MZEE WA UPAKO NAE AFUNGUA HAYA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA
Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony
‘Mzee wa Upako’ amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao
wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Amefunguka
na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati
mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na
watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake.
Mchungaji
Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI
kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano.
“Mimi
ni mhanga wa dawa za kulevya mwaka 1997 nilituhumiwa kuwa nauza madawa,
lakini wale askari walikuwa wastaarabu, waliniandikia samasi nikafika
kutoa maelezo yangu, lakini baadaye niliwaambia kuwa wao ni polisi
wafanye uchunguzi wao, walifanya uchunguzi na kugundua mimi sihusiki,
watu walifuatilia na kugundua siyo kweli, na kila mtu akajitoa kwenye,
ilionekana kuwa ni wivu tu, ila mbaya zaidi ile taarifa kuwa niliitwa
polisi kwa madawa ya kulevya ilivuja, hadi wachungaji wenzangu
walininyanyapaa, nikivaa suti au nikiendesha gari kila anajua ni pesa za
madawa” alisema Mzee wa Upako
Mzee
wa Upako ameshauri vita ya dawa za kulevya kwa watu wanaotuhumiwa ni
bora viongozi wangetumia njia za kipolisi kuwataka kufika polisi kwani
kutumia njia ya magazeti inaweza kushusha heshima ya baadhi ya watu
ambayo wameijenga kwa miaka mingi.
“Mimi
kutokana na tuhuma zangu kuvuja kuwa niliitwa polisi kwa madawa ya
kulevya niliishi miaka saba watu wananinyayapaa, tena hiyo ni tuhuma tu.
Imenichukua miaka saba kusafisha jina, nimekuja kuanza kusafisha jina
mwaka 2005 hivi”
Mchungaji
huyo alisema hata yeye binafsi anachukia sana dawa za kulevya kutokana
na madhara yake kwa jamii, hivyo hawezi kuthubutu kujihusisha nazo wala
hawezi kuunga mkono watu wanaofanya shughuli hizo kwa kuwa dawa za
kulevya zinaua kizazi cha maendeleo na taifa kwa ujumla.
Comments
Post a Comment