Abdi Banda ameaga rasmi Simba

BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Hassan Banda amefikia makubaliano na klabu ya Baroka F.C ya Afrika Kusini kusaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga nayo.
Baada ya kung’ara katika michuano ya Kombe la COSAFA Castle nchini Afrika Kusini akiiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tatu, mchezaji huyo wa Simba ya nyumbani, Tanzania sasa anakaribia kwenda kuanza maisha mapya timu hiyo ya Ga-Mphahlele, karibu na Polokwane, Limpopo ambayo inacheza Ligi Kuu ya nchini humo.
Banda amesema anaondoka Simba SC aliyoichezea kwa miaka miwili, baada ya kumaliza mkataba wake na hakuwahi kusaini mkataba mpya, hivyo anajiunga na Baroka kama mchezani huru.
“Nipo njiani narudi nyumbani kwa ajili ya kuja kuchukua vitu na kurudi rasmi Afrika Kusini kuanza maisha mapya na klabu yangu mpya ya Baroka,”amesema Banda akizungumza kwa simu leo.
Banda alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza michuano ya COSAFA Castle na kutwaa Medali ya Shaba baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Lesotho kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 usiku wa jana Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg.

Comments

Popular posts from this blog