Posts

MSANII NUH MZIWANDA AFUNGUKA MENGINE KUHUSU SHILOLE

Image
MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa japo kuna tetesi zinaenea mtaani kwamba amerudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ suala hilo halina ukweli wowote ndani yake na wala hafikirii kabisa kurudiana na mwanadada huyo. Tetesi za Nuh kurudiana na Shilole zilianza kuvuma baada ya kusambaa kwa kipande cha video kilichowaonesha wakipatanishwa wakati wakiwa kwenye safari za Tamasha la Fiesta na watu kujiongeza kuwa wamerudiana. “Kilichotokea ni kwamba mimi na Shilole tumeondoa tofauti zetu za kibinadamu ambazo tulikuwa nazo baada ya kuachana. Lakini kuhusu kurudiana hahitakuja kutokea hata siku moja na siwezi kurudi nyuma kwenye hili maana nina mpenzi wangu ninayempenda,” alisema Nuh.

JAJI CHANDE: NAFURAHI KUUACHA MUHIMILI WA MAHAKAMA KATIKA HALI NZURI

Image
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamedi Othman Chande amezitaka mahakama kufanya kazi kwa kuendana na kasi ya awamu ya tano pamoja na kufuata maadili ya taaluma ya sheria katika kutoa haki na sawa kwa wakati na kwa watanzania wote. Jaji Mkuu Mstaafu - Mohamed Chande Othman Jaji Chande ameyasema hayo mara baada ya kuapishwa kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma ambapo amesema kuwa kuongezeka kwa uwazi katika shughuli za mahakama kutasaidia sana katika kuendeshwa kwa kesi na kuamuliwa kwa wakati na watendaji wake. Amesema anafurahi anauacha muhimili wa mahakama katika hali nzuri huku akiwataka watendaji kuendeleza juhudi za kuboresha mifumo taratibu na sheria ili kutoa nafasi zaidi kwa kesi nyingi kushughulikiwa kwa haraka ikiwemo usikilizwaji wa kesi. Akizungumzia kuhusu mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambao ameuacha amesema kuendelezwa kwa mpango huo kutasaidia kuharakisha usikilizaji wa kesi, kuongeza mfumo wa usikilizwaji wa kesi pamoj

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA PROFESA IBREAHIM HAMISI JUMA KUWA KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju wakiwa katika

SABABU ZA EDWARD LOWASSA KUKAMATWA NA POLISI JANA

Image
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana alikamatwa na polisi mkoani Geita akituhumiwa kufanya mkutano bila kibali.  Lowassa, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alikuwa njiani akitokea mkoani Kagera, ikiwa ni mwendelezo wa ziara za viongozi wa chama hicho katika kanda zake kutekeleza Operesheni Kata Funua inayohusisha mikutano ya ndani. Hata hivyo, aliachiwa jana jioni.   Akiwa ameongozana na viongozi na makada wa Chadema, Lowassa aliingia Geita saa 9:30 alasiri na kupokewa na umati wa wananchi waliojitokeza eneo la Nyankumbu, tayari kwa safari ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Nkome.  Viongozi wengine waliokuwamo kwenye msafara huo ni Profesa Mwesiga Baregu, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Hamis Mgeja, ambaye ni kada wa chama hicho.  Msafara huo uliokuwa wa magari matano, ukisindikizwa na pikipiki na wafuasi kadhaa wa chama hicho, ulipitia makutano ya barabara

WAZIRI SIMBACHAWENE: “RUKSA WENYEVITI SERIKALI ZA MITAA KUTUMIA MIHURI

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa muda kwa waraka uliotoa muungozo wa matumizi ya Mihuri kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji leo jijini Dar es Salaam. Na Beatrice Lyimo-MAELEZOSerikali imesitisha waraka wa muongozo uliotolewa kuhusu matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa Mitaa na vijiji mpaka pale itakaposhirikiana na kukubaliana namna bora ya kuendesha masuala ya kuhudumia wananchi.Akizungumza na baadhi ya wenyeviti wa mtaa, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amewataka wenyeviti wa mitaa nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.Mhe.Simbachawene alisema kuwa nia ya kusitisha waraka huo ni kuweka utendaji mzuri baina ya Serikali na watendaji wake wa chini.“Utaratibu uliopo uendelee mpaka pale Serikali itakapotoa utaratibu mwingine wa matumizi mbalimbali ya mihuri hiyo baada ya

Emmanuel Mbasha asema bado anamuhitaji mke wake Flora ingawa anadai amezaa nje ya ndoa

Image
Msanii wa muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha amesema bado anamuhitaji aliyekuwa mke wake Flora Mbasha ingawa anadai tayari ameshazaa nje ya ndoa na mwanaume mwingine. Muimbaji huyo amedai ameshafanya jitihada mbalimbali bila mafanikio kwa kipindi cha miaka miwili ili kurudiana na mama watoto wake huyo. “Moyo wa kurudiana nilikuwa nao sana, tena sana, ikiumbukwe mambo yametokea 2014, mwaka huo mzima nilikuwa namuomba Flora rudi nyumbani tuendelee na maisha, 2015 nikaendelea kumuomba rudi nyumbani tuendelee na maisha. Tumeitisha vikao vya kila aina ili kusuluishwa lakini bado amekuwa mgumu lakini nadhani tayari alishapanga haya yatokee ndio maana akaamua yeye kuniacha mimi nilikuwa sina mpango huo,” Emmanuel Mbasha alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV.. “Mimi sijaachana naye, sema tumetengana na kipindi tumetengana amepata mtoto labda kuna kitu anaogopa, lakini mimi sina tatizo naye, Flora mimi nakuhitaji rudi nyumbani tuendelee na maisha,” aliongeza. Muimbaji h

MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MAPINDUZI YALIVYOFANYIKA LEO ZANZIBAR

Image
Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha uwezo wao wa kupigana bila silaha katika Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye wawnja wa Aman Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionyesha jinsi matofari yanavyoweza kuvunjwa juu ya kichwa katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwa amelala juu ya misumari huku wenzake wakipita juu yake ikiwa ni moja ya maonyesho ya ukakamavu yaliyoonyeshwa na Makomandoo hao katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 12. 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA SHINYANGA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 53 MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwasalimia wananchi wa Shinyanga waliofika katika uwanja wa mpira wa Kambarage katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar mkoani humo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kwaya ya KKKT Shinyanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MWIGUMBI-MASWA (50.3) MKOANI SIMIYU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka watatu kutoka kulia Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa wakwanza kulia pamoja na viongozi wengine.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengiene  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3). Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS  Mhandisi Cristianus Ako kabla ya kuweka jiwe la msingi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Maswa kabla ya kuweka jiwe la

MAJALIWA AFUNGUA UKUMBI WA SACCOS YA MELI NNE ,ZANZIBA NA KUZUNGUMZA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shamrashamra za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar januari 11, 2017. Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Kassim Majaliwa , viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd wakati alipozungumza baada ya Waziri Mkuu kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar Januari 11, 2017.  Baadhi ya wananchama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua ukumbi wa SACCOS hiyo Januari 11, 2017. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar baada ya kufungua ukumbi wao Januari 11, 2017. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd. Waziri Mkuu, Kassim Maj