Posts

FAROE, KISIWA CHENYE UHABA WA WANAWAKE

Image
Kuna upungufu wa wanawake katika kisiwa cha Faroe. Hivyobasi wanaume katika kisiwa hicho wanatafuta wanawake kutoka maeneo mengine kama vile mataifa ya Thailand na Ufilipino. Lakini je ni changamoto gani zinazowakumba wanawake wanaoelekea katika kisiwa hicho. Wakati Athaya Slaetalid alipoelekea katika kisiwa hicho ambapo kipindi cha majira ya baradi huchukua muda wa miezi sita alikuwa akikaa karibu na kikanza ama heater kwa jina la Kiingereza kwa siku nzima. ''Watu walikuwa wakiniambie niende nje kwa sababu kuna jua lakini nilisema'': ''Hapana niwacheni, nahisi baridi sana''. Kuhamia katika kisiwa hicho miezi sita iliopita ilikuwa vigumu kwa Bi Athaya aliyekiri. Alikutana na mumewe Jan alipokuwa akifanya kazi na rafikiye mmoja wa kisiwa hicho ambaye alikuwa ameanza biashara nchini Thailand. Jan alijua mapema kwamba kumpeleka mkewe katika utamaduni huo, hali ya hewa itakuwa changamoto kubwa. "Nilikuwa na wasiwasi kwa sababu kil

PICHA: MVUA KUBWA ILIVYOPOROMOA MIAMBA LUSHOTO LEO

Image
Taarifa tulizozipata kutoka wilani Lushoto kutoka kwa mashuhuda wa matukio hayo zinasema mvua kubwa zinaendelea kunyesha nnchi zimeendelea kuketa madhara kwa wakazi wa wilaya hiyo ya mkoa wa Tanga. Tunaambiwa kuwa njia ya mombo Lushoto haipitiki, na kwamba  magari yameangukiwa na miamba ya mawe iliyoporomoka barabarani.. Ujumbe unaandikwa 'Naombeni kila mtu na kwa imani yake tuwaombee dua  ndugu zangu waliopo wilaya ya Lushoto  MUNGU awanusuru na mvua kubwa inayoendelea kunyesha usiku na mchana ,njia ya mombo Lushoto  haipitikia magari  yameangukiwa na ngema zenye mawe makubwa na inasemekana kuna waliopoteza maisha !!'

RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA AWASILI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFIULI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wa Nyimbo za Mataifa mawili (Tanzania & Afrika Kusini) zikipigwa katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipita kukagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikitumbuiza ndani ya viwanja vya Ikulu kwa Heshima ya ugeni huo wa Rais wa Afrika Kusini. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza mazungumzo yao Rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa T

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA MGENI WAKE RAIS WA AFRIKA KUSINI,JACOB ZUMA LEO JIJINI DAR

Image
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma pamoja na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu na wananchi waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017. Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma akimueleza jambo mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa sambamba na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma mapema leomara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017. Rais Dkt Magufuli akimsikiliza Makamua wa Rais,Samia Suluhu Hassan wakati wa mapokezi ya Rais wa Afrika Kusini,Jacob Zuma mapema leo kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini,Jacob Zuma akisalimiana na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassani mapema leo kwenye viwanja vya Ikulu,jijini Dar,kushoto ni Rais Dkt John Pombe Magufuli akishuhu

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BNGENI MJINI DODODA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe, bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017 .   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo Bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Nkasi, Ally Bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017.   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Rombo Roman Joseph Selasini, kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 11, 2017, katikati ni Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Francis Mbatia, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mama Lulu Aitolea Povu Zito Ndoa Ya Mwanae

Image
Staa wa sinema za Kibongo, Elizebeth Michael ‘Lulu’. STORI: BRIGHTON MASALU | AMANI | HABARI DAR ES SALAAM: Wakati kukiwa na madai ya kufanyika kwa vikao vya mwishomwisho vya harusi ya staa wa sinema za Kibongo, Elizebeth Michael ‘Lulu’, mama mzazi wa mrembo huyo, Lucresia Karugila ameitolea povu. Mama Lulu aliliambia gazeti hili kuwa, hataki ujinga wa kuulizwaulizwa juu ya harusi hiyo badala yake aachwe ili apumzike nakufanya mambo ya msingi. Mama mzazi wa mrembo huyo, Lucresia Karugila. Hayo yalikuja kufuatia swali alilotwangwa na mwandishi wetu aliyetaka kujua juu ya maendeleo ya vikao vya harusi yamwanaye na mmiliki mmoja wa kituo cha redio na televisheni ambapo badala ya kutoa ufafanuzi, alianza kumshambulia mwandishi wetu kwa maneno makali. Mama Lulu alisema hataki kabisa kusikia jambo la ndoa wala mapenzi ya Lulu, kwani hakuna uhalali wala uthibitisho wa wazi alioupokea juu ya suala hilo, hivyo kumuuliza nini kinaendelea ni sawa na kumuingiza kweny

Man United watambulisha uzi mpya kwaajili ya msimu ujao

Image
 Manchester United mapemaa imeamua kuuweka hadharani uzi wake mpya wa msimu wa 2017/18. Uzi huo unaonekana kurudisha kumbukumbu ya Man United kuhusiana na jezi za enzo hizoo wakati wa kipindi cha Alex Ferguson na wachezaji kama Ryan Giggs walikuwa wakichipukia.

SABABU ZA SHILOLE KUKACHA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI KWA DENTI WA CHUO

Image
Msanii wa muziki wa kizazi wa Bongo Fleva na filamu, nchini Zuwena Mohamed maarufu kama  Shilole ameshindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi ya matumizi mabaya ya mtandao kwa kuwa anaumwa. Leo (Jumatano) Shilole alipaswa kutoa ushahidi katika kesi hiyo inayomkabili mwanafunzi wa Chuo cha Bandari, Thomas Lucas (20) inayosikilizwa mbele ya Hakimu Boniface Lyamwike. Katika kesi hiyo, Lucas anakabiliwa na shtaka la mtandao kwa kumkashfu Shilole kupitia kwenye mtandao wa Instagram. Inadaiwa  kuwa mshtakiwa huyo alifanya hivyo wakati akijiua ni kosa na kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya mtandao namba 14 ya 2016.  Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17,2017 ambapo itaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Nandy: Wanaume wananisumbua sana

Image
MWANADADA anayefanya poa na ngoma yake ya One Day, Faustina Charles ‘Nandy’ amekiri kuwa anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume wakware ambao wanahitaji penzi lake, lakini bila mafanikio. Akipiga stori na Za Motomoto News, Nandy alifunguka kuwa amekuwa akikumbana na vishawishi mbalimbali kwa ahadi kedekede ili tu waweze kutimiza azma yao lakini anajitahidi kupambana na hali hiyo sababu ameshajifunza kupitia kwa wenzake. “Usumbufu ni mkubwa mno kwa kweli, lakini siwezi kuwataja majina hata hao vigogo wanaonisumbua, mimi ni msichana ninayejielewa na wanaume wengi wamekuwa wakihaha kutaka kuonja penzi langu, wanagonga mwamba,” alisema.

Maalim Seif Aibukia Kanisani Kwa Askofu Gwajima

Image
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hammad (kushoto) akiwa na  Mchungaji wa Kanisa la Ufufuno na Uzima, Askofu Josephat Gwajima. LEO Mei 10, 2017, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hammad amekwenda kumtembelea Mchungaji wa Kanisa la Ufufuno na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, kanisani kwake Ubungo, Dar es Salaam. Akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo ya faragha na Maalim Seif, Askofu Gwajima amesema ujio wa kiongozi huyo kanisani hapo ulikuwa ni kwa ajili ya kubadilishana mambo mbalimbali kuhusu nchi na mahusiano yao. “Maalim Seif ni rafiki yangu, ni siku nyingi tulikuwa hatujaonana, tumezungumzia mambo ya nchi mbalimbali na mahusiano yangu mimi na yeye. “Unaweza kuwa na rafiki ambaye anafanya kazi tofauti na yako, anaweza kuwa daktari na wewe ukawa siyo daktari, hata serikali haikatazi urafiki. “Nimemuuliza ni kipi kimempata Profesa (Lipumba) mpaka anavuruga chama chake, amenielezea ili na mim