RC MAKONDA AELEZA KILICHOMFANYA ATAJE MAJINA YA WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa uamuzi wa kuwataja hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya ni kutokana na maombi ya Watanzania waliyayotoa wakati wa serikali ya awamu ya nne. Makonda alisema kuwa licha ya watu wengi kupaza sauti zao wakitaka watuhumiwa wa dawa za kulevya watajwe hadharani, lakini Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete yeye hakuwataja huku akiacha vyombo husika vifanyekazi zao kwa usiri. Lakini kwa upande wa serikali ya awamu ya tano, waliamua kuwataja watuhumiwa hao ikiwa ni kujibu maombi ya kile watanzania walichokitaka tangu kipindi cha nyuma, alisema Makonda jana akiwa kwenye semina ya Walimu Wanaosomesha Quran Tanzania (JUWAQUTA). Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam. “Mzee Jakaya mlimpigia kelele taja, taja, taja, taja, sasa tulipoingia sisi tukaona wacha tufanye kama