Posts

Serikali Yatoa Onyo kwa Wanaotumia Vibaya Mitandao ya Kijamii

Image
Serikali imesema inajipanga kukabiliana na matumizi mabaya ya mtandao ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wanaotumia vibaya. Akizungumza katika majadiliano ya usalama wa mitandao ya kijamii kati ya Tanzania na China, Naibu Waziri wa Wizara wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Edwin Ngonyani amesema serikali itawachukulia hatua kali wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii wakiwamo wanaotuma ujumbe wenye dhamira ya kuwachafua wengine. Kwani Tanzania bado inakabiliwa na changamoto ya udhibiti wa usalama wa matumizi ya mitandao ya kijamii. “Tanzania bado iko nyuma katika masuala ya kudhibiti usalama wa matumizi ya mitandao kama vile Twitter, Facebook, Instagram na YouTube, wenzetu China wamefanikiwa kudhibiti suala hilo,” amesema Injinia Ngonyani. Naibu Waziri wa Udhibiti wa mtandao wa China, Ren Xianliang alisema nchi yao imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kudhibiti matumizi ya usalama wa mtandao kwa kuwa walianz

BREAKING NEWS:MAKONTENA 10 YA KEMIKALI BASHIRIFU YAKAMATWA BANDARINI

Image
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imekamata makontena 10 yenye lita 200,000 za kemikali bashrifu katika Bandari ya Dar es Salaam yenye ambayo yameingizwa kutoka nchini Swaziland kinyume cha sheria.

Madiwani 3 wa CHADEMA Wajiuzulu LEO na Kujiunga CCM

Image
Wakati Wimbi la Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kujiunga na Chama cha Mpinduzi (CCM) likiwa limepamba moto mkoani Arusha, majirani zao wa Kilimanjaro nao wameanza kutimka kwa kile wanachodai kuwa ni kuweza kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli. Mapema leo mchana Julai 26, 2017, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewapokea madiwani watatu kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambao wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga CCM. Madiwani waliojiuzulu ni, Diwani wa Kata ya Machame Magharibi, Goodluck Kimaro, Diwani wa Kata ya Weruweru, na  Diwani wa Kata ya Mnadani, Everist Peter Kimati. Akizungumza wakati wa kutangaza azma hiyo, Goodluck Kimaro alisema kwamba CHADEMA hakuna demokrasia kama ambavyo chama hicho kimekuwa kikijinasibu.  Akitolea mfano Halimashauri ya Wilaya ya Hai ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ni Mbunge wa jimbo hilo, alisema chama hakina uwezo wa

VILIO, SIMANZI VYATAWALA KUAGWA KWA MTOTO NORAH

Image
Jeneza lenye mwili wa marehemu. NI huzuni na simanzi kubwa kwa ndugu jamaa na marafiki iliyoambatana na vilio wakati wa shughuli yaa kuaga mwili wa mtoto Norah Jimmy (11) aliyefariki dunia juzi kwa kile kinachodaiwa kuwa alibakwa kisha kunyongwa. Wanafunzi wenzake wakiwa katika majonzi. Wanafunzi waliokuwa wakisoma na Norah wameingiwa na simanzi kubwa na kushindwa kujizuia na kuangua vilio baada ya kuona jeneza lenye mwili wa mwenzao alitetangulia mbele za haki. …Wakiangua vilio. Norah aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Atlas iliyopo Sinza, ameagwa leo nyumbani kwao maeneo ya Sinza Mori jijini Dar na anatarajiwa kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni. Gari lenye mwili wa marehemu likiwasili nyumbani kwao. Inadaiwa mtoto huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili cha kubakwa kisha kunyongwa mpaka kufa na mjomba wake aitwaye John Msigala. Mwili wa marehemu ukipelekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa. Mpaka sasa bado

UJIO MPYA WA MPOTO NA CASSIM MGANGA HAUTAMUACHA MTU SALAMA!

Image
Mrisho Mpoto ‘Mjomba. Baada ya kufanya vizuri na kibao chake cha Sizonje, mwanamuziki wa miondoko ya Asili, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ ambaye aliamua kufuata nyayo za kobe na kukaa kimya kwa muda, hatimaye anatarajia kuibuka na wimbo wake mpya unaoitwa Kitendawili. Wimbo huo aliomshirikisha msanii wa Bongo Fleva, Cassim Mganga, utaachiwa rasmi Agosti 1, mwaka huu ambapo staili ya kuimba ya Mpoto iliyozoeleka imebadilika kabisa, ni moja kati ya nyimbo ambazo zitaacha historia kwenye muziki wake. Cassim Mganga “Kitendawili ni wimbo ambao ni kitendawili kama jina lake, audio nitaiachia Agosti 1, mwaka huu, kiukweli sijawahi kuhisi kama ninaweza kufanya muziki wa tofauti na ukawa na ladha kama huu, mashabiki wangu mkae mkao wa kula msubiri kukitegua kitendawili siku hiyo,” amesema Mpoto na kuongeza: “Yawezekana ukanisikia kwenye singeli au ninachana au hata Taarab, ni staili gani nimekuja nayo hicho ndicho kitendawili chenyewe.” Na Isri Mohamed/GPL

Wizara ya Afya Yatangaza Nafasi 3,152 za Kazi

Image
Tangazo la nafasi za kazi 3,152 kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Linah Ajifungua Mtoto wa Kike

Image
Linah . Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kama Linah amejifungua mtoto wa kike salama katika hospitali ya Marie Stopes, Mwenge jijini Dar es Salaam. Linah amejifungua leo, Jumanne, Julai 25 ikiwa ni muda mfupi baada ya maneno ya mashabiki zake kusambaa kwamba ujauzito wake ni wa muda mrefu tofauti na ilivyo kawaida. Alipokuwa mjamzito. Mtu wa karibu na msanii huyo amesema kuwa mama na mtoto kiafya wanaendelea vizuri. Hata hivyo katika kipindi chote cha ujauzito wake, Linah amekuwa akimtaja mpenzi wake wa sasa anayejulikana kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye baba wa mtoto wake. Miaka kadhaa nyuma, Linah amewahi kuzungumzia kuhusu taarifa za kuharibika kwa ujauzito wake wa kwanza ambao ulikuwa wa mpenzi wake wa zamani.

Alibaba Yawatengea Sh. 22 Bilioni Wabunifu wa Tehama Afrika

Image
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kampuni za Alibaba Jack Ma Baada ya kukamilisha ziara yake nchini Kenya wiki iliyopita, bilionea Jack Ma ametangaza kuanzisha mfuko wa kuendeleza wajasiriamali wa Kiafrika. Ma ambaye ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kampuni za Alibaba, alitangaza kutoa Dola 10 milioni za Marekani (zaidi ya Sh22 bilioni ) kwa mwaka,  kwa ajili ya mfuko aliouanzisha ujulikanao kama African Young Entrepreneurs Fund. “Nataka kuzisaidia biashara za mtandaoni,” alisema Ma ambaye ni mshauri wa Shirika la Dunia la Maendeleo na Biashara (UNCTAD) kuhusu ujasiriamali na biashara ndogo kwa vijana. “Fedha zipo. Ni zangu, hivyo sina haja ya kuomba kibali cha yeyote kuzitumia,” alisisitiza akibainisha kwamba ataajiri watu wa kuzisimamia na mchakato huo uanze mwaka huu. ..akiendesha mkutano wake nchini Kenya. Kuongeza fursa Ma alisema atashirikiana na UNCTAD kuwapata vijana 200 wabunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambao wataenda nch

AMPIGA RISASI BABA MKWE WAKE KANISANI

Image
Chanzo cha mwandishi wa habari wa kujitegemea, Elias Mhegera kumpiga risasi baba mkwe wake kanisasni juzi ni hisia kuwa mzazi wa mwanamke huyo ndiye chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yao miaka 10 iliyopita. Mhegera ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu juzi amekuwa katika mvutano na mke wake ambaye waliachana miaka 10 iliyopita. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi majira ya saa1:30 asubuhi katika Parokia ya Bikira Maria, Kibangu na kueleza kuwa chanzo ni ugomvi wa kifamilia. “Adrian Mpande alijeruhiwa bega la kushoto na mtu anayedaiwa kuwa ni mkwe wake. Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa sababu ni mambo ya kifamilia,” alisema Kamanda Kaganda na kuongeza: “Tunaendelea na uchunguzi na kukiwa na umuhimu tutawaeleza kwa uwazi. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa Mzee Mpande alipigwa risasi mbili wakati akijiandaa kuingia kanisani kwa ibada juzi Jumapili. N

Mabasi 11 yafungiwa kufanya safari za mikoani

Image
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limefanya ukaguzi wa kushitukiza kwa mabasi ya kusafirisha abiria kwenda mikoani wilayani na maeneo ya vijijini na kugundua makosa mengi kwenye magari hayo  ambapo zaidi ya mabasi arobaini yametozwa faini huku  mabasi kumi na moja  yakifungiwa kusafirisha abiria baada ya kukutwa na makosa makubwa yanayohatarisha uhai wa wasafiri. Katika ukaguzi huo maafisa wa jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani wamegundua makosa mengi yakiwemo kukosa mikanda ya abiria uchakavu wa maumbo ya magari na kati ya zaidi ya mabasi hamsini yaliyokaguliwa madereva watano wenye makosa sugu wamefikishwa mahakamani. Wakizungumzia operesheni hiyo wafanyakazi wa mabasi na mawakala wamekuwa na maoni tofauti wakati wengine wakidai kutopatiwa muda wa kutosha kufanya marekebisho wengine wameunga mkono  zoezi hlo  huku abiria wakieleza walivyoathirika.

SPIKA JOB NDUGAI ATAMBULISHWA KWA MASPIKA WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA

Image
Mhe Spika Job Ndugai akitambulishwa katika mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika unaofanyika Abuja Nigeria.Mkutano huo unafanyika kujadili masuala mbali mbali yanayohusu mabunge hayo unashirikisha Maspika toka nchi 18 za Jumuiya ya Madola Barani Afrika

Baba Adaiwa Kutaka Kumtoa Kafara Mwanaye!

Image
Msichana anayedaiwa kupewa mimba na Babu mmoja.   STORI: IMELDA MTEMA, DAR DUNIA imekwisha! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia kuwepo kwa matukio mawili ya kusikitisha, moja la baba aliyefahamika kwa jina la Ombani Emmanuel mkazi wa Pansiansi jijini Mwanza, kukamatwa na polisi kwa kumfanyia vitendo vya kikatili mwanaye ikiwa ni pamoja na kudaiwa kutaka kumtoa kafara na tukio lingine ni la babu mmoja kudaiwa kumpa mimba mjukuu wake. Katika tukio la kwanza imedaiwa kuwa Emmanuel, hivi karibuni alikamatwa na polisi kwa kile kinachodaiwa kumfanyia mambo ya ajabu mwanaye mwenye umri wa miaka 10, huku majirani wakidai kuwa, kulikuwa na kila dalili za baba huyo kutaka kumtoa kafara. …Akiwa katika pozi. Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee, Flora Lauo alidai mambo aliyokuwa akifanya baba huyo yalikuwa yakiwakera majirani wengi kwa sababu mbali na kuwepo kwa dalili za kutaka kumfanyia tukio baya, pia alikuwa hamruhusu kujichanganya na mtu yeyot

SHILOLE: UMAMA N’TILIE UMENITEKA KULIKO MUZIKI

Image
Zuwema Mohammed ‘Shilole. MWANAM-UZIKI wa miondoko ya mduara, Zuwema Mohammed ‘Shilole’ ameweka wazi kuwa huenda akaukacha muziki siku za usoni kutokana na kunogewa na biashara yake ya kuuza chakula katika mgahawa wake.Akizungumza na Risasi Vibes, Shilole alisema anaona biashara yake hiyo inampa faida nyingi kuliko uigizaji na hata muziki anaofanya, hivyo kutokana na maisha magumu ni bora kufanya kitu kinachomu-ingizia kipato. “Huku kwa mama ntilie naona kunanilipa zaidi ya sehemu nyingine ambazo nipo, sasa ni bora kufanya kitu ambacho kina kuingizia kipato kuliko kung’ang’ania sehemu ambayo haikulipi au inakulipa kidogo tena kwa kusubiri,” alisema Shilole.

“Wanaume wa WCB wote Waaminifu” – Babutale

Image
 Kutoka Makao Makuu ya WCB kwa Meneja wa mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz na Tip Top Connection, Babutale leo July 25, 2017 amepost picha yenye maneno yalioandikwa ‘Wanaume wa WCB wote waaminifu’ kupitia ukurasa wake wa Instagram @babutale

Lile sakata la mama kuibiwa mtoto kutua kwa JPM

Image
DAR ES SALAAM: Lile sakata la mwan­amama Asma Juma (29) aliyedai kujifungua watoto wawili mapacha katika Hospitali ya Temeke Machi mwaka huu, limechukua sura mpya baada ya familia yao kusema italifikisha suala hilo kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kupatiwa suluhisho. Hatua ya familia hiyo inatoka­na na kutoridhishwa na ripoti iliyotolewa na timu iliyoundwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambayo ilidai baada ya uchunguzi wa kina, ilibainika kuwa mama huyo al­ijifungua mtoto mmoja, tofauti na madai yake kuwa alikuwa na ujauzito wa mapacha waw­ili. Akizungumza na Risa­si Mchanganyiko jana, mama huyo alisema yeye na mumewe, hawajakubaliana hata kidogo na ripoti hiyo ili­yotolewa siku chache zilizopi­ta na kwamba msimamo wao upo palepale. “Ile ripoti iliniumiza mno, ni ngumu kwangu kukubaliana nayo, tumeona bora kwenda kwenye haki za binadamu ili watusaidie swala letu, kwa mujibu wa ripoti hiyo inasema sikuzaa mapach

TRA yaanika deni la Acacia, ni sawa na 'bajeti ya miaka 13'

Image
Mamlaka ya Mapato (TRA) imeitaka Kampuni ya Acacia kulipa zaidi ya Sh424 trilioni kutokana na ukwepaji kodi ilioufanya kuanzia mwaka 2000. Kwa kutumia bajeti ya sasa, fedha hizo ni sawa na bajeti ya Tanzania ya miaka 13. Deni hilo, ambalo ni sawa na dola 190 bilioni za Kimarekani limetokana na hesabu zilizopigwa kwa kutumia taarifa iliyotolewa na kamati mbili zilizoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza usafirishaji wa mchanga wa madini unaofanywa na kampuni hiyo kutoka migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi. Taarifa iliyotolewa jana na kampuni hiyo imekataa kulipa deni hilo kwa maelezo kwamba haijapewa ripoti ya kamati zote mbili. “Hatuyakubali makadirio haya. Kampuni itaangaalia haki na namna zote zilizopo kuhusu suala hili,” inasema taarifa hiyo. Kwa mujibu wa Acacia, deni hilo limeelekezwa kwa kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine (BGML) inayoendesha mgodi wa Bulyanhulu, na Pangea Minerals (PML) inayosimamia mgodi wa Buzwagi. Taarifa hiyo iliyo

Masanja Alivyokutana na Majeruhi wa Lucky Vicent nchini Marekani

Image
Emmanuel Mgaya, Maarufu kama Masanja Mkandamizaji akiwa nchini Marekani amekutana na kuzungumza na watoto Sadia na Wilson ambao ni majeruhi ya ajali ya shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha wanaopatiwa matibabu nchini humo.  Masanja pia kupitia ukurasa wake wa instagram amethibisha kukutana na watoto hao: MUNGU AMENIPA NEEMA YA KWENDA KUWAONA WADOGO ZETU WALIOPATA AJALI SADIA NA WILSON NA KUWEPO MAREKANI KWA MATIBABU….. IMEKUWA SIKU NJEMA KWETU SOTE TUMEFURAHI PAMOJA NAO KULA NAO NA KUMTAFAKARI MUNGU KWA PAMOJA. LAKINI PIA NIMEZUNGUMZA NA WENYEJI WAO WALIOFANIKISHA SAFARI YA WAO KUJA MAREKANI!! HAKIKA MUNGU NI MWEMA WAMEENDELEA KUIMARIKA NA WANAENDELEA VIZURI!! SHUKRANI KWA MADAKTARI NA KILA ALIYETENGA MDA WAKE KUWAOMBEA!! WAZAZI WAO WANAWASALIMU NA WANAWASHUKURU KWA USHIRIKIANO NA MAOMBI YENU..🙏🏾🙏🏾🙏🏾 Tazama picha:

TCU Yataja Vyuo Vilivyozuiliwa Kudahili Wanafunzi 2017/18

Image
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imetoa orodha ya vyuo vilivyozuiliwa kufanya udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo 2017/18. Orodha hii imetolewa wakati wahitimu wa kidato cha sita wakiwa wanaendelea na mchakato wa kutuma maombi vyoni.  

Rihanna ‘The Bad Gal’ Uhuni, Usela Vinampa Mkwanja Mnono

Image
Rihanna. UKIMTAZAMA mwonekano wake jinsi alivyo mrembo, mwenye haiba nzuri ya kike, mvuto wa asili na sauti yenye utamu wa aina yake, huwezi kumdhania kwamba nyuma ya pazia ni mhuni na ‘msela’ aliyepitiliza! Jina lake halisi anaitwa Robyn ‘Rihanna’ Fenty, anapenda zaidi ukimuita Riri au The Bad Gal, mwanadada asiyechuja kutoka Visiwa vya Barbados, anayefanya poa kinoma kwenye anga la muziki wa kimataifa, maskani yake yakiwa nchini Marekani. Jina lake ni miongoni mwa wasanii wachache wa kike wanaoitingisha dunia kwa sasa, akichuana vikali na Beyonce Knowles, ingawa wapo baadhi ya watu wanaosema si sahihi kuwapambanisha wawili hao kwani Beyonce ni mkongwe na ana mafanikio zaidi ya Rihanna. Miongoni mwa matukio ya hivi karibuni yanayodhihirisha jinsi Rihanna ‘alivyopinda’, ni kwenye video ya Wimbo wa Wild Thoughts wa DJ Khaled , akiwa amemshirikisha mwanadada huyo na chalii mwingine, Bryson Tiller. Ukiisikiliza ngoma hii iliyoachiwa mwishoni mwa mwezi uliopita,