AMPIGA RISASI BABA MKWE WAKE KANISANI

Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo juzi majira ya saa1:30 asubuhi katika Parokia ya Bikira Maria,
Kibangu na kueleza kuwa chanzo ni ugomvi wa kifamilia.
“Adrian
Mpande alijeruhiwa bega la kushoto na mtu anayedaiwa kuwa ni mkwe wake.
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa sababu ni mambo ya kifamilia,”
alisema Kamanda Kaganda na kuongeza: “Tunaendelea na uchunguzi na kukiwa
na umuhimu tutawaeleza kwa uwazi.
Mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa
Mzee Mpande alipigwa risasi mbili wakati akijiandaa kuingia kanisani kwa
ibada juzi Jumapili.
Nipashe
Comments
Post a Comment