Posts

VANESSA, DUMISHA HERI WAENDELEA KUSOTA POLISI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Image
Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni mbalimbali zilizofanyika na jeshi hilo kwa wiki moja leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha dawa za kulevya zilizokamatwa katika operesheni leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akinyesha gari lililokuwa linatumika kwa ajili ya utapeli na magari yaliyokamatwa kwa tuhuma mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha pikipiki zinazopita katika barabara ya mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha bunduki iliyoteleekezw

Je una herufi "M" katika kiganja chako? Hii ndio maana yake

Image
Watu wengi wanasema, mistari katika viganja vya kila binadamu vimebeba mambo mengi na maana nyingi kuhusu tabia yako na hatima yako kwa ujumla. Pia inasemekana watu wenye herufi  'M'  katika viganja vyao,ni watu wa aina muhimu sana.Inasemekana watu hawa wana sifa za ajabu.Wana ushirikiano mzuri na wafanyakazi katika aina yeyote ile ya biashara. Kama una mpenzi mwenye alama  'M'  katika kiganja chake,basi yakupasa kujua yupo makini katika uhusiano wenu.Hakuna utani,hakuna uongo na hakuna udanganyifu. Watu wenye herufi  'M'  katika viganja vyao, wana uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko katika maisha yao na daima utumia vizuri fursa wanazozipata katika maisha yao. Imekuwa ikijulikana kwa watu wa zamani, kwamba manabii wote walikuwa na alama hii katika mikono yao. Angalia mkoni wako na endapo ukijikuta una alama ya  'M'  basi tambua kwamba wewe ni mtu maalamu.

HIZI NDIO SENTENSI ZA MBUNGE LEMA KATIKA MKUTANO WAKE WA KWANZA ARUSHA

Image
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema leo amefanya mkutano wa hadhara ukiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu alipotoka mahabusu wiki moja iliyopita. Lema amefanya mkutano huo katika uwanja wa Shule ya Msingi Ngarenaro ili kuweza kuzungumza na wapiga kura wake kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo ya maendeleo katika jimbo hilo. Miongoni mwa mengi aliyoyazungumza, Godbless Lema amezungumzia kukamatwa kwake ambapo amesema kuwa amekaa mahabusu kwa miezi minne pasipo kuwa na kosa kabisa. Aidha, ameeleza kuwa mahabusu kuwa watu wengi ambao wapo kule kwa kusingiziwa wengine wamewekwa tu kwa uonevu na hawana kosa, hivyo kama kiongozi ataendelea kuwapigania huku akiwasihi wakazi wa Arusha kuwaombea waliopo mahabusu. Mbali na Lema, mwingine aliyepata nafasi ya kuzungumza na umati huo uliojitokeza leo ni mwanachama mpya wa chama hicho, muigizaji Wema Sepetu. Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa

HUU NDIO UJUMBEE ALIOANDAKA STAA WEMA SEPETU KABLA YA MKUTANO WA MBUNGE LEMA

Image
MSANII wa filamu na malkia wa mtandao nchini Wema Sepetu ‘Madam’,  amejikita zaidi katika siasa baada ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivi karibuni. Wema ameendelea kuzianika mitandaoni  baadhi ya harakati zake za kisiasa ikiwa ni pamoja na kujihusisha na shughuli za kijamii kama vile upandaji wa miti,  uliofanywa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na leo kabla ya Lema kuhutubia, ameweka picha na ujumbe mtandaoni unaowahamasisha watu kufika katika mkutano huo. “All Ready Kwa Ajili ya Mkutano wa Mhe. GodBless Lema… See you there…. Giving MY Chadema A New Look… Y’all Know Black And Khaki Be our Colour…. A lil White to add Flavor wont Hurt Nobody…. #CallMeKamanda cc @upendosimwita1 @ _ elm _ @blowassa”, alimaliza Wema. Share this

UN SECRETARY GENERAL STOPS IN DAR ON HIS WAY TO NEW YORK

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres (kushoto) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam jana. Mhe. Guterres alisimama kwa muda katika uwanja huo akitokea nchini Kenya kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Balozi Mahiga.  Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe Guterres aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa Mgogoro huo Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Benjamin Willium Mkapa. Aidha, Dkt. Mahiga aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.  Waziri Mahiga akizungumza jambo huku Mhe. Guterres akimsikiliza kwa makini.  Dkt. Mahiga akiendelea kuzungumza na Mhe. Guterres huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa S

KESI INAYOMKABILI MAXENCE MELO YAAHIRISHWA TENA HADI APRILI 3

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kesi namba 456 inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na mwenzake na Mwanahisa Mike Mushi isipoendelea itafutwa. Hayo yalisemwa alhamisi hii na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kukerwa na upande wa Jamhuri ambao ulishindwa kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali badala yake ukaomba kuahirisha kesi. Mwendesha Mashtaka, Inspekta Hamis Said, alidai mbele ya Hakimu Simba kwamba kesi ilitakiwa kuanza kusikilizwa awali lakini wakili anayeiendesha anaumwa. Mwendesha mashtaka aliomba kesi hiyo iahirishwe mpaka tarehe nyingine itakayopangwa. Hata hivyo Hakimu Simba alieleza kukerwa na tabia ya kesi kuahirishwa na kusema wakati mwingine kama kesi hiyo haitaendelea ataifuta. Aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 3, mwaka huu na dhamana ya washtakiwa inaendelea. By: Emmy Mwaipopo

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA.

Image
Picha namba 1-5. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo tarehe 9/03/2017. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU

SAIDA KAROLI ASIMULIA JINSI ALIVYOIBIWA KAZI ZAKE KISA KUTOJUA KUSOMA NA KUANDIKA

Image
Jana kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, mtangazaji Zamaradi alimuhoji mwimbaji wa muziki wa asili Saida Karoli ambapo alikiri kuwa hana haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa na Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na akadai zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye haki nazo .Kingine alichozungumza Saida ni kuhusu wimbo wa Salome ambao Diamond Platnumz aliurudia ambapo alisema ana hesabu kama alitoa bure kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea. ”Siwezi kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo, sina haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa bure”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja kweli, roho yangu moja  

Paul Makonda Aenda Mapumziko ya Miezi Miwili South Africa

Image
Wakati utata ikigubika kuhusu safari ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenda nchini Afrika Kusini, imebainika kuwa kiongozi huyo atakuwa likizo nchini humo kwa zaidi ya miezi miwili. Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa katika gazeti la TanzaniaDaima imeeleza uwepo wa RC Makonda nchini Afrika Kusini ndio sababu ya kushindwa kuhudhuria sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia ambapo ilitangazwa kuwa angekuwa mgeni rasmi katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Mwembeyanga. Kuondoka kwake nchini kumekuwa kwa kutatanisha wakati mamlaka husika zikishindwa kutoa taarifa kamili kuhusuana na safari yake. Wadadisi wa mambo wanahoji uhalali wa Makonda kupewa mapumziko hayo nje ya nchi huku serikali ilitangaza kuzuia ziara zote za watumishi nje ya nchi ili kubana matumizi. Kutokana na zuio la safari za nj

Tundu Lissu Afunguka Baada ya Kusikia Mwakyembe Amemzuia Kugombea Nafasi ya Rais wa TLS

Image
Anaandika Wakili Msomi Tundu Lissu: Waheshimiwa mawakili na wananchi wa nchi yetu. Nimesoma taarifa katika magazeti kadhaa ya leo kwamba Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison George Mwakyembe amenizuia kugombea nafasi ya Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS). Kama taarifa hizo ni za kweli basi naomba kuweka masuala yafuatayo wazi: (1) Waziri wa Sheria na Katiba hana mamlaka yoyote, kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha TLS na kanuni zake, ya kuzuia ama kuruhusu mwanachama yeyote wa TLS kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya TLS. Hivyo, kama kweli Dkt. Mwakyembe ametoa kauli hiyo, basi huo utakuwa uthibitisho wa ama upungufu mkubwa wa uelewa wa Sheria au hulka ya ukiukaji wa sheria (culture of impunity) ambayo imeshamiri sana katika utawala huu wa sasa. (2) Mamlaka pekee inayohusika na uchaguzi wa TLS ni Kamati ya Uteuzi (Nominations Committee) ambayo ilikwishafanya uteuzi wa wagombea wote kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa na Sheria na Kanuni za

VANESSA MDEE MIKONONI MWA POLISI

Image
Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia Mwanamziki Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya. Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita. Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi. Vanessa Mdee ni Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume Challenge na baadae kidogo wakati ananza kujikita kwenye muziki alikuwa ch

VIROBA VYA BILIONI 5 VYAKAMATWA DAR

Image
KATONI 32,634 za pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.18 zimekamatwa jana, katika operesheni maalumu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uingizaji, uuzaji na matumizi ya pombe hizo. Pombe hizo zimekamatwa katika operesheni inayoendelea katika mikoa mitatu ya Kikodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dar es Salaam ambayo ni Temeke, Kinondoni na Ilala. Akizungumza katika operesheni hiyo, Mkaguzi kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), John Nzila alisema walikamata katoni 14,393 za konyagi, katoni 9,964 za Vradmill, Zanzi 31 na Valeur. 268. Alisema mzigo huo ulikutwa katika ghala la Loverira Enterprises lililopo Kimara Temboni na kwamba mzigo huo umezuiwa kwa hatua zaidi. Kwa upande wake Mwanasheria Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Suguta alisema kuwa walikamata katoni 7,000