UJIO MPYA WA MPOTO NA CASSIM MGANGA HAUTAMUACHA MTU SALAMA!

Mrisho Mpoto ‘Mjomba.

Baada ya kufanya vizuri na kibao chake cha Sizonje, mwanamuziki wa miondoko ya Asili, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ ambaye aliamua kufuata nyayo za kobe na kukaa kimya kwa muda, hatimaye anatarajia kuibuka na wimbo wake mpya unaoitwa Kitendawili.
Wimbo huo aliomshirikisha msanii wa Bongo Fleva, Cassim Mganga, utaachiwa rasmi Agosti 1, mwaka huu ambapo staili ya kuimba ya Mpoto iliyozoeleka imebadilika kabisa, ni moja kati ya nyimbo ambazo zitaacha historia kwenye muziki wake.
Cassim Mganga

“Kitendawili ni wimbo ambao ni kitendawili kama jina lake, audio nitaiachia Agosti 1, mwaka huu, kiukweli sijawahi kuhisi kama ninaweza kufanya muziki wa tofauti na ukawa na ladha kama huu, mashabiki wangu mkae mkao wa kula msubiri kukitegua kitendawili siku hiyo,” amesema Mpoto na kuongeza:
“Yawezekana ukanisikia kwenye singeli au ninachana au hata Taarab, ni staili gani nimekuja nayo hicho ndicho kitendawili chenyewe.”
Na Isri Mohamed/GPL

Comments

Popular posts from this blog