WAZIRI PROF. MAGHEMBE AMEWAPOKEA MABILIONEA 28 KUTOKA MABARA YOTE DUNIANI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea
26 kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakiwa na
wenza wao katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
wakati wa mapokezi yao jana kwa ajili ya ziara yao ya siku tatu nchini
Tanzania.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi
(katikati waliosimama) akizungumza na Mabilionea hao. Kulia kwake ni
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe .
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea
hao jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania
(TANAPA), Alan Kijazi.
Kiongozi
wa msafara wa Mabilionea hao, Perry Amber akizungumza wakati wa mapokezi
hayo jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti.
Mabilionea hao kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakimsikiliza Waziri Maghembe.
……………………………………………………………………..
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amewapokea Mabilionea 26 wa
taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakiwa na wenza wao
katika Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa ajili ya kutembelea vivutio vya
utalii katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.
Mabilionea
hao ambao wanatoka katika mabara yote duniani wapo nchini Tanzania kama
sehemu ya ziara yao katika nchi 8 duniani ikiwemo Uingereza, Rwanda,
Maldives, Nepal, Bhutan na Rajastan.
Katika
hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake, Prof. Maghembe
aliwakaribisha Tanzania na kwenye Maajabu ya Dunia yanayobebwa na
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Alisisitiza “hakuna eneo lolote katika
uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivores)
na wale wanaokula nyama (canivores) kama Serengeti”.
Prof.
Maghembe aliwaeleza Wageni wake kuwa kuhifadhi ni gharama kubwa
inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia. Hivyo akawaomba wageni hao
wawe mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo lenye amani na vivutio
vyenye ubora wa pekee. Hatua hiyo italeta watalii wengi na kuiongezea
Tanzania mapato.
Aidha,
aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi
unaokua kwa wastani wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.
Comments
Post a Comment