ZARI THE BOSS LADY AIBUA MAZITO TENA BAADA YA KIFO CHA MAMA YAKE,WASEMA ANA ROHO NGUMU
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na mama yake, Halima Matovu Hassan ‘Mama Zari’ enzi za uhai wake. Kifo cha mama mzazi wa staa ambaye ni mjasiriamali Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Halima Matovu Hassan ‘Mama Zari’ (58) kilichojiri Alhamisi iliyopita nchini Uganda, kimeibua gumzo ambalo si la nchi hii.Gumzo hilo kutoka nyumbani kwa mama Zari huko Busunju, Munyonyo jijini Kampala, Uganda lilihitimishwa wikiendi iliyopita na vyombo vya habari za mastaa nchini humo baada ya mazishi ya mama Zari yaliyofanyika mchana wa Ijumaa iliyopita, kuwa, Zari ana roho ngumu aisee!Kwa mujibu wa vyombo hivyo, wakati wa kifo cha aliyekuwa mume wa Zari, Tycoon Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ aliyefariki dunia Mei 25, mwaka huu, mwanamama huyo, kabla, wakati na baada ya mazishi ya baba watoto wake huyo alikosolewa juu ya tabia alizozionesha wakati wa msiba huo.Ilielezwa kuwa, baadhi ya mambo aliyoyafanya wakati ule ikiwemo kuposti vitu mitandaoni, mara akik