Serikali Yatoa Onyo kwa Wanaotumia Vibaya Mitandao ya Kijamii
Serikali
imesema inajipanga kukabiliana na matumizi mabaya ya mtandao ikiwa ni
pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wanaotumia vibaya.
Akizungumza
katika majadiliano ya usalama wa mitandao ya kijamii kati ya Tanzania
na China, Naibu Waziri wa Wizara wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Injinia Edwin Ngonyani amesema serikali itawachukulia hatua kali
wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii wakiwamo wanaotuma ujumbe wenye
dhamira ya kuwachafua wengine. Kwani Tanzania bado inakabiliwa na
changamoto ya udhibiti wa usalama wa matumizi ya mitandao ya kijamii.
“Tanzania
bado iko nyuma katika masuala ya kudhibiti usalama wa matumizi ya
mitandao kama vile Twitter, Facebook, Instagram na YouTube, wenzetu
China wamefanikiwa kudhibiti suala hilo,” amesema Injinia Ngonyani.
Naibu
Waziri wa Udhibiti wa mtandao wa China, Ren Xianliang alisema nchi yao
imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kudhibiti matumizi ya usalama wa
mtandao kwa kuwa walianzisha mtandao wao ambao umekua anasaidia
kufuatilia masuala ya nchi yao vikiwamo vivutio mbalimbali ambavyo
huwashawishi na kutoa hamasa kwa wananchi wengi kuweza kutumia mtandao
huo.
“Sisi
katika kudhibiti matumizi ya usalama wa mitandao ya kijamii katika nchi
yetu tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa Kutokana kuanzisha mtandao
maalumu ambapo tumekua tukifanya vipindi mbalimbali vya kuhamasisha na
kuwashawishi wananchi kutumia mtandao huo,” alisema Xianliang.
Comments
Post a Comment