Posts

Diwani Chadema Mbaroni kwa Tuhuma za Rushwa

Image
Diwani Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa  Sh.5,000,000/=. kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa  TAKUKURU wilaya ya  Kinondoni Teddy Mjangira, amesema kuwa Watuhumiwa walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha toka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa alitakiwa  na watuhumiwa kuwapa  rushwa ya Sh.10,000,000/= Inadawaiwa Watuhumiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango miji  inashughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo. Uchunguzi wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa k...

Majaliwa Amkalia kooni Mkurugenzi Lindi

Image
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Lindi, Samuel Warioba Gunzar leo alijikuta katika wakati mgumu mbele ya waziri mkuu wa Jamuhuri ya Tanzania, Kassim Majaliwa baada ya kukutana na maswali mzito mfululizo kutoka kwa kiongozi huyo wa juu wa nchi.  Hayo yamejiri katika mji mdogo wa Mtama kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa umefurika mamia ya wananchi. Hali ilikuwa mbaya kwa Gunzar kutokana na taarifa iliyotolewa na mbuge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye aliyekueleza waziri mkuu kwamba katika mji huo mdogo in unaokadiriwa kuwa na wakazi takribani 4000 hauna kituo cha afya.  Maelezo ya Nape yalisababisha waziri mkuu amuite mkurugenzi huyo aeleze nikwanini eneo hilo lisiwe na kituo cha afya wakati linaidadi kubwa ya watu. Huku akihoji kwanini imekuwa hivyo wakati kuna madiwani na watendaji katika halmashauri hiyo.  Alisema sera ya afya ipo wazi nasifa za kuwa na zahanati, vituo vya afya na hospitali zinafahamika. "Mkurugenzi  njoo utuele...

Usher Raymond atembelea mbuga ya Serengeti

Image
Usher Raymond Msanii wa Marekani Usher Raymond yuko ziarani nchini Tanzania akitembelea eneo la uhifadhi wa wanyama pori la Serengti National Park. Bwana Raymond alichapisha baadhi ya picha akiwa na familia yake katika akaunti yake ya Twitter. Alielezea hali ilivyo katika eneo hilo kama ya kufurahisha . Ripoti za Usher Raymond kuzuru Tanzania zilisambaa kwa haraka nchini humo. Watu wengine maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid David Becham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho, mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin ni miongoni mwa wale waliozuri katika sehemu mbali mbali za kitalii nchini humo mwaka huu. Vivutio vya kitalii nchini Tanzania kama vile mbunga ya uhifadhi wa wanyama pori ya Serengeti na mlima Kilimanjaro ni vivutio vinavyoongoza kwa utalii ambapo watu wengi maarufu wametembela.

ACACIA Yakubali Kulipa Mirabaha Iliyomo Kwenye Sheria Mpya Madini

Image
Balozi wa Canada nchini na Mwenyekti wa Barrick Gold Corporation (mmiliki mkubwa wa Acacia) Prof. Thornton wakiongea na waandishi wa habari Ikulu Dar. (Picha na Maktaba). Kampuni inayomiliki Makampuni ya Uchimbaji wa Madini ya ACACIA imesema italipa mirabaha iliowekwa katika sheria mpya za madini. Sheria mpya ya madini inawataka wawekezaji katka sekta hiyo kulipa asilimia 6 ya mirabaha ikiwa ni ongezeko la asilimia 2 zilizokuwepo awali, ambapo asilimia 1 ni kwaajili ya usafirishaji kwenda nje.

Umewaona mapacha wa Beyonce?

Image
Beyonce na mapacha wake. MWANAMUZIKI maarufu duniani, Beyonce Knowles kwa mara ya kwanza ameawaanika hadharani watoto wake mapacha ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya kujifungua. Alichokiandika Beyonce Januari akiwa na mimba. Muimbaji huyo kupitia mtandao wa Instagram, ameonyesha kuwa watoto hao wana mwezi mmoja tangu wamezaliwa. “Sir Carter and Rumi 1 month today. 🙏🏽❤️👨🏽👩🏽👧🏽👶🏾👶🏾,” ameandika Queen Bey kwenye mtandao huo. Mapacha hao waliozaliwa ni mmoja wa kike na mwingine wa kiume na tayari walishapewa majina ya Sir na Rumi.

Taiwan: Wabunge Wavurugana Bungeni, Wachapana Live

Image
Wabunge wakizichapa kavukavu. WABUNGE wa Taiwan leo walichapana makonde, wakarushiana viti na mabaluni ya maji baada ya kutofautiana kuhusu mradi mmoja wa miundombinu. Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio yaliyoanza jana ambapo katika kubishana, wabunge hao walikwidana mashati na kuchapana wakati wa kupitia bajeti ya mradi huo. Mpango huo ni moja ya miradi mikubwa iliyopendekezwa na Rais Tsai Ing-wen ambayo inajumuisha ujenzi wa reli za kutoa huduma ndogondogo, hatua za kuthibiti mafuriko na mazingira yanayosababishwa na viwanda. Hata hivyo, chama cha upinzani cha Kuomintang kinapinga mradi huo kikisema unapendelea miji na wilaya ambazo zinaunga mkono chama cha Democratic Progressive (DPP) ambako kina uhakika wa kuungwa mkono katika uchaguzi wa mikoa mwaka kesho. Isitoshe, wapinzani wanapinga kiasi kikubwa mno cha Dola bilioni 13.8 ambazo zitatumika katika mradi huo. Waziri Mkuu Lin Chuan alishindwa kutoa ripoti ya bajeti hiyo Alhamisi baada kutupiwa b...

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MADAKTARI AFRIKA YA NCHINI MAREKANI WAFANYA MATIBABU YA MOYO KWA WAGONJWA KWA KUWEKA KIFAA MAALUM

Image
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa kifaa maalum cha kurekebisha mapigo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) . Kushoto ni Daktari Bingwa na Magonjwa ya Moyo Mathew Sackett. Tangu kuanza kwa kambi hiyo mwanzoni wa juma hili jumla ya wagonjwa 20 wameshapatiwa matibabu kati ya hao nane wamewekewa Pacemaker na wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na kesho.  Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya Nchini Marekani Mathew Sackett akizungumza na waandishi wa habari na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa ulioufanya katika matibabu ya Moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana n...

Hakuna aliyekamilika, Cha Muhimu ni Kuvumiliana

Image
UHALI gani msomaji wangu! Ni matumaini yangu kuwa uko poa kabisa. Ni ijumaa nyingine nzuri ninayokualika kwenye uwanja huu, kwa wewe ambaye mambo yako hayaendi sawa, nakuombea kwa Mungu akufanyie wepesi. Mada yetu ya leo ni kama inavyojieleza, wapo baadhi ya watu ambao wao kamwe hawakosei, kila tatizo linapotokea basi wanawasukumia mizigo wenzi wao, wanaamini wao ni wakamilifu ila wenzi wao ndiyo wana matatizo. Ipo wazi kwamba uhusiano wa kimapenzi ni jambo ambalo linatakiwa kuwa la furaha, wewe na mwenzi wako muishi kwa upendo na amani, hata kama kunatokea misuguano, basi inakuwa ni ile ya kawaida ambayo mnaimaliza mapema, kwa amani na maisha yanaendelea. Kwa bahati mbaya, uhusiano wa kimapenzi wa watu wengi siku hizi, umejawa na migogoro, maudhi na karaha za mara kwa mara, hasa kwa wale wapenzi wanaoishi kwenye uhusiano wa kudumu, uwe ni uchumba au ndoa. Jambo ambalo watu wengi huwa hawalijui, ni kwamba amani, upendo na maelewano huwa haviji tu, ni lazima vij...

Malinzi ajiuzulu Urais TFF Akiwa Rumande

Image
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amejiuzulu wadhifa wake wa Ujumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Kupitia kwa wakili wake, kampuni ya Rwegoshora, Malinzi amewaandikia barua FIFA kuwataarifu kujitoa kwenye Kamati hiyo kutokana na kuwa mikononi mwa dola kwa sasa. Malinzi, pamoja na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga. wapo rumande hadi Julai 17, upepelezi wa kesi yao utakapokamilika baada ya kunyimwa dhamana Julai 3 katika kesi inayowakabili. Watatu hao walipandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza Juni 29 na kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam. Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isaw...
Image
Katika hatua isiyo ya kawaida, binti yake Bwana Trump, Ivanka, alikaa kwa niaba ya baba yake wakati wa kikao kinachohusu Afrika kwenye mkutano wa nchi tajiri wa G20. Vikao vya asubuhi vililenga masuala muhimu ya uhamiaji na afya. Picha iliyowekwa twitter na mmoja wa wapatanishi kutoka Urusi ilimwonyesha Ivanka Trump akikaa katikati ya Rais wa China Xi Jinping na waziri mkuu wa Uingereza, Bi Teresa May. Mwandishi wa BBC katika mkutano huo anasema hakumbuki kuwepo na mipango kama hiyo hapo zamani na kiongozi wa nyadhifa ya juu kama vile waziri wa mambo ya nje, ndio aghlabu huchukua nafasi ya Rais. Bi Trump hakuonekana akishiriki katika mchango wowote kuhusu uhamiaji wa raia wa Afrika kuelekea Ulaya na afya wakati babake alipokuwa ameondoka. Picha ya uwepo wake ilichapishwa katika mtandao wa Twitter na mshiriki mmoja wa Urusi na kuzua hisia kali katia mitandao ya kijamii. Baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo walisema kuwa bi Trump hajachaguliwa wala...

PROFESA JAY AFUNGA NDOA KANISA LA ST. JOSEPH -DAR

Image

Abdi Banda ameaga rasmi Simba

Image
BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Hassan Banda amefikia makubaliano na klabu ya Baroka F.C ya Afrika Kusini kusaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga nayo. Baada ya kung’ara katika michuano ya Kombe la COSAFA Castle nchini Afrika Kusini akiiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tatu, mchezaji huyo wa Simba ya nyumbani, Tanzania sasa anakaribia kwenda kuanza maisha mapya timu hiyo ya Ga-Mphahlele, karibu na Polokwane, Limpopo ambayo inacheza Ligi Kuu ya nchini humo. Banda amesema anaondoka Simba SC aliyoichezea kwa miaka miwili, baada ya kumaliza mkataba wake na hakuwahi kusaini mkataba mpya, hivyo anajiunga na Baroka kama mchezani huru. “Nipo njiani narudi nyumbani kwa ajili ya kuja kuchukua vitu na kurudi rasmi Afrika Kusini kuanza maisha mapya na klabu yangu mpya ya Baroka,”amesema Banda akizungumza kwa simu leo. Banda alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza michuano ya COSAFA Castle na kutwaa Medali ya Shaba baada ya ushindi wa penalti...

Viongozi wawili wa serikali wauawa Kwa Kupigwa Risasi Kibiti

Image
Viongozi wawili wa serikali za mtaa katika Kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti mkoani Pwani wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumatano, Juni 28. Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga zimeeleza kuwa waliouawa ni Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi, Shamte Makawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus. Aidha, kamanda wa polisi amesema kuwa tayari askari wamekwenda eneo hilo kwa ajili ya hatua zaidi. Hadi sasa watu zaidi ya 37 tayari wameuawa katika mfululizo wa matukio ambayo bado Polisi hawajafahamu ni nani mhusika na lengo haswa la kufanya hivyo.

Rais Wa TFF Na Katibu Wake Watiwa Mbaroni

Image
Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao.  Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao. Licha ya kuwa tuhuma zinazowakabili hazijawekwa wazi, lakini mwezi uliopita ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliripoti kuhusu mabilioni ya shilingi yaliyobainika kuchotwa kwenye akaunti za TFF na kulipwa kwa wadau wa soka kinyume cha sheria. Miongoni mwa waliotuhumiwa kunufaika na fedha hizo ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa msaidizi wake, Juma Matandika...

MBUNGE WA CHADEMA ASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE

Image
Siku kadhaa zilizopita kutoka Bungeni Dodoma Wabunge wa CHADEMA Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda Mjini walisimamishwa kutohudhuria vikao vya Bunge, leo June 28, 2018 Mbunge Conchesta Rwamlaza wa Viti Maalum CHADEMA amesimamishwa. Conchesta Rwamlaza amesimamishwa kutohudhuria Vikao vitatu vya Bunge linaloendelea kwa kosa la kusema uongo mbele ya Bunge akimtuhumu Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka kujimilikisha ardhi yenye ukubwa wa ekari 400 kinyume cha sheria taarifa ambazo sio za kweli. Aidha, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa msamaha kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwa kosa alilolifanya May 30, 2017 kudharau mamlaka ya Spika ikiwemo kupiga kelele Bungeni na kutupa karatasi ovyo. Nassari amepata msamaha huo kwa kuwa imeonesha ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo kisha kupelekwa mbele ya Kamati.

Kafulila afunguka haya kuhusu Escrow

Image
DAR ES SALAAM: WAKATI gumzo nchi nzima likiwa ni wizi mkubwa ambao haujawahi kufanyika wa zaidi ya shilingi bilioni 300 kutoka akaunti iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Tegeta Escrow, imeelezwa kuwa baadhi ya wabunge walikuwa wakihatarisha maisha yao na wengine wamepoteza ubunge kwa sababu ya kupinga ufisadi huo. Vinara wa kufichua sakata hilo, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ndiyo waliofichua mambo hayo kwa nyakati tofauti. Kafulila aliyehojiwa na gazeti hili wiki iliyopita alisema kundi lao la kupiga vita ufisadi huo lilikuwa hatarini kwa sababu kuna fedha zilikuwa zinatumika ili kuzima wizi huo. Marehemu Deo Filikunjombe (ushoto), Davidi Kafulila, Zitto Kabwe pamoja na David Silinde. “Hata wenzetu wabunge walikuwa wakitupinga na kwa kweli tulikuwa katika wakati mgumu, hata hivyo, hatukuacha kupigania jasho la umma ambalo lilikuwa limeliwa na watu wachache,” alisema Kafulila. Alisem...

BABU KIKONGWE WA MIAKA 80 AISHI KWA KULA UDONGO

Image
  Katika hali ya kushangaza na kusikitisha sana, kikongwe mmoja aitwaye Athuman Ngusa Kulaba (80) amekuwa akiishi kwa kula udongo wa nyumba anayoishi kwa sababu ya kukosa chakula cha kibinadamu. Kikongwe huyo alikutwa na Uwazi hivi karibuni nyumbani kwake, Chanika wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam baada ya majirani kusema kwamba wamekuwa wakimshuhudia akipata mlo huo kwa karibu mwaka mmoja sasa. Baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, mjumbe wa eneo hilo, John Kanguya na majirani  zake walimchukuwa hadi kwenye Kituo cha Afya cha Chanika kwa ajili ya kumpima afya yake ambapo madaktari walisema tayari alipatwa na ugonjwa wa safura ambapo tumbo lake limejaa minyoo. Uwazi lilishuhudia sehemu kubwa ya ukuta wa nyumba anayoishi kikongwe huyo ikiwa imemeguka kwa ajili ya kuchimbuliwa na kuliwa. Majirani walilieleza Uwazi kwamba, nyumba anayoishi kikongwe huyo aliachiwa kuilinda na mtu aliyetajwa kwa jina moja la Musada karibu miaka 20 i...

Njia hizi 16 za kuondoa Sumu Mwilini

Image
NJIA 16 ZA KUONDOA SUMU MBALIMBALI MWILINI Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku. Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali. Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako. Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi: -Uchovu sugu -Maumivu ya maungio -Msongamano puani -Kuumwa kichwa kila mara -Tumbo kujaa gesi -Kufunga choo au kupata choo kigumu -Kukosa utulivu -Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi -Pumzi mbaya -Mzunguko wa hedhi usio sawa -Kuishiwa nguvu -Kushindwa kupungua uzito -Kupenda kula kula kila mara Njia 16 za kuondoa sumu mbalimbali mwilini 1. Fanya mlo wako mmoja wa siku kuwa ni matunda pekee Amua moja ya mlo wako kw...

MH.LOWASSA AWASILI MAKAO MAKUU YA POLISI LEO DAR KWA MAHOJIANO

Image
WAZIRI Mkuu Mstaafu na mgombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, amewasili katika Makao Makuu ya Polisi jijini Dar saa nne kama alivyotakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI). Lowassa alikuwa amefuatana na magari manne ya msafara wake pamoja na magari mawili ya polisi wenye siraha. Kabla ya kuwasili kwa Lowassa, aliyetangulia mapema leo alikuwa katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Mashinji aliyewasili kuhakikisha anaweka sawa maswala ya kisheria na msaada wowote utakaohitajika. Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kusogea eneo la tukio kwani ulinzi umeimalishwa. Jana Edward Lowassa alipokea wito wa kumtaka aonane na DCI leo saa nne bila kukosa.