Mabasi 11 yafungiwa kufanya safari za mikoani


Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limefanya ukaguzi wa kushitukiza kwa mabasi ya kusafirisha abiria kwenda mikoani wilayani na maeneo ya vijijini na kugundua makosa mengi kwenye magari hayo  ambapo zaidi ya mabasi arobaini yametozwa faini huku  mabasi kumi na moja  yakifungiwa kusafirisha abiria baada ya kukutwa na makosa makubwa yanayohatarisha uhai wa wasafiri.

Katika ukaguzi huo maafisa wa jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani wamegundua makosa mengi yakiwemo kukosa mikanda ya abiria uchakavu wa maumbo ya magari na kati ya zaidi ya mabasi hamsini yaliyokaguliwa madereva watano wenye makosa sugu wamefikishwa mahakamani.

Wakizungumzia operesheni hiyo wafanyakazi wa mabasi na mawakala wamekuwa na maoni tofauti wakati wengine wakidai kutopatiwa muda wa kutosha kufanya marekebisho wengine wameunga mkono  zoezi hlo  huku abiria wakieleza walivyoathirika.

Comments

Popular posts from this blog