Taiwan: Wabunge Wavurugana Bungeni, Wachapana Live
WABUNGE wa Taiwan leo walichapana makonde, wakarushiana viti na mabaluni ya maji baada ya kutofautiana kuhusu mradi mmoja wa miundombinu. Tukio
hilo ni mwendelezo wa matukio yaliyoanza jana ambapo katika kubishana,
wabunge hao walikwidana mashati na kuchapana wakati wa kupitia bajeti ya
mradi huo.
Mpango huo
ni moja ya miradi mikubwa iliyopendekezwa na Rais Tsai Ing-wen ambayo
inajumuisha ujenzi wa reli za kutoa huduma ndogondogo, hatua za
kuthibiti mafuriko na mazingira yanayosababishwa na viwanda.
Hata
hivyo, chama cha upinzani cha Kuomintang kinapinga mradi huo kikisema
unapendelea miji na wilaya ambazo zinaunga mkono chama cha Democratic
Progressive (DPP) ambako kina uhakika wa kuungwa mkono katika uchaguzi
wa mikoa mwaka kesho. Isitoshe, wapinzani wanapinga kiasi kikubwa mno
cha Dola bilioni 13.8 ambazo zitatumika katika mradi huo.
Waziri
Mkuu Lin Chuan alishindwa kutoa ripoti ya bajeti hiyo Alhamisi baada
kutupiwa baluni la maji na kumfanya aondoke bungeni ambalo
liliahirishwa. Leo, Lin aliingia tena bungeni lakini akiwa bado hajasema
chochote vurugu ziliibuka.
Wapinzani
waliinua viti juu na kulizunguka jukwaa la kutolea hotuba huku
wakishikana mashati na mahasimu wenzao na hivyo kumfanya Lin ashindwe
kusema chochote ambapo mabaluni ya maji yalikuwa yakitupwa kuelekea eneo
hilo.
Comments
Post a Comment