PICHA: Maiti Yaokotwa Ufukweni Ikiwa Imefungwa Kwenye Baiskeli
Tukio la kusikitisha Wakati familia kadhaa za watanzania zikiendelea
kupoteza ndugu zao bila kujulikana walipo, leo huko mkoani Mara katika
ufukwe wa ziwa Victoria imeokotwa maiti ya mtu mmoja asiyefahamika ikiwa
imetupwa ziwani. Mazingira ya kifo chake yanaonesha mtu huyo mwanaume
aliuawa, akafungwa kama kifurushi kwenye baiskeli, kisha yeye na
baiskeli yake wakatoswa ziwani.
source:Muungwana
Comments
Post a Comment