Posts

Breaking News: Roma apatikana, yupo kituo cha Polisi Oysterbay

Image
  Msanii Roma Mkatoliki anadaiwa kupatikana na yupo Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar . Habari ya akina Roma kupatikana imethibitishwa na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Mada. Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia. Kwa sasa wanadaiwa kuwepo kituoni hapo kwa taratibu za kipolisi kwa kuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo. Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii. Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake. Taarifa zaidi zinafuata..

Sababu za Faru Fausta kutumia Sh760 milioni kwa mwaka zatajwa

Image
Arusha. Hakuna bosi yeyote serikalini anayelipwa zaidi ya Sh17 milioni baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kutekeleza sera zake za kubana matumizi, lakini yupo kiumbe hai mmoja tu ambaye matumizi yake yalifika Sh64 milioni kwa mwezi; na kuna sababu za kuhalalisha gharama hizo. Kiumbe huyo ni mnyama mwitu aina ya faru aliyepewa jina la Fausta, ambaye sasa anatumia Sh20.4 milioni. Fausta ndiye faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia. Fausta anaishi Hifadhi ya Ngorongoro ambako analindwa kwa saa 24 kumuepusha kushambuliwa na wanyama wengine kama fisi na mbwa mwitu kutokana na uzee, lakini gharama za ulinzi zitapungua baada ya kupata makazi salama ndani ya mwitu jengo lake litakapomalizika. Hiyo ni sehemu tu ya gharama zinazomfanya Fausta kutumia fedha nyingi zaidi ya mfanyakazi mwandamizi wa serikalini. Kazi ipo kwe

SUPERSTAA DIAMOND PLATNUMZ ATOA SABABU YA KUACHIA NYIMBO YAKE MPYA "ACHA NIKAE KIMYA

Image
Diamond Platnumz ameachia wimbo wake mpya kwa kushtukiza uitwao ‘Acha Nikae Kimya.’ Wimbo unazungumzia masuala mengi yanayotokea sasa ikiwemo hofu iliyotanda baada ya Roma na wenzie kutekwa. Wimbo huo hata hivyo umepokelewa kwa hisia tofauti. Hizi ni sababu zake kwanini ameamua kuuachia: Ili Nchi ipate maendeleo inahitaji Upendo na Ushirikiano wa Wananchi na Serikali..Na Nikiwa kama Msanii, jukumu langu ni kuhakikisha natumia Hekma na busara kukemea jambo nilionalo haliko sawa ili lirekebishwe, lakini pia panapokuwa hakuna maelewano jukumu langu pia ni kupatanisha ili kwa pamoja tujenge nchi yetu kusudi wazazi wetu, watoto pamoja na familia zetu waishi kwa Upendo Amani na kufurahia nchi yetu…Na ndiomaana kwenye nyimbo nakwambia “MI NA WEWE WA TAIFA MOJA…KAMBARAGE BABA MMOJA….SASA TOFAUTI ZA NINI TUSHIKAMANE TUKAIJENGE TANZANIA”… Unatakiwa utambue kuwa kila kiongozi ni Binadamu na kama wote tujuavyo, Binadamu hatujakamilika… hivyo katika nch

Bashe: ‘Uchunguzi makontena ya mchanga uoneshwe kwenye TV’

Image
MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe(CCM), ameiomba Kamati iliyoundwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kuchunguza makontena ya mchanga katika Bandari ya Dar es Salaam, kurekori kilichomo katika makontena hayo ili yaoneshwe kwenye televisheni kwa lengo la kuwaondoa hofu Watanzania. Ombi hilo limekuja siku chache baada ya Rais Magufuli kuunda Kamati kwa ajili ya kuchunguza makontena ya mchanga katika Bandari ya Dar esSalaam. Alitoa ombi hilo bungeni mjini hapa wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi yaWaziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018. Alisema wengi wanaamini kwamba yale makontena yaliyokamatwa bandarini yana dhahabu. “Spika kule kwangu Nzega wanaamini yale makontena yaliyopo bandarini yana dhahabu,tunaomba mrekodi hili tukio la uchunguzi halafu mtuoneshe kwenye TV tuone kilichomo ndani ya zile kontena,” alisema. Alisema yeye ni miongoni mwa watu amba

Mdee: Niliwahi Dodoma kuepuka kukomolewa

Image
Dar es Salaam. Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amesema aliamua kuwahi Dodoma kuepuka kukomolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyeagiza afike mbele ya Kamati ya Maadili jana asubuhi na kuagiza polisi wamsake popote alipo, ikiwezekana apelekwe akiwa amefungwa pingu. Mdee, ambaye alikuwa Dar es Salaam wakati amri hiyo ikitolewa juzi saa 5:00 asubuhi, aliwasili Dodoma jana, lakini suala lake litajadiliwa leo. “Spika ana mamlaka ya kisheria ya kuomba vyombo vingine vya dola kumsaidia kumkamata mtu,” alisema Mdee alipoongea na Mwananchi jana. “Kwa sababu hiyo, ana uwezo wa kutumia mamlaka hayo kumkomoa mtu. Ndiyo maana nikaja mwenyewe Dodoma. Niliacha majukumu mazito niliyokuwa nayo ili lengo lake la kunikomesha lisifanikiwe,” alisema. Spika Ndugai, aliyezungumza kwa ukali, alisema anajua kuwa Mdee alikuwa nje ya Dodoma, lakini akataka awe amefika mbele ya kamati hiyo jana muda sawa na ule aliokuwa akitoa maagizo hayo juzi. Mdee anatuhumiwa kutoa lugha

Taarifa mpya ya Wizara ya Habari na sanaa kuhusu Roma kutoweka

Image
Taarifa za kupotea kwa Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wawili baada ya kutekwa na kuchukuliwa na Watu wasiojulikana kwenye studio za TONGWE Dar es salaam, zilianza kusambaa kuanzia juzi usiku (April 5 2017) Leo April 7 2017 Wizara ya Sanaa, Utamaduni na michezo ambayo iko chini ya Dr. Mwakyembe imetoa taarifa ifuatayo >>>> “kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa Wizara imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki”” Wizara imefuatilia kwa karibu suala hili kwa kuwa lina muelekeo wa jinai. Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi. Kutokana na hali hiyo, Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.

PICHA: Maiti Yaokotwa Ufukweni Ikiwa Imefungwa Kwenye Baiskeli

Image
Tukio la kusikitisha Wakati familia kadhaa za watanzania zikiendelea kupoteza ndugu zao bila kujulikana walipo, leo huko mkoani Mara katika ufukwe wa ziwa Victoria imeokotwa maiti ya mtu mmoja asiyefahamika ikiwa imetupwa ziwani. Mazingira ya kifo chake yanaonesha mtu huyo mwanaume aliuawa, akafungwa kama kifurushi kwenye baiskeli, kisha yeye na baiskeli yake wakatoswa ziwani. source:Muungwana

Umati Wamyoshea Mabango Waziri wa sanaa kuhusu Roma Mkatoliki

Image
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo kile kipindi cha XXL kilichokuwa kinaruka moja kwa moja toka Dodoma kimegeuka majonzi baada ya mamia ya vijana kunyoosha mabango yaliyoandika FREE ROMA. Watanganzaji walilazimika kubadili interview na kumwambia naibu waziri habari utamaduni na michezo Antony Mavunde kwamba hawawezi kupuuzia mabango waziri aseme chochote. Naibu waziri akasema anasikitishwa na kitendo hicho lakini ana taarifa kwamba jeshi la polisi litatoa taarifa punde. Baada ya hapo kwenye segment ya hot 3 at 3 zimepigwa nyimbo mbili za ROMA ambapo umati umepagawa na kupiga mayowe.

MAMA KANUMBA NA MRITHI WA KANUMBA KIMENUKA TENA

Image
Mama Kanumba (Flora Mtegoa) na Fredy Swai.   SIKU chache baada ya mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kumtambulisha mrithi wa mwanaye kuwa ni Fredy Swai, wametibuana na sasa kila mmoja yuko kivyake chanzo kikidaiwa kuwa ni masuala ya fedha. Chanzo kilicho karibu na wawili hao kilimwaga ubuyu kuwa, hali ya kutibuana ilikuja baada ya mama Kanumba kutumia jina la kijana huyo katika kutafutia pesa kwa madai kuwa wanataka kuandaa fi lamu na mchezo uliposhtukiwa, Fredy akamaindi na kununa. Baada ya kupata ubuyu huo gazeti hili lilimtafuta mama Kanumba aliyekuwa na haya ya kusema: “Nadhani mimi sina bahati, huwa nawapokea watu kwa moyo wote kisha wananiona sifai, huyu kijana huenda utoto unamsumbua.” Kwa upande wake Fredy alisema: “Kuna mambo madogo tumekwazana lakini sipo tayari kuyaongelea kwa sasa, namheshimu mama Kanumba kama mzazi wangu.”

MISS TANZANIA 2014 AZAA NA KIGOGO HUYU

Image
Nicole Sarakikya. DAR ES SALAAM: Imevuja! Mbunge wa jimbo moja lililopo katikati ya nchi ya Tanzania akikiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) anadaiwa kuzaa na Miss Shinyanga, 2014  aliyeingia Top 5 ya Miss Tanzania mwaka huo ambaye pia ni Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Nicole Sarakikya (pichani) ikiwemo na kumpangishia chumba maeneo ya Salasala jijini hapa. MADAI MEZANI Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na wawili hao, imeshangaza wengi mbuge huyo kuzaa na mlimbwende  wakati huo yeye ana familia yake yenye mke na watoto watatu. “Hivi jamani OFM wako wapi siku hizi? Mbona kuna mambo yanaendelea na hamyafichui? Kwa mfano, mbunge wa… (anataja jimbo na jina) amezaa na Miss Shinyanga mwaka 2014, Nicole ambaye kampangishia nyumba maeneo ya Salasala, wakati mimi ninavyofahamu jamaa ana mke na watoto watatu. Kama siyo kuitesa familia yake ni nini?” alihoji mtoa taarifa wetu. Amani: Amezaa lini? Huyo mtoto ana umri gani kwa sasa? Chanzo: Ni miezi mitatu nadh

Maneno matatu ya Nape Nnauye kuhusu Roma

Image
 Baada ya mastaa mbalimbali kuguswa juu ya stori ya Roma mkatoliki na wenzake watatu kuchukuliwa na watu wasiofahamika kwenye Studio za Tongwe Records na kupelekwa sehemu isiyojulikana, sasa leo April 7 2017 Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Moses Nnauye ameonesha hisia zake juu ya tukio hilo. Kupitia account yake ya twitter Nape Nnauye ameyaandika maneno haya matatu kuhusu Roma…>>>”Roma! Oooooh No!” – Nape Nnauye.

Mbunge Hussein Bashe aandika haya kuhusu Roma Mkatoliki

Image
 Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatolikia zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuripotiwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana. Watu mbalimbali ikiwemo wasanii mbalimbali wamekuwa wakionesha hisia zao juu ya tukio hilo kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuoneshwa kuguswa na tukio hilo, mbunge wa Nzega Hussein Bashe ni miongoni mwa watu waliyotumia kuraza zao za instagram kuandika anachowaza kuhusu Roma. Who is behind all this? “Ni genge ambalo limejipa mamlaka ya kupandikiza woga na chuki miongoni mwa jamii na kuharibu Taswira ya CCM. Tunawajibu wa kukataa woga ,Tunawajibu wa kutoruhusu Misuse ya vyombo vya Ulinzi na usalama, Tunawajibu wa kulinda Taifa letu” “Tunawajibu wa kupigania Values zilizopiganiwa na waasisi wa Taifa letu kama Mzee Karume na Mwl Nyerere, Tunawajibu wa kukataa ukandamizaji

BREAKING NEWS:WATU WANNE WAFUKIWA NA KIFUSI DAR NA MMOJA AFARIKI DUNIA

Image
Watu wanne wameripotiwa kufukiwa na kifusi  katika machimbo ya kokoto, Golani yaliyopo eneo la Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. DC wa Ilala, Sophia Mjema akizungumza na wanahabari eneo la tukio. Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana Alhamisi majira ya saa 8 mchana ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa vyombo vya uokoaji vimefanikiwa kupata watu wawili ambapo mmoja alikuwa tayari amekwishafariki dunia. Mjema ameeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na mtu wa pili  aliyeokolewa akiwa hai alikuwa amevunjika mguu ambaye pia amepelekwa Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa. Aidha DC Mjema ameeleza kuwa, wawili waliobakia hawajafanikiwa kuokolewa kutokana na changamoto ya mvua nyingi zinazoendelea kunyesha pamoja na ubovu wa miundombinu ya njia za kupitishia mitambo ya uokoaji. Eneo la machimbo hayo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salumu Hamdun