Posts

Taarifa mpya ya Wizara ya Habari na sanaa kuhusu Roma kutoweka

Image
Taarifa za kupotea kwa Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wawili baada ya kutekwa na kuchukuliwa na Watu wasiojulikana kwenye studio za TONGWE Dar es salaam, zilianza kusambaa kuanzia juzi usiku (April 5 2017) Leo April 7 2017 Wizara ya Sanaa, Utamaduni na michezo ambayo iko chini ya Dr. Mwakyembe imetoa taarifa ifuatayo >>>> “kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa Wizara imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma Mkatoliki”” Wizara imefuatilia kwa karibu suala hili kwa kuwa lina muelekeo wa jinai. Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi. Kutokana na hali hiyo, Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.

PICHA: Maiti Yaokotwa Ufukweni Ikiwa Imefungwa Kwenye Baiskeli

Image
Tukio la kusikitisha Wakati familia kadhaa za watanzania zikiendelea kupoteza ndugu zao bila kujulikana walipo, leo huko mkoani Mara katika ufukwe wa ziwa Victoria imeokotwa maiti ya mtu mmoja asiyefahamika ikiwa imetupwa ziwani. Mazingira ya kifo chake yanaonesha mtu huyo mwanaume aliuawa, akafungwa kama kifurushi kwenye baiskeli, kisha yeye na baiskeli yake wakatoswa ziwani. source:Muungwana

Umati Wamyoshea Mabango Waziri wa sanaa kuhusu Roma Mkatoliki

Image
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo kile kipindi cha XXL kilichokuwa kinaruka moja kwa moja toka Dodoma kimegeuka majonzi baada ya mamia ya vijana kunyoosha mabango yaliyoandika FREE ROMA. Watanganzaji walilazimika kubadili interview na kumwambia naibu waziri habari utamaduni na michezo Antony Mavunde kwamba hawawezi kupuuzia mabango waziri aseme chochote. Naibu waziri akasema anasikitishwa na kitendo hicho lakini ana taarifa kwamba jeshi la polisi litatoa taarifa punde. Baada ya hapo kwenye segment ya hot 3 at 3 zimepigwa nyimbo mbili za ROMA ambapo umati umepagawa na kupiga mayowe.

MAMA KANUMBA NA MRITHI WA KANUMBA KIMENUKA TENA

Image
Mama Kanumba (Flora Mtegoa) na Fredy Swai.   SIKU chache baada ya mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa kumtambulisha mrithi wa mwanaye kuwa ni Fredy Swai, wametibuana na sasa kila mmoja yuko kivyake chanzo kikidaiwa kuwa ni masuala ya fedha. Chanzo kilicho karibu na wawili hao kilimwaga ubuyu kuwa, hali ya kutibuana ilikuja baada ya mama Kanumba kutumia jina la kijana huyo katika kutafutia pesa kwa madai kuwa wanataka kuandaa fi lamu na mchezo uliposhtukiwa, Fredy akamaindi na kununa. Baada ya kupata ubuyu huo gazeti hili lilimtafuta mama Kanumba aliyekuwa na haya ya kusema: “Nadhani mimi sina bahati, huwa nawapokea watu kwa moyo wote kisha wananiona sifai, huyu kijana huenda utoto unamsumbua.” Kwa upande wake Fredy alisema: “Kuna mambo madogo tumekwazana lakini sipo tayari kuyaongelea kwa sasa, namheshimu mama Kanumba kama mzazi wangu.”

MISS TANZANIA 2014 AZAA NA KIGOGO HUYU

Image
Nicole Sarakikya. DAR ES SALAAM: Imevuja! Mbunge wa jimbo moja lililopo katikati ya nchi ya Tanzania akikiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) anadaiwa kuzaa na Miss Shinyanga, 2014  aliyeingia Top 5 ya Miss Tanzania mwaka huo ambaye pia ni Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Nicole Sarakikya (pichani) ikiwemo na kumpangishia chumba maeneo ya Salasala jijini hapa. MADAI MEZANI Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na wawili hao, imeshangaza wengi mbuge huyo kuzaa na mlimbwende  wakati huo yeye ana familia yake yenye mke na watoto watatu. “Hivi jamani OFM wako wapi siku hizi? Mbona kuna mambo yanaendelea na hamyafichui? Kwa mfano, mbunge wa… (anataja jimbo na jina) amezaa na Miss Shinyanga mwaka 2014, Nicole ambaye kampangishia nyumba maeneo ya Salasala, wakati mimi ninavyofahamu jamaa ana mke na watoto watatu. Kama siyo kuitesa familia yake ni nini?” alihoji mtoa taarifa wetu. Amani: Amezaa lini? Huyo mtoto ana umri gani kwa sasa? Chanzo: Ni miezi mi...

Maneno matatu ya Nape Nnauye kuhusu Roma

Image
 Baada ya mastaa mbalimbali kuguswa juu ya stori ya Roma mkatoliki na wenzake watatu kuchukuliwa na watu wasiofahamika kwenye Studio za Tongwe Records na kupelekwa sehemu isiyojulikana, sasa leo April 7 2017 Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Moses Nnauye ameonesha hisia zake juu ya tukio hilo. Kupitia account yake ya twitter Nape Nnauye ameyaandika maneno haya matatu kuhusu Roma…>>>”Roma! Oooooh No!” – Nape Nnauye.

Mbunge Hussein Bashe aandika haya kuhusu Roma Mkatoliki

Image
 Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatolikia zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuripotiwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana. Watu mbalimbali ikiwemo wasanii mbalimbali wamekuwa wakionesha hisia zao juu ya tukio hilo kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuoneshwa kuguswa na tukio hilo, mbunge wa Nzega Hussein Bashe ni miongoni mwa watu waliyotumia kuraza zao za instagram kuandika anachowaza kuhusu Roma. Who is behind all this? “Ni genge ambalo limejipa mamlaka ya kupandikiza woga na chuki miongoni mwa jamii na kuharibu Taswira ya CCM. Tunawajibu wa kukataa woga ,Tunawajibu wa kutoruhusu Misuse ya vyombo vya Ulinzi na usalama, Tunawajibu wa kulinda Taifa letu” “Tunawajibu wa kupigania Values zilizopiganiwa na waasisi wa Taifa letu kama Mzee Karume na Mwl Nyerere, Tunawajibu wa kukataa ukandamiz...

BREAKING NEWS:WATU WANNE WAFUKIWA NA KIFUSI DAR NA MMOJA AFARIKI DUNIA

Image
Watu wanne wameripotiwa kufukiwa na kifusi  katika machimbo ya kokoto, Golani yaliyopo eneo la Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. DC wa Ilala, Sophia Mjema akizungumza na wanahabari eneo la tukio. Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana Alhamisi majira ya saa 8 mchana ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa vyombo vya uokoaji vimefanikiwa kupata watu wawili ambapo mmoja alikuwa tayari amekwishafariki dunia. Mjema ameeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na mtu wa pili  aliyeokolewa akiwa hai alikuwa amevunjika mguu ambaye pia amepelekwa Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa. Aidha DC Mjema ameeleza kuwa, wawili waliobakia hawajafanikiwa kuokolewa kutokana na changamoto ya mvua nyingi zinazoendelea kunyesha pamoja na ubovu wa miundombinu ya njia za kupitishia mitambo ya uokoaji. Eneo la machimbo hayo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala,...

Hiki ndicho kilichofanya TID amuite Jide 'genious'

Image
Mbongo fleva ambaye amegoma kuitwa jina la TID na kupendekeza aitwe 'Mnyama' amekiri hewani kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa mkongwe wa muziki Bongo Lady Jadee ni 'genious' kwa kitendo cha kuwa na albam yenye jina kama la albam yake. Akiwa anaachia ngoma yake impya yenye jina la 'Woman' TID amesema wimbo wake huo aliutengeneza tangu mwaka uliopita hivyo hakuwa anajua kama mwana dada huyo ana albam inayofanana na jina la track yake. "Jide is a woman but mimi ni mwanaume ninayeimba kuhusu mwanamke. Huwezi amini kama mimi albamu yangu pia inaitwa Woman na kama Jide albamu yake inaitwa woman jua mimi ni hatari sana. Sasa kama mimi nina uwezo wa kufikiria kama Lady Jaydee basi mimi nitakuwa genious kufikiria kama lady Jaydee si kitu cha kitoto" Alisema TID Katika hatua nyingine TID amesema video yake ya Woman ni kazi ambayo imekuja kufanya mapinduzi kwenye kazi zake zote kwa sababu imegharimu dolla 12,000 (zaidi ya shilin...

RAPA NAYA WA MITEGO NA ZITTO KABWE WAANDIKA UJUMBEE HUU BAADA YA ROMA KUKAMATWA

Image
Baada ya Mbunge wa Mikumi na staa Bongo Fleva  Joseph Haule  ‘Prof Jay’ kutoa taarifa kupitia account yake ya Instagram kuhusu kukamatwa kwa staa mwingine wa Hip Hop  Roma Mkatoliki  katika studio za  Tongwe Records  na watu wasiojulikana, taarifa hiyo imeamsha hisia za watu mbalimbali wakiwepo mastaa wa Bongo Fleva na wanasiasa. Leo April 6 2017 kupitia account zao za Instgram na Twitter Rapa  Nay wa Mitego  na Mbunge wa Kigoma Mjini  Zitto Kabwe  wameyaandika haya.. >>>” Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?!  Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo.”  – Nay wa Mitego. >>>”Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote.”  – Zitto Kabwe.

Nape kuwaeleza ukweli wapiga kura wake jumamosi hii

Image
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ametoa shukrani kwa wote waliomuunga mkono katika kusimamia haki huku akisema kuwa ataenda kuwaeleza wananchi wake ukweli wote. Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17,” ameandika Nape kupitia Twitter. Marchi 23, Rais Magufuli alimuondoa Nape kama Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo na nafasi hiyo kuchukuliwa na Dkt Harrison Mwakyembe aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria. 

Breaking News: Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande Afariki Dunia

Image
Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande afariki Dunia. Sir Andy amekuwa mwanachama wa Freemasons kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge. Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania). SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS ​ Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi. Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani. Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012. Siyo hiv...