FAHAMU MADHARA YA KUTOBOA PUA, MDOMO NA ULIMI!
Katika
zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili
na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika
tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi
kwa sababu tofauti tofauti sana. Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama
ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla
hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili.
Kutoga Ulimi ama Mdomo kunaweza kukusababishia madhara yasiyotarajiwa.
Matokeo
mazuri zaidi ya kutoga ulimi ama mdomo ni kutokutokea kwa kidonda ama
kivimbe, wakati matokeo mabaya kutokea kwa baadhi ya watu ni pamoja na
kuvunjika kwa meno/jino, kuvuja kiasi kikubwa cha damu, ama maambukuzi
ya bakteria kwenye kidonda. Kutoga ulimi hujumuisha kutumika kwa sindano
inayopenyezwa katikati ulimi ili kupitisha na kuhifadhi kipini, ama
ndoana ama hereni ya urembo. Kazi hii ya kutoga ulimi mara nyingi ganzi
huwa haitumiki. Baada ya kutoga, kuvimba kwa ulimi na maumivu ya muda
hutokea.
Madhara ya kutoga Ulimi
Kuvuja
damu kiasi kidogo hutarajiwa, kuna hatari ya mishipa ya damu kuharibiwa
wakati wa kutoga ulimi, hali inayoweza kusababisha kuvuja damu kwa kiasi
kikubwa kuliko ilivyotarajiwa.
Ingawa
kuvimba kwa ulimi kunatarajiwa baada ya kitendo cha kutoga ulimi, wakati
mwingine ulimi huvimba kwa kiasi cha kuziba kwa njia ya hewa. Kuziba
kwa njia ya hewa kunaweza kusababisha kifo
Comments
Post a Comment