RAIS MUSEVENI ATEMBELEA VIWANDA VYA BAKHRESA LEO JIJINI DAR
Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara ...