Posts

Ruby Ajazwa Kibendi

Image
Msanii Hellen George ‘Ruby’ JAZA ujazwe! Habari ya mjini kwa sasa inamhusu sexy lady wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ kujazwa kibendi na staa mkubwa wa muziki huo, licha ya kwamba mwanadada huyo amekuwa akifanya siri. Chanzo makini kililieleza Ijumaa Wikienda kuwa, Ruby ana ujauzito ambao umekuwa ukimfanya ajifichefiche huku akimficha aliyemjaza kibendi hicho kwa madai kuwa, jamaa aliyempachika kibendi amezaa na wanawake tofauti. Kama ilivyo desturi yake, Ijumaa Wikienda lilimnyatia Ruby ambaye alikiri kuwa mjamzito, lakini akatia ngumu kumtaja baba kijacho na umri wa mimba yake kwani wakati muafaka haujafika. “Mimba bado ni changa, siwezi kusema ina miezi mingapi. Kuhusu nimepewa na mwanamuziki mkubwa, siyo kweli ila ipo siku wakati ukifika nitasema ni ya nani,” alisema Ruby

MUIGIZAJI WA HOME ALONE AFARIKI DUNIA

Image
Aliyekuwa muigizaji wa Home Alone1,Home Alone 2 na Lost in New York, John Heard ameripotiwa kufariki dunia akiwa katika chumba cha hoteli moja jijini Callifonia. Muigizaji huyo ambaye amepata umaarufu kupitia filamu hizo zilizotamba miaka ya 90, amefariki akiwa na miaka 72, Mpaka sasa chanzo cha kifo cha muigizaji huyo hakijawekwa bayana. Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, marehemeu alikuwa amejipumzisha katika hoteli hiyo baada ya kufanyiwa upasuaji siku ya Jumatano katika kituo cha afya cha Stanford. Marehemu ameacha mke Margot Kidder na mtoto wake mmoja aitwaye John Matthew “Jack”

Uwoya, Kelvina Hapatoshi!

Image
Irene Uwoya. SIFA ya ubuyu wenye rangi nyekundu ni kuacha rangi midomoni vivyo hivyo penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Wamama wawili wa Bongo Muvi, Irene Uwoya na Kelvina John, wanadaiwa kuingia kwenye vita nzito ya penzi la msanii wa Bongo Fleva, Patrick Chrisopher ‘PCK’ na sasa hapatoshi, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye ubavu wa kukupa ubuyu ulionyooka. MAPENZI SHATASHATA Chanzo makini cha ubuyu huo kililieleza Ijumaa Wikienda kuwa, kwa sasa PCK na Kelvina ni mahaba niue au mapenzi shatashata, jambo ambalo linamchukiza Uwoya ambaye anasemekana kwamba, aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo anayesifika kwa kuwachanganya na kuwapanga kama mafungu ya nyanya mastaa wa kike Bongo. “Hivi watu wa ubuyu mnajua kuwa kuna vita nzito kati ya Uwoya na Kelvina? Unaambiwa sasa hivi vita yao siyo ya nchi hii na wanaviziana kama Korea Kaskazini na Marekani, eti, kisa nasikia wanagombea penzi la PCK. WAKUTANA BAA YA UWOYA “Tukio bichi la Uwoya na Kelvin

Lipumba Atangaza Kuwavua Uanachama Wabunge 8 wa CUF

Image
Profesa Ibrahim Lipumba. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge wanane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho. Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam, kwa makosa kama hayo. Profesa Lipumba ametangaza uamuzi huo leo Jumatatu, Julai 24 wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam. “Leo asubuhi tumewasilisha nyaraka  za hatua hizi kwa Spika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa hatua zaidi,” amesema Profesa Lipumba. Amesema wabunge hao wanane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na Chadema kumwondoa yeye madarakani.

WAZIRI PROF. MAGHEMBE AMEWAPOKEA MABILIONEA 28 KUTOKA MABARA YOTE DUNIANI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea 26 kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakiwa na wenza wao katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa mapokezi yao jana kwa ajili ya ziara yao ya siku tatu nchini Tanzania. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi (katikati waliosimama) akizungumza na Mabilionea hao. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe . Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea hao jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi. Kiongozi wa msafara wa Mabilionea hao, Perry Amber akizungumza wakati wa mapokezi hayo jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.  Mabilionea hao kutoka taasisi ya Young Presidents Organ

Mboto: Mzee Majuto Hajafa Jamani!

Image
MSANII wa filamu nchini, Haji Salum maarufu kama Mboto , amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zinazodai kuwa nguli wa vichekesho katika tasnia ya uigizaji , Amri Athuman maarufu kama King Majuto amefariki dunia. Mboto baada ya kupata taarifa hizi alifunga safari kuelekea mkoani Tanga ambapo ni nyumbani kwa Mzee Majuto na kumkuta hai, na amekanusha uvumi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuposti picha inayowaonyesha yeye na Majuto wakiwa nyumbani kwake, na picha hiyo iliambatana na maneno yafuatayo: “ Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu Mzee Majuto nimelazimika kuja kwake Tanga . Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye Tanga ,” ameandika Mboto . Siku chache zilizopita, gazeti la Ijumaa Wikienda liliripoti taarifa za kuumwa kwa Mzee Majuto , anayesumbuliwa na tatizo la ngiri, lakini jana kwenye mitandao ya kijamii zikaenea taarifa zisizo za kweli kwamba King Majuto amefariki

FAHAMU MADHARA YA KUTOBOA PUA, MDOMO NA ULIMI!

Image
Katika zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi kwa sababu tofauti tofauti sana. Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili. Kutoga Ulimi ama Mdomo kunaweza kukusababishia madhara yasiyotarajiwa.  Matokeo mazuri zaidi ya kutoga ulimi ama mdomo ni kutokutokea kwa kidonda ama kivimbe, wakati matokeo mabaya kutokea kwa baadhi ya watu ni pamoja na kuvunjika kwa meno/jino, kuvuja kiasi kikubwa cha damu, ama maambukuzi ya bakteria kwenye kidonda. Kutoga ulimi hujumuisha kutumika kwa sindano inayopenyezwa katikati ulimi ili kupitisha na kuhifadhi kipini, ama ndoana ama hereni ya urembo. Kazi hii ya kutoga ulimi mara nyingi ganzi huwa haitumiki. Baada ya kutoga, kuvimba kwa ulimi na maumivu ya m

RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO

Image
Mh.David Kafulila Na Editha Karlo- Globu ya Jamii Kigoma RAIS Wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ,David Kafulila kwa kujitoa Muhanga kutetea Watanzania kupitia sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo Mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nguruka,leo Katika uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza, alisema atakuwa mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuibua Ubadhilifu uliofanywa na Kampuni ya IPTL ambapo kwasasa suala hilo ameanza kulifanyia kazi na mafanikio yameanza kuonekana. Amesema Kafulila alitukanwa sana alipo ibua sakata la Escrow na kuitwa majina mengi ya kudhalilishwa kama tumbili na mengine mengi ya ajabu kwasababu ya uzalendo wake wa kutetea Taifa. "Mimi ninafahamu unapoibua kitu cha kizalendo lazima usemwe, hivyo ninampongeza Kafulil

Samatta Aandika Historia Mbele ya Rooney, Aifunga Everton

Image
KRC Genk vs Everton. Mtanzania Mbwana Samatta ameandika historia ya kuwa Mtanzania aliyeweza kufunga bao dhidi ya timu ya Everton ambayo inashiriki Ligi Kuu ya England baada ya kufanya hivyo katika mchezo wa kirafiki akiwa ndani ya jezi ya KRC Genk. Samatta ambaye amekabidhiwa jezi namba tisa hivi karibuni katika kikosi hicho, amefanikiwa kuifungia timu yake hiyo bao katika dakika ya 55 katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Everton ambao walikuwa na staa wao, Wayne Rooney. Bao la Samatta lilipatikana baada ya kupigwa pasi zaidi ya saba kuanzia kwa kipa wa Genk hadi mpira ulipomfikia Samatta ambaye alimalizia kwa kupiga shuti kali. Mchezo huo uliochezwa Jumamosi hii nchini Ubelgiji ni maalum kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa 2017/18 kwa timu zote mbili. Bao la Everton lilifungwa na Rooney katika dakika ya 45. Samatta amekuwa na mwendelezo mzuri katika mechi za maandalizi ambapo wiki iliyopita pia alifunga bao moja katika sare ya maba

Jerry Muro Aiponda Yanga, Adai Kuna Wanafiki

Image
Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema kuwa ilikufanikiwa katika utendaji ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria ni lazima kuangalia ni nani anakuletea ushauri. Muro ameyasema hayo ikiwa ni sikuchache tu zimepita tangu Yanga imtangaze msemaji mpya wa timu hiyo, Dismass Ten aliyochukua nafasi yake. “Yanga kuna majungu watu wanapenda wafanye vitu vyao, kuna wanafiki ambao watakwambia ufanye hiki ukikifanya unaingia chaka. “Wapo Yanga SC watu wenye msaada wa kweli, wazuri sana, wenye akili na wenye mapenzi ya kweli kuhakikisha Yanga inakuwa kama TP Mazembe watu wote hao wapo Yanga. “Unachotakiwa kufanya ni kufungua macho kuangalia ni nani anakuletea ushauri, maana kuna mwingine anakuletea ushauri wakati yeye kashindwa kuongoza nyumba yake kaachana na mkewe ,hajali watoto wake yeye mwenyewe kufua nguo hafui nguo maisha yake yamemshinda,” alisema Jerry Muro aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo. Mungu anasema unapojipenda nafsi yako wewe mp

Sanchi Anunua Kiwanja cha Milioni 70!

Image
VIDEO Queen Jane Rimoy ‘Sanchi ’ baada ya kufanya kazi zake za mitindo na upigaji picha amenunua kiwanja cha shilingi milioni 70 kilichopo Mbweni jijini Dar es Salaam . Akizungumza na Risasi Jumamosi , Sanchi alisema kuwa ameamua kununua kiwanja hicho kama moja ya kumbukumbu ya kazi zake alizofanya kwa kipindi cha miaka mitatu. “Unajua mtu akikuona upo kwenye mitandao ya kijamii unaweka picha mbalimbali hajui ni kitu gani unafanya kumbe kila mmoja ana akili yake, mimi najivunia kununua kiwanja hicho tena pembezoni mwa bahari kwani ndiyo ndoto yangu ya muda mrefu,” alisema Sanchi.

Wahuni wa Mwanza Wamng’oa Kucha Kajala

Image
    STAA wa filamu za Kibongo , Kajala Masanja hivi karibuni yalimkuta makubwa jijini Mwanza baada kunyofolewa kucha na wahuni alipokuwa kwenye majukumu ya kazi yake anayoifanya kwa sasa ya kampuni ya mchezo wa kubahatisha. Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Kajala alisema kuwa alikuwa kwenye harakati za kazi yake anayoifanya kwa sasa kwenye kampuni hiyo ambapo alikuwa akigawa tisheti ndipo mashabiki wakaanza kumvuta mkono mpaka kumbandua kucha aliyokuwa amebandika mkononi ambayo iliondoka na ukucha wake na kujikuta akipata jeraha na kumwaga damu nyingi. Kajala akipozi. “Yaani mimi nilikuwa sina ili wala lile nagawa matisheti mara wakaanza kunivuta kwa nguvu mpaka wakaitoa kucha yangu, hali hiyo ilinitesa asikwambie mtu jeraha la kucha linauma sana,” alisema Kajala. Aliongeza kuwa, baada ya kucha yake kubanduka alitoa kilio kikubwa kwani alipata maumivu yaliyosababisha ashindwe kuendelea na majukumu yake. “Maumivu niliyopata yalikuwa ni makali mno kias

Kimenuka: Mbasha ‘Amtolea Povu’ Flora

Image
Emmanuel Mbasha. Aliyekuwa mume wa Flora Mbasha ‘Madam Flora’ ambaye pia ni mzazi mwenziye, Emmanuel Mbasha ameibuka gumzo mitandaoni baada ya kuandika ujumbe wa ghadhabu unaodaiwa kuwa huenda ni dhidi ya mtalaka wake. Mbasha aliandika ujumbe huo kama majibu, baada ya hivi karibuni kusambaa kwa taarifa ambazo si za kweli zilizodai kuwa Flora alifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio na kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Mbasha, akisema uvivu wake kitandani ndiyo chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yao, ambapo Flora alikanusha vikali taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram. Flora Mbasha ‘Madam Flora’. Baada ya taarifa hizi kutua mezani kwa Emmanuel , alipiga kimya kwa muda kutokana na kuwa bize na msiba wa bibi yake, lakini baada ya mazishi, akaingia kwenye mahakama ya mastaa , Instagram na kuandika ujumbe huu. “Sipendi ujinga kabisa kwani hamuwezi kuuza hicho kidaftari chenu mpaka mtafute kiki kwangu?, acheni hizo mnaniingiza kwenye upumbavu wenu i

Katibu wa Habari Ikulu Ajiuzulu Kupinga Uamuzi wa Rais Trump

Image
Rais Trump na Shawn Spicer. Msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House, Shawn Spicer , amejiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kupinga mabadiliko ya Timu ya Mawasiliano ya Ikulu hiyo. Bw. Spicer ameachia wadhifa huo, kwa sababu hakufurahishwa na uamuzi wa kumteua, Anthony Scaramucci kuwa Mkrugenzi mpya wa Mawasiliano wa Ikulu, Mabadiliko hayo yanafanyika wakati White House ikikabiliwa na uchunguzi kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka jana. Gazeti la New York Times linaarifu kwamba, Bw. Spicer alipinga vikali uteuzi wa Bw. Scaramucci kama Mkurugenzi wa Mawasiliano akidai ni kosa kubwa. Bw. Scaramucci, ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Mike Dubke kujiuzulu Mei mwaka huu.

Mama aliyenaswa bila nguo ‘Airport’ Dar, Mapya yaibuka

Image
ZIKIWA zimepita siku tatu tangu mama mmoja kuzua kizaazaa karibu na eneo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kwa kukutwa akiwa barabarani bila nguo, mambo mapya yameanza kuibuka kuhusiana na siri ya kadhia hiyo. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni Banana, Praxeda Mkandara, ndiye aliyeanza kufichua undani wa kile kilichojiri baada ya kuiambia Nipashe katika mahojiano naye jana kuwa hakika, ni Mungu ndiye ajuaye juu ya uhai wa mama huyo kwa sababu alikuwa katika hatari kubwa ya kuumizwa vibaya na pia hata kuchomwa moto na wananchi walioshtushwa na tukio hilo. Alisema badala ya tuhuma za uchawi zinazoenezwa dhidi ya mama huyo ambaye mtaani kwao ni maarufu, ukweli alioupata kutokana na kauli yake mwenyewe ni kwamba alikuwa amevuliwa nguo na mtu aliyekuwa akidaiana naye siku nyingi na kuachwa eneo hilo. Alisema katika maelezo ya mama huyo, ni kwamba yeye si mchawi na hakuwa akifanya uchawi eneo hilo, bali kuna mtu aliyekuwa akimdai siku nyingi alikutana

Njia 10 Za Kupunguza Magonjwa Ya Mlipuko Wa Kuku

Image
Mlipuko wa magonjwa ni moja ya sababu za hasara kubwa kwa wafugaji na vifo vinavyotokea kwa wakati mmoja. Pindi mfugaji anapokumbwa na janga la vifo vya ndege, kabla ya kufikia mwisho wa mzunguko wa uzalishaji hivyo basi asitarajie kupata faida nzuri mara baada ya mauzo. Hasara itokanayo na vifo inaweza kuepukika au kupunguzwa na kutokea kwa kiasi kidogo. Hili linawezekana, ifuatayo ni namna ya kufanikisha hilo;- 1. Osha vyombo vya maji kila wakati na mwaga maji yaliyobaki. Hakikisha unamwaga maji yaliyosalia mbali na kuosha chombo na sabuni kila siku, weka maji safi yasiyo na dawa na wala usitumie maji ya mto au yale usiyoyajua chanzo chake. Kama utaweka maji dawa basi tumia ‘vitamini’ muhimu kama ‘vitalyte’ ambazo zinasaidia kuua vijidudu. 2. Wape maji kabla ya chakula. Ndege wapo tofauti na binadamu au wanyama wengine. Hakikisha unawapa maji kabla ya chakula hasa kama unatumia maranda, hii ni kuhakikisha hawakanyagani wanapogombania chakula sehemu moja. 3

WATANZANIA WATIKISA TENA TUZO ZA AFRIMMA 2017,DARASSA NA DIAMOND NAO NDANI

Image
Majina ya wasanii wanaowania tuzo za mwaka huu za Afrimma yametajwa. Diamond ameongoza kwenye orodha hiyo kwa kutajwa kwenye vipengele vitano. Rayvanny ametajwa katika vipengele vitatu wakati Darassa na Tuddy Thomas wakitajwa kwenye vipengele viwili. Wengine walitajwa ni Alikiba, Lady Jaydee, Vanessa Mdee, Yamoto Band, Dj D-Ommy, Dayna Nyange na Mose Iyobo. Tuzo hizo zitafanyika October 8 ya mwaka huu mjini Texas. Hii ni orodha kamili ya vipengele hivyo. Best Male West Africa Wizkid – Nigeria Falz – Nigeria Serge Beynaud – Ivory Coast Mr Eazi – Nigeria Toofan – Togo Moh Dediouf – Senegal Davido – Nigeria Stonebwoy – Ghana Tekno – Nigeria Kedejevara DJ (Ivory Coast) Best Female West Africa Tiwa Savage – Nigeria Yemi Alade – Nigeria Efya – Ghana Adiouza – Senegal Becca – Ghana Josey – Ivory Coast Mz Vee – Ghana Simi – Nigeria Best Male East Africa Eddy Kenzo – Uganda Diamond Platnumz – Tanzania Jacky Gosee – Et