Wanawake Watano Wauawa kwa Kuchomwa Moto



Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.

WANAWAKE watano wameuawa kwa kuchomwa moto Kijiji cha Undomo, Uchama, Nzega mkoani Tabora kwa tuhuma za kuhusika na imani za kishirikina.

Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ameziagiza kamati za ulinzi za mkoa na wilaya kusitisha mara moja kazi zote za sungusungu kwa madai kwamba sungusungu hao wanahusika na mauaji hayo na kuvitaka vyombo vya usalama kuhakikisha vinawakamata na kuwafikisha mbele ya sheria watu wote wanaohusika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwataja waliouawa kuwa ni Ester Kaswahili, Njungu Maswari, Christina Said, Kabula Kagito.

Kamanda Mutafungwa ameeleza kwamba wamewakamata viongozi wa eneo tukio hilo lilipotokea, akiwemo diwani, Ofisa mtendaji wa kata na Ofisa mtendaji wa kijiji kwa madai kwamba walikuwa wakifahamu kinachoendelea kwenye eneo lao lakini kwa makusudi, waliamua kutotoa taarifa kwa jeshi la polisi, jambo lililosababisha wanawake hao wauawe kikatili.

Comments

Popular posts from this blog