Katibu wa Habari Ikulu Ajiuzulu Kupinga Uamuzi wa Rais Trump
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House, Shawn Spicer, amejiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kupinga mabadiliko ya Timu ya Mawasiliano ya Ikulu hiyo.
Bw. Spicer ameachia wadhifa huo, kwa
sababu hakufurahishwa na uamuzi wa kumteua, Anthony Scaramucci kuwa
Mkrugenzi mpya wa Mawasiliano wa Ikulu,
Mabadiliko hayo yanafanyika wakati
White House ikikabiliwa na uchunguzi kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia
uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka jana.
Gazeti la New York Times linaarifu
kwamba, Bw. Spicer alipinga vikali uteuzi wa Bw. Scaramucci kama
Mkurugenzi wa Mawasiliano akidai ni kosa kubwa.
Bw. Scaramucci, ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Mike Dubke kujiuzulu Mei mwaka huu.
Comments
Post a Comment