julai 25 ikiwa ni muda mfupi baada ya maneno ya mashabiki zake kusambaa kwamba ujauzito wake ni wa muda mrefu tofauti na ilivyo kawaida. Alipokuwa mjamzito. Mtu wa karibu na msanii huyo amesema kuwa mama na mtoto kiafya wanaendelea vizuri. Hata hivyo katika kipindi chote cha ujauzito wake, Linah amekuwa akimtaja mpenzi wake wa sasa anayejulikana kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye baba wa mtoto wake. Miaka kadhaa nyuma, Linah amewahi kuzungumzia kuhusu taarifa za kuharibika kwa ujauzito wake wa kwanza ambao ulikuwa wa mpenzi wake wa zamani.

Alibaba Yawatengea Sh. 22 Bilioni Wabunifu wa Tehama Afrika

Image
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kampuni za Alibaba Jack Ma Baada ya kukamilisha ziara yake nchini Kenya wiki iliyopita, bilionea Jack Ma ametangaza kuanzisha mfuko wa kuendeleza wajasiriamali wa Kiafrika. Ma ambaye ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kampuni za Alibaba, alitangaza kutoa Dola 10 milioni za Marekani (zaidi ya Sh22 bilioni ) kwa mwaka,  kwa ajili ya mfuko aliouanzisha ujulikanao kama African Young Entrepreneurs Fund. “Nataka kuzisaidia biashara za mtandaoni,” alisema Ma ambaye ni mshauri wa Shirika la Dunia la Maendeleo na Biashara (UNCTAD) kuhusu ujasiriamali na biashara ndogo kwa vijana. “Fedha zipo. Ni zangu, hivyo sina haja ya kuomba kibali cha yeyote kuzitumia,” alisisitiza akibainisha kwamba ataajiri watu wa kuzisimamia na mchakato huo uanze mwaka huu. ..akiendesha mkutano wake nchini Kenya. Kuongeza fursa Ma alisema atashirikiana na UNCTAD kuwapata vijana 200 wabunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambao wataenda nch