SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUANZISHA DESTURI YA KUNUNUA KAZI ZA WASANII
Serikali
imewataka wananchi kuanzisha desturi ya kununua kazi za wasanii, kwakuwa
ndiyo njia pekee inayoweza kuwanufaisha kwa kazi wanazozifanya.Wito huo
umetolewa wiki hii na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa
tovuti a Afro Premiere, iliyoanzishwa kwa lengo la kuuza video za muziki
za wasanii.Alisema mpango huo unaweza kuwa ni moja ya mikakati muhimu
ya kupambana na wezi wa kazi za wasanii, kwakuwa video za muziki
zitakuwa zikipatikana kwenye mtandao huo peke yake kwa kipindi maalum na
hivyo kuingiza pesa zinazoenda kwa msanii, serikali na watayarishaji
moja kwa moja.
Pia
alidai kuwa kwakuwa Afro Premiere itakuwa ikiweka nyimbo za Kiswahili
zaidi, itasaidia kukikuza zaidi Kiswahili, ambacho ni cha 10 kati ya
lugha elfu sita duniani na kuahidi kupitia wizara ya mambo ya nje,
wizara yake itawaunganisha na Watanzania waliopo nje ya nchi.
Prof Ole Gabriel amewataka wasanii wao wenyewe kuunga mkono mpango huo sababu ndio njia pekee ya kuufanya ufanikiwe.
“Mpango
huu utafanikiwa kama ninyi mkiwa sehemu ya mpango huu, kama ninyi
wenyewe tena mkianza kuwa na kona kona na kuupiga vita, basi mpango huu
utaonekana feki na utashindikana,” alisema.
Hadi sasa
kuna video mbili mpya zilizowekwa kwenye Afro Premiere ambazo ni Go Low
ya G-Nako na Jux pamoja na K wa Roma na Baghdad. Mashabiki wanaweza
kununua nyimbo hizo kwa shilingi 300 tu kwa kutumia simu zao.
Kuiona video ya Go Low, bofya link hii>>>http://afropremiere.com/prevideo/1487839158_afropremiere.
Comments
Post a Comment