MAMA KANUMBA NA MRITHI WA KANUMBA KIMENUKA TENA

Mama Kanumba (Flora Mtegoa) na Fredy Swai.
SIKU
chache baada ya mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa
kumtambulisha mrithi wa mwanaye kuwa ni Fredy Swai, wametibuana na sasa
kila mmoja yuko kivyake chanzo kikidaiwa kuwa ni masuala ya fedha.
Chanzo kilicho karibu na
wawili hao kilimwaga ubuyu kuwa, hali ya kutibuana ilikuja baada ya mama
Kanumba kutumia jina la kijana huyo katika kutafutia pesa kwa madai
kuwa wanataka kuandaa fi lamu na mchezo uliposhtukiwa, Fredy akamaindi na
kununa.
Baada ya kupata ubuyu huo gazeti hili lilimtafuta mama Kanumba aliyekuwa na haya ya kusema:
“Nadhani mimi sina bahati, huwa nawapokea watu kwa moyo wote kisha
wananiona sifai, huyu kijana huenda utoto unamsumbua.” Kwa upande wake
Fredy alisema:
“Kuna mambo madogo tumekwazana lakini sipo tayari kuyaongelea kwa sasa, namheshimu mama Kanumba kama mzazi wangu.”
Comments
Post a Comment