FAROE, KISIWA CHENYE UHABA WA WANAWAKE
Kuna
upungufu wa wanawake katika kisiwa cha Faroe. Hivyobasi wanaume katika
kisiwa hicho wanatafuta wanawake kutoka maeneo mengine kama vile mataifa
ya Thailand na Ufilipino.Lakini je ni changamoto gani zinazowakumba wanawake wanaoelekea katika kisiwa hicho.Wakati
Athaya Slaetalid alipoelekea katika kisiwa hicho ambapo kipindi cha
majira ya baradi huchukua muda wa miezi sita alikuwa akikaa karibu na
kikanza ama heater kwa jina la Kiingereza kwa siku nzima.''Watu walikuwa wakiniambie niende nje kwa sababu kuna jua lakini nilisema'': ''Hapana niwacheni, nahisi baridi sana''.
Kuhamia katika kisiwa hicho miezi sita iliopita ilikuwa vigumu kwa Bi Athaya aliyekiri.
Alikutana
na mumewe Jan alipokuwa akifanya kazi na rafikiye mmoja wa kisiwa hicho
ambaye alikuwa ameanza biashara nchini Thailand.
Jan alijua mapema kwamba kumpeleka mkewe katika utamaduni huo, hali ya hewa itakuwa changamoto kubwa.
"Nilikuwa
na wasiwasi kwa sababu kila kitu alichokiwacha nchini Thailand kilikuwa
tofauti na kile alichokuja kuona katika kisiwa cha Faroe'', alisema.
''Lakini kwa sababu namjua Athaya nilijua ataingiliana na hali ya hewa''.
Kufikia sasa kuna takriban wanawake 300 kutoka Thailand na Ufilipino wanaoishi katika kisiwa cha Faroe.
Haionekani
kuwa idadi kubwa lakini kisiwa hicho chenye idadi ya watu 50,000 sasa
wanawakilisha watu walio wachache katika visiwa hivyo 18 kati ya Norway
na Iceland.
Katika
miaka ya hivi karibuni visiwa vya Faroe vimepata upungugufu wa wa idadi
ya watu huku vijana wakiondoka ili kutafuta elimu na huwa hawarudi.
Kulingana
na waziri mkuu Axel Johannese, kisiwa hicho kina upungufu wa jinsia
huku kukiwa na uchache wa takriban wanawake 2000 ikilinganishwa na
wanaume.
Hatua hiyo imewafanya wanaume katika kisiwa hicho kutafuta wanawake katika maeneo mengine kwa mapenzi.
Wengi
ijapokuwa sio wote wa wanawake hao wa bara Asia, walikutana na wanaume
zao kupitia mtandaoni wengine kupitia mitandao ya kukutanisha
wapendanao.
Wengine wamepatana kupitia mitandao ya wanandoa wa Asia na visiwa vya Faroe.
Kwa wale wanaowasili, utamaduni wa eneo hilo unaweza kuwaathiri.
Vikiwa ni miliki za Denmark, visiwa vya Faroe vina lugha yao na utamaduni wa kipekee hususan katika maswala ya chakula.
Comments
Post a Comment