RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO
Mh.David Kafulila
Na Editha Karlo- Globu ya Jamii Kigoma
RAIS Wa
Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza aliekuwa
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ,David Kafulila kwa kujitoa Muhanga
kutetea Watanzania kupitia sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo
Mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.Akizungumza
na Wananchi wa Kata ya Nguruka,leo Katika uzinduzi wa Mradi mkubwa wa
Maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza, alisema atakuwa
mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya
kuibua Ubadhilifu uliofanywa na Kampuni ya IPTL ambapo kwasasa suala
hilo ameanza kulifanyia kazi na mafanikio yameanza kuonekana.
Amesema
Kafulila alitukanwa sana alipo ibua sakata la Escrow na kuitwa majina
mengi ya kudhalilishwa kama tumbili na mengine mengi ya ajabu kwasababu
ya uzalendo wake wa kutetea Taifa.
"Mimi
ninafahamu unapoibua kitu cha kizalendo lazima usemwe, hivyo
ninampongeza Kafulila kwa uzalendo wake kwa nchi na nitaendelea
kumpongeza maisha yangu yote"alisema Magufuli.Magufuli alisema maendeleo
hayana chama ndio maana Kafulila alijitoa kwa hali ya juu na kutetea
fedha za Wananchi zilizo kuwa zikiibiwa na mafisadi wachache na
kujinufaisha wao.
"Ninajua
Kafulila ulitukanwa sana wakati wa kuibua sakata la Escrow, wapo watu
walikuita tumbili mimi najua wewe sio tumbili ,matumbili ni wao wewe
najua ni wa Chama kingine lakini umefanya kazi kubwa ya kulinda maslahi
ya nchi, kwahiyo nitakuwa mnafiki sana nisipo kupongeza kitu
ulichokifanya ni kikubwa Kwa,Taifa naomba nikupongeze kwa hilo",
Alisema
Kiongozi mzuri ni yule ambae anatetea wananchi bila kujali chama wala
siasa za uchochezi , hivyo atahakikisha kuwa Wananchi hawateseki na Wale
ambao wameiba fedha za serikali na Wananchi wanazirudisha bila kujali
nyadhifa walizonazo, ili pesa hizo zitumike katika kuleta maendeleo.
Rais
Magufuli aliwaahidi Wananchi wa Nguruka atahakikisha anatatua kero ya
Maji na umeme katika kata yao,kuhusu suala la umeme atamtuma Waziri wa
Nishati na madini ili aweze kutatua tatizo hilo na kuwasaidia Wananchi
kuepukana na shida hizo.
Rais
Magufuli amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kwa
kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji mkubwa katika kata ya Nguruka
uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 ambao unatarajiwa kukamilika
desemba 30 mwaka huu ambao utafuta kero ya maji kwa wananchi wa kata ya
Nguruka.
Akiongea
kwa njia ya simu na mtandao huu akiwa jijini Dar es Salaam aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Kigoma kusini kupitia tiketi ya chama cha NCCR
Mageuzi David Kafulila kuhusu kauli ya Rais Kafulila amesema kuwa Rais
amekuwa akimtia moyo kwani anaona kazi aliyokuwa akiifabya sasa imeanza
kuleta matokeo mazuri.
"Kwakweli
nafarijika na inanipa moyo wa kizalendo zaidi ninapo ona Rais anaunga
mkono sakata la Escrow ambalo mimi ndo nililiibua wakati nikiwa mbunge
japo nilipitia kwenye kipindi kigumu "alisema Kafulila
Kafulila alisema kuwa wakati akiwa mbunge kwenye sakata la Escrow msimamo wake na Rais ulikuwa unafanana toka bungeni.
Comments
Post a Comment